Walimu wa Taifa Secondary watanyanyaswa sana na wakubwa wao wa kazi

Walimu wa Taifa Secondary watanyanyaswa sana na wakubwa wao wa kazi

Kwa matokeo waliyoyapata katika mtihani wa taifa wa kidato cha nne yaliyotangazwa leo, natabiri walimu wa shule hiyo watanyanyaswa mno na wakubwa wao wa kazi.

Yaani watafokewa kuanzia na wazazi,diwani wa kata yao, mbunge, afisa elimu kata, afisa elimu wa wilaya, afisa elimu wa mkoa, wizara za elimu na tamisemi, mkuu wa wilaya ya temeke, mkuu wa mkoa wa dar, kamati ya bunge ya elimu (kama ipo) nk

Kama binadamu wa kawaida nimejikuta nimewaonea huruma, maana wanafunzi karibia 470 wana daraja sifuri.

Poleni sana walimu sio kwahyo mitoto ya temeke!
View attachment 2499396
Nawaza hiki kizazi miaka 10 ijayo.. Tanzania itakuwa na watu wajinga mno na hiki ndio ccm wanachotaka
 
Badala ya kuboresha elimu wanakimbilia kuficha ranking.......hivi hii nchi itakalika kama watajaa vilaza watupu, maana kustaarabika kunaendana na uwezo wa kiakili.
 
Waalimu Wana kazi kweli lawama zote zitashushwa kwao!!bila kuangaliwa Mambo mengine nje ya waalimu ,jamani hata maadili kwa watt ni shida siku hizi,mwalimu akitoa adhabu kwa mwanafunzi (sio zile zilizo kinyume) mzazi anakuja juu na wakati mwingine atamtafutia zengwe Hadi kwenye mitandao ,waalimu inafikia mahali wanawaogopa wanafumzi kuwapa adhabu hata zile zinazoruhusiwa ,watt wanakuwa na kiburi,nidhamu kwa waalimu wao zero,matokeo yake mwalimu anaamua kutimiza tu wajibu wa kuingia kwenye vipindi Basi,hajisumbui na kutumia weledi wa ziada juu ya wanafunzi wake.tutegemee taifa la watt wa ajabu kweli.Kuna Mambo kweli yamepitwa na wakati,lakini yapo Mambo sio ya kusema yamepitwa na wakati,hasa elimu na malezi ya mtt kielimu.mfano zamani s/msingi unaletewa paper ya mathematics maswali 50 ,ukokotoe yote mwenyewe ,upate majibu sahihi,unadhani tuliweza hvhv ,NI nidhamu kwa waalimu ilikuwa ya Hali ya juu mno.yaani unalazmika wakati mwingine ulirudi home unatorika nyumbani kukwepa wazaz wasikupe kazi ,halafu unaenda kupanda juu ya mti na vitabu vyako au maswali ya mitihani ,una solve huko juu ,kujikumbusha ,ili tu kujihami na bakora za shuleni ,maana ilikuwa kila kosa moja kwenye mtihani,fimbo moja .watt wetu wa Leo wangeyaweza haya !!!
 
... Mkuu hayo aulizwe Waziri TAMISEMI na viongozi wenzake. Mimi kazi yangu ni moja tu; KUFYATUA na kuwapelekea vijana wasomeshe!
Mkuu nina hasira nakuuliza maswali magumu samahani bhana ujue umenichekesha sana ujue...
 
Daah Div 0 wanafunzi wa kiume zaidi ya 400 aisee hizi shule zina wakaguzi kweli maana matokeo hayo sio yamekuja tuu kwa ghafra...
Hamna div 0 mkuu.
No div 1 mpaka 4
Sifuri haipo kwenye kundi la div
 
Wakufunzi/walimu tupo tayari kupokea lawama zote ila wakumbuke wakati wakuja kutulaumu je wamafanyia kazi maoni/mapendekezo yetu?
Tupo tauari kwenda watakapotuhamishia kama adhabu ila hata hao watakaoletwa hapa watafanya kama sisi tu
 
Back
Top Bottom