Walimu wamegeuza pesa ya chakula mashuleni kuwa posho zao wanajilipa

Walimu wamegeuza pesa ya chakula mashuleni kuwa posho zao wanajilipa

Halafu uweke wazi huwa mnachangia shilingi ngapi ya chakula kiasi cha kutaka mtoto wako ale chakula chenye ubora, na mtoto wako ashibe?

Na hicho chakula anachokula huko shuleni ni chakula gani? Je, matumbo yanalingana?

Ushauri wangu kwako;
1. Acha malalamiko yasiyo na kichwa wala miguu.
2. Jitahidi kuhudhuria vikao vya wazazi na walimu shuleni (PTA)
3. Usipende kuwalea watoto wako kama mayai! Utawaharibu. Yaani kwa sababu mtoto anakula wali nyama kila siku nyumbani, basi unataka na shuleni ale chakula cha aina hiyo hiyo. Jambo hilo haliwezekani.
Wanachanga sh 700-1,000..Mia saba hadi elfu moja tena kwa mbinde.
Na msimamizi ni kamati ya wazazi waliyoichagua wenyewe.
Walimu walishapigwa marufuku kupokea hela za wanafunzi.
Mpaka mchango unaitishwa huko shule za kata lazima wawe wamefanya kikao na kamati iombe kibali manispaa cha kuitisha mchango.

Huyu alipata duara.
 
Sikuwahi kukubali wala kupenda hili swala la pesa za chakula, nilijua tu ni kuja kugombanisha walimu na wazazi....
Serikali/viongozi hawajawahi kusimama kutamka popote hili swala zaidi ya kutoa tu waraka ambao unatakiwa kutekelezwa tena kwa 100% hivo Kwa kuwaambia wazazi watoe hela ni kama vile walimu ndio wanataka..kwa hili serikali imeamua kugombanisha tu.
Somehow. Lkn makusanyo ya hela yanafanywa na kamati ya wazazi kwa ruhusa ya mkutano wa wazazi. Na kwann wachangie bila kujua chimbuko la mchango?!?!?! SI WAMEAMBIWA ELIMU BURE
 
WALIMU WANAIIBA MAHARAGE, WANAIIBA MKAA NA UNGA WA SHULE.

KUNA SHULE ANASOMA MWANANGU WA KIUME ANANIAMBIAGA KUWA WALIMU NA FAMILIA ZAO WANAPANGA FOLENI KULA CHAKULA CHA SHULE

WALIMU NI MASKINI SANA
 
WALIMU WANAIIBA MAHARAGE, WANAIIBA MKAA NA UNGA WA SHULE.

KUNA SHULE ANASOMA MWANANGU WA KIUME ANANIAMBIAGA KUWA WALIMU NA FAMILIA ZAO WANAPANGA FOLENI KULA CHAKULA CHA SHULE

WALIMU NI MASKINI SANA
Hata wewe uliepeleka watoto wako kwenye shule za walimu masikini halafu unawaponda walimu ndio masikini wa mwisho. Takataka kabisa.
 
Habari haijitoshelezi.....wapi ? Wanalipaje? Chakula gani wanapikiwa? Wanasharije? Etc
 
Kero kweli kweli,kila siku watoto wanakula makande,wakati huo majumban mchana hurejea kula,bora wangekuwa wanachangia kwa watoto wanaotoka maeneo ya mbali na shule.
 
Pendekezo ... Warudishe ratiba ya zamani,masomo yawe mwisho saa nane na nusu. Elimu itakuwa Bora kuliko hivi watoto wanafundishwa na njaa maana sio wote wanachanga chakula. Kwa suala la chakula shuleni serikali imefeli pakubwa labda watoe ruzuku za chakula ,lakini siyo wazazi ndio wachange. Wizara ya Elimu wajitafute wajipate waachie viti hivyo Kama haviwatoshi.
 
Kero, Waziri wa Elimu liangalie hili hali imezidi kuumiza wazazi.
Chakula chenyewe mtoto ashibi na usipompa mtoto pesa simu nyingi za walimu.
Chakula hakina ubora.
Elimu bure imegeuzwa elimu mchaka mchaka.
Hoja Zako zinamshiko Sana.

Shule za serikali especially za secondary wanatoza wanafunzi pesa za chakula 20,000 kwa mwezi.

Na hili ni lazima kulipa pesa hizo sio hiyari.
Secondary kiluvya,,gogoni sec na zingine.
 
Tanzania Kuna shule ngapi za sekondari na msingi Ndugu mtoa mlalamikaji?
Mfano wewe ungekuwa ndio wizara ungefahamu mlalamikaji anazungumzia sehemu gani ya nchi?
Je una watoto kila shule hapa nchini labda hadi ukafahamu kuwa shule zote zinachangisha?
Je unafahamu agizo la watoto kupata chakula shuleni?
 
Kama kuna kitu kinatupasua kichwa walimu ni hili la kulazimishwa eti tuhakikishe watoto wa watanzania wanakula shuleni!! Yaani alieliwaza hili na alaaniwe maana mitanzania yenyewe ndio kama hii!!

Hela yenyewe ukipiga hesabu utakuta mtoto anakula shilingi 800 kwa siku hapo imejumlishwa hadi pesa ya mpishi, ila kupatikana kwa hiyo hela ni mbinde maana wazazi ndio wana akili kama hizi eti tunagawana pesa zao!! Hizo pesa zinakusanywa na kuratibiwa matumizi yake na wazazi wenyewe, sasa walimu siji mnawalaumu wa nini🙆🙆🙆
 
Hoja Zako zinamshiko Sana.

Shule za serikali especially za secondary wanatoza wanafunzi pesa za chakula 20,000 kwa mwezi.

Na hili ni lazima kulipa pesa hizo sio hiyari.
Secondary kiluvya,,gogoni sec na zingine.
Suala la kula shuleni ni la lazima hivyo huo mchango ni lazima pia. Na nina hakika mliupitisha wazazi wenyewe kwenye vikao vyenu, unless ndio nyie hamuhudhurii vikao.

Lakini pesa hizo zipo chini ya usimamizi wa wazazi wenyewe.
 
Tafuta pesa umsomeshe mtoto shule nzuri utakayo... Uampeleka mtoto shule ya elimu bure unalalamika hivyo..? Wewe hata nyumban kwako inaonekana watoto hawashibi...
 
Sikuwahi kukubali wala kupenda hili swala la pesa za chakula, nilijua tu ni kuja kugombanisha walimu na wazazi....
Serikali/viongozi hawajawahi kusimama kutamka popote hili swala zaidi ya kutoa tu waraka ambao unatakiwa kutekelezwa tena kwa 100% hivo Kwa kuwaambia wazazi watoe hela ni kama vile walimu ndio wanataka..kwa hili serikali imeamua kugombanisha tu.
Wao ni wanasiasa washatangaza elimu ni bure, hivyo hawataki kujichafua. Kwahiyo tumebebeshwa sie hili la chakula tupambane nalo.
 
Back
Top Bottom