Tetesi: Walimu wamegeuza Shule za Serikali kuwa Vitega Uchumi vyao

Nimeliandika mara zote hili. Kero kabisa. hasa hawa walimu wa shule za msingi.
CCM ndio wanao haribu elimu hasa Kwa walimu WA shule za msingi na sekondari kila siku wanaongopewa maslaji Yao wewe unataka wafanye nini!?CCM ni majangili ya nchi
 
Pesa za serikali hazitoshi
 
Huwa wanawadai Hela Kwa ajili ya Nini? Huwa wanasema mtoto aende na Hela halafu wanazifanyia Nini?
 
Shule huwa inapokea shilingi ngapi Kila mwezi?
 
Hakuna elimu bure
 
Mleta hoja ana kitu cha msingi naomba asikilizwe.

Asipuuzwe.
 
Acheni kuzaa watoto bila mpango kwa kisingizio kila mtoto anakuja na sahani yake,aya tuambie jumla ni sh ngapi anadaiwa?
Mtoto uzae wewe alafu utegemee kulipiwa,narudia zaeni kwa mipango
Utanisamehe bure ila haya yote yanaletwa na umaskini sidhani kama wanadai hela nyingi hivo
 
Wanafanya remedial bure asubuhi na jioni ,hapa katani kwetu wanafanya mock na wanaenda kusahihisha bure,mitihani yote eti wanalipa elfu tano tena kwa mbinde,kuna watu wana moyo mi sifanyi kazi hiyo
 
Nani kakudanganya, huko nako zipo field extra time n.k zote hizo hulipiwa, nimesonesha huko watoto watatu, mmoja kasoma huko miaka 7, mwingine miaka 10, na wamwishoni miaka 3, katika hizo shule za 3M + sababu nako zipo program ambazo ni nje ya ada, acha kujitia ujinga.
 
Wanafanya remedial bure asubuhi na jioni ,hapa katani kwetu wanafanya mock na wanaenda kusahihisha bure,mitihani yote eti wanalipa elfu tano tena kwa mbinde,kuna watu wana moyo mi sifanyi kazi hiyo
Kama una pesa nenda vituo vya watoto yatima jichukulie watoto kadhaa uwasomeshe, hivi ndivyo wafanyavyo wenye pesa.
 
Mimi naona shida ipo kwenye utaratibu, je mchango umefata utaratibu?wazazi wameshirikishwa? Je mchango umefanya shughuli iiyokusudiwa? Toka waanze hiyo michango ufaulu unapanda? Watoto wanasemaje juu ya ufundishaji wa walimu wakujitolea na ufundishaji wa vipindi vya ziada.

Kiukweli shule zetu Zina Hela mbaya sana. Unakuta shule inapewa 400,000 Kwa mwezi ya uedeshaji. Hapo Kuna posho ya mkuu ya mwezi 250,000 inabaki 150,000 . Haya hapo Kuna mlinzi anaipwa 100,000 Kwa mwezi. Bado una walimu wa kujitokea wa sayansi na maths wanatakiwa kupewa hata 100,000 ya sabuni na chakula, Bado kulipa umeme na maji. Inafikia hatua mkuu anatumia Hela binafsi kuendesha shule.
Na hapo inabidi kutunza Hela kwajil ya mitihani na miterm tests. Walimu wengi wanafanya kazi za kutoka kwenda halmashaur au mkoani bila kulipwa posho maana Hela hakuna.

Fanya research ndogo angalia Hali za walimu wengi hata wakuu wa shule za kata, angalia kama nyumba zao na usafiri kama wanao, utagundua hawana maendeleo yoyote. Na michango mingi inaenda Kwa shughuli husika.
 
Sasa si amesema kwamba huko pa kulipia ni nafuu? Sasa kwanini anaacha nafuu anaenda kwenye gharama?
 
Zingatia haya yako ya mwisho.
 
Sasa,si umpeleke huyo Mwanao shule za private.
 
Kuna huyu Mkuu wa Oysterbay Primary ni noma kwa mlungula
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…