Walimu wa Taifa Secondary watanyanyaswa sana na wakubwa wao wa kazi

Walimu wa Taifa Secondary watanyanyaswa sana na wakubwa wao wa kazi

Daah Div 0 wanafunzi wa kiume zaidi ya 400 aisee hizi shule zina wakaguzi kweli maana matokeo hayo sio yamekuja tuu kwa ghafra...
... garbage in, garbage out! Hiyo ndio kanuni. Wasiojua kusoma, kuandika, wala kuhesabu wanachaguliwa kuingia kidato cha kwanza unategemea nini? Tusipoboresha kule chini tusitegemee tofauti!
 
Wanafunzi wengi sana kuwa form four kwenye shule moja, hapo lazima utakuta uwiano na walimu hata hauendani kutosheleza mafunzo etc

Lazima waulizwe kibusara tatizo wanaloona hapo shuleni, wafanye majadiliano.

Ila wanafunzi ni wengi sana sanaaaa
 
... garbage in, garbage out! Hiyo ndio kanuni. Wasiojua kusoma, kuandika, wala kuhesabu wanachaguliwa kuingia kidato cha kwanza unategemea nini? Tusipoboresha kule chini tusitegemee tofauti!
Ina maana kwamba miaka yote minne shule ya mjini kabisa walimu wazuri wapo mtaaani wengine wana Center zao wameshindwa kufanya kitu hapo au Utani huu Mkuu...unakuta shule ipo Nanjirinji huko inatoa Div 1 ya mjini wanajazana na Zero kweli yaani Necta wanenda kwa kupanda bus moja tuu...
 
... mwongozo wa Wizara ya Elimu unakataza tution; ukikamatwa unafundisha hiyo kitu! Ole ni wako! Tena unasisitiza wakati wa likizo ni kwa ajili ya watoto kupumzika ni kosa kupewa kazi za kufanya kipindi cha likizo! Bongolala!
Kwa walimu mashuleni na muda wa shule
 
Ina maana kwamba miaka yote mine shule ya mjini kabisa walimua wazuri wapo mtaaani wengine wana Center zao wameshindwa kufanya kitu hapo au Utani huu Mkuu...unakuta shule ipo Nanjirinji huko inatoa Div 1 ya mjini wanajazana na Zero kweli yaani Necta wanenda kwa kupanda bus moja tuu...
... iko hivi, mwongozo wa Wizara unaharamisha kabisa tuition au watoto kurundikiwa kazi za kufanya wakati wa likizo! Mmesahau maelekezo ya Waziri Ummy Mwalimu akiwa TAMISEMI? Likizo ni wakati wa watoto wetu wapendwa kupumzika na kupumzisha akili zao na sio vinginevyo. Ni kosa kabisa walimu kufundisha tuition!
 
Kwa matokeo waliyoyapata katika mtihani wa taifa wa kidato cha nne yaliyotangazwa leo, natabiri walimu wa shule hiyo watanyanyaswa mno na wakubwa wao wa kazi.

Yaani watafokewa kuanzia na wazazi,diwani wa kata yao, mbunge, afisa elimu kata, afisa elimu wa wilaya, afisa elimu wa mkoa, wizara za elimu na tamisemi, mkuu wa wilaya ya temeke, mkuu wa mkoa wa dar, kamati ya bunge ya elimu (kama ipo) nk

Kama binadamu wa kawaida nimejikuta nimewaonea huruma, maana wanafunzi karibia 470 wana daraja sifuri.

Poleni sana walimu sio kwahyo mitoto ya temeke!
View attachment 2499396
Inakuwaje shule iwe na wanafunzi zaidi ya 1,000 kidato kimoja?
Mazingira ni rafiki?
Kuna wali na miundombinu muhimu?
Tuanzie hapa
 
Tuilaumu Serikali kwa kulazimisha watu waende Sekondari bila kujua kusoma na kuandika
Tuwalaumu wazazi kwa kutoweka muda wao kufatilia maendeleo ya watoto
... wazazi walishaelezwa kazi yao ni moja tu; KUFYATUA. Baada ya hapo serikali ita-take responsibilities nyingine zote. Wazazi wasilaumiwe kwa hili; wametekeleza jukumu lao la kufyatua vizuri sana. Mashule yamejaa hadi vyumba vya madarasa havitoshi tena kwa muda mfupi sana.
 
... iko hivi, mwongozo wa Wizara unaharamisha kabisa tuition au watoto kurundikiwa kazi za kufanya wakati wa likizo! Mmesahau maelekezo ya Waziri Ummy Mwalimu akiwa TAMISEMI? Likizo ni wakati wa watoto wetu wapendwa kupumzika na kupumzisha akili zao na sio vinginevyo. Ni kosa kabisa walimu kufundisha tuition!
OK tuition ni kosa kwa hiyo walikua wanasoma nini kwa miaka minne mkuu na pia hiyo shule ipo mlangoni kwao hata hao Baraza ina maana walikua hawajui kinachoendelea hapo mpaka kipindi cha Mtihani umewahi ona wapi Div 0 karibu 600 huko..
 
... Mkuu hayo aulizwe Waziri TAMISEMI na viongozi wenzake. Mimi kazi yangu ni moja tu; KUFYATUA na kuwapelekea vijana wasomeshe!
 
Back
Top Bottom