Walimu wa Taifa Secondary watanyanyaswa sana na wakubwa wao wa kazi

Walimu wa Taifa Secondary watanyanyaswa sana na wakubwa wao wa kazi

Teko Modise

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
2,331
Reaction score
7,733
Kwa matokeo waliyoyapata katika mtihani wa taifa wa kidato cha nne yaliyotangazwa leo, natabiri walimu wa shule hiyo watanyanyaswa mno na wakubwa wao wa kazi.

Yaani watafokewa kuanzia na wazazi,diwani wa kata yao, mbunge, afisa elimu kata, afisa elimu wa wilaya, afisa elimu wa mkoa, wizara za elimu na tamisemi, mkuu wa wilaya ya temeke, mkuu wa mkoa wa dar, kamati ya bunge ya elimu (kama ipo) nk

Kama binadamu wa kawaida nimejikuta nimewaonea huruma, maana wanafunzi karibia 470 wana daraja sifuri.

Poleni sana walimu sio kwahyo mitoto ya temeke!
D1B6E25B-697E-464D-BD85-44F8BF3ACB2C.jpeg
 
Kwa matokeo waliyoyapata katika mtihani wa taifa wa kidato cha nne yaliyotangazwa leo, natabiri walimu wa shule hiyo watanyanyaswa mno na wakubwa wao wa kaz...
kwa idadi hiyo ya wanafunzi, unaona kabisa hakutakuwa na uwiano na idadi ya walimu waliopo...

Ukijumlisha na aina ya wanafunzi wenyewe, ni hatari!

Picha kinaanza jama tu nimepanda gari na mwanafunzi anatoka shule (anavyodai tuition) ananuka pombe, gari zima tunamshangaa... mtu kama huyu akipata 4 tu, tunaisubiri dalili ya mwisho ya kumuona masihi!
 
Mitoto yoote hio hakuna give 1 hata moja na ni Dar salaam sehemu wanasoma tuition really?
... mwongozo wa Wizara ya Elimu unakataza tution; ukikamatwa unafundisha hiyo kitu! Ole ni wako! Tena unasisitiza wakati wa likizo ni kwa ajili ya watoto kupumzika ni kosa kupewa kazi za kufanya kipindi cha likizo! Bongolala!
 
Ifikie mahali shule kama haiwezi ku perform haina haja ya kuendelea kuwepo. Madarasa yafanywe hostel kwa ajili ya shule jirani ambayo ina perform vizuri. Hatuna haja ya kuwa na kundi kubwa la wajinga waliosoma o'level.

Mtu kama hana uwezo toka la 7 anajulikana tu. Atafte mishe zingine za kufanya sio kupoteza muda shule.
 
Back
Top Bottom