Walimu wa Taifa Secondary watanyanyaswa sana na wakubwa wao wa kazi

Walimu wa Taifa Secondary watanyanyaswa sana na wakubwa wao wa kazi

Hesabu zinatusumbua mkuu yaani hata kujumlisha tunasumbuka tunawacheka waliopata Zero kweli...
Tuishi maishi ya ki zero zero kila kona, hata kushughulisha akili hata kidogo ni zero
Zero
Zero
Lakini kwa uzinzi tunachezea 80% to 100%🤣🤣
 
Kwa hiyo miaka mine walikua wanafundishwa nini? Wangeweza sema ndio hivyo Watendaji wameitelekeza shule
Sasa secondary mwalimu aanze kufundisha a, e i o u. Mwalimu anafundisha muelewe msielewe mtajua wenyewe kwa sababu kosa si la mwalimu .
 
Sasa secondary mwalimu aanze kufundisha a, e i o u. Mwalimu anafundisha muelewe msielewe mtajua wenyewe kwa sababu kosa si la mwalimu .
Hapana Mkuu mimi niliwahi fanya kazi Handeni hapo Halmashauri ila kwa kuwa napenda vijana wapende hesabu nikawa muda wa jioni naenda kuwapa Darasa la hesabu kidato cha Tatu na cha Nne nilikaa pale miaka miwili tuu ila niliona tofauti maana tulikuwepo kama wahasibu wanne baada ya mazoezi ya Mpira tunawapiga darasa vijana mpaka Geog na English ili waone urahisi wa shule wapo waliofanya vizuri na waliobadilika ndio maana najiuliza hao miaka yote minne walikua wanasoma nini?
 
Sometime kuwa na li-toto ambalo halijitambui limeenda shule kufanya nini ni tatizo,,,angalia hizo zero za hiyo mitoto,,hivi utawaza kweli hao watoto walienda kusoma au yalienda kukua tu huko.
 
Aisee! Inasikitisha sana sema basi,Zama za digitalis kila kitu kipo uchi unapata sifuri 400 kweli vijana wa siku hizi ni vilaza wa hovyo sana....waalimu nao wajitafakari,Mkuu wa shule na wenzake wawajibike ili iwe fundisho kea wengine wanaokula mishahara ya bure bure....kama mwalimu anawajibika kweli sidhani kama unaweza pata matokeo ya hivi.
 
Darasa moja wanafunzi 1000 duh sehem nyingine si shule nzima sasa hao form one mpaka three wakoje...si hatari he ratio ya walimu na wanafunzi ikoje maana wqnafunzi 1000 kwa ratio ya wanafunzi 45 darasani angalau wanaohitajika kitalamu haya ni madarasa 20. Form four tu ilitakiwa kuwa na madarasa 20 ....Sasa tungeanza kuhukumu hapa kabla ya kulaumu walimu
 
Inakuwaje shule iwe na wanafunzi zaidi ya 1,000 kidato kimoja?
Mazingira ni rafiki?
Kuna wali na miundombinu muhimu?
Tuanzie hapa
Na hawa ni waliofika form four wengi wameacha wakiwa madara ya form 1,2,3
Na kufel form 2
Ukienda hapo diplomacia watoto nyomi mwalimu wa physics
Form 1 hadi four...mpaka mwaka jana labda kama mwaka huuwameongeza.
Ni msiba
 
Na hawa ni waliofika form four wengi wameacha wakiwa madara ya form 1,2,3
Na kufel form 2
Ukienda hapo diplomacia watoto nyomi mwalimu wa physics
Form 1 hadi four...mpaka mwaka jana labda kama mwaka huuwameongeza.
Ni msiba
Hatari sana
 
Kwa matokeo waliyoyapata katika mtihani wa taifa wa kidato cha nne yaliyotangazwa leo, natabiri walimu wa shule hiyo watanyanyaswa mno na wakubwa wao wa kazi.

Yaani watafokewa kuanzia na wazazi,diwani wa kata yao, mbunge, afisa elimu kata, afisa elimu wa wilaya, afisa elimu wa mkoa, wizara za elimu na tamisemi, mkuu wa wilaya ya temeke, mkuu wa mkoa wa dar, kamati ya bunge ya elimu (kama ipo) nk

Kama binadamu wa kawaida nimejikuta

Hii shule ilikuwa na wanafunzi 1,032 waliokuwa kidato cha 4 mwaka 2022. Jiulize ilikuwa na walimu wangapi? Kulikuwa na vitendea kazi? Madarasa yaliwatosha. Kwa wastani hii form four tu ina hao wanafunzi 1,032 kuna form 1, 2 na 3. Kama tukichukulia huo ndiyo wastani wa kila stream ina maana hii shule ina wanafunzi 4,000 plus.

Kwa maana hiyo inabidi iwe na walimu walau 100 kwa wastani wa wanafunzi 40 kwa kila darasa. Kabla ya kuwahukumu walimu nadhani tukaangalie kama shule ina resources za kutosha kwa maana ya walimu, mazingira na vitendea kazi.
 
Wakufunzi/walimu tupo tayari kupokea lawama zote ila wakumbuke wakati wakuja kutulaumu je wamafanyia kazi maoni/mapendekezo yetu?
Tupo tauari kwenda watakapotuhamishia kama adhabu ila hata hao watakaoletwa hapa watafanya kama sisi tu
Binafsi siwezi mlaumu Mwalimu.

Wakulaumiwa ni wazazi, kwanini hawafatilii maendeleo ya watoto wao?

Kwanini wasiwapeleke shule nzuri?

Kwanini wanakubali vya bure?
 
Back
Top Bottom