KERO Walinzi katika Mtaa wa Kidete, Manispaa ya Kahama wamekuwa kero kwa Wananchi, tunaomba msaada

KERO Walinzi katika Mtaa wa Kidete, Manispaa ya Kahama wamekuwa kero kwa Wananchi, tunaomba msaada

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari,

Naomba kutumia nafasi hii kuwasilisha kero kuhusu adha wanayopitia wakazi wa Mtaa wa Kidete, Manispaa ya Kahama.

Kwa muda sasa, wakazi tumekuwa tukivamiwa na kusimamishwa mara kwa mara barabarani na baadhi ya walinzi wa eneo hili. Badala ya kubaki katika maeneo yao ya kazi na kutekeleza majukumu ya kulinda maeneo wanayohusika nayo, wamekuwa wakisimama barabarani na kuzuia wapita njia, kuwapekua na kuwafanyia upekuzi bila kuwa na mamlaka ya kufanya hivyo.

Kadiri tunavyoelewa, walinzi hawa si askari wa doria wala hawana mamlaka ya kusimamisha na kupekua wananchi wanaopita barabarani. Hali hii imezua hofu na usumbufu mkubwa kwa wakazi na inaweza kusababisha taharuki au migogoro isiyo ya lazima.

Tunaomba mamlaka husika, hususan Jeshi la Polisi pamoja na viongozi wa serikali za mitaa, zilichukulie suala hili kwa uzito na kuchukua hatua stahiki ili kulinda usalama na haki za wananchi.
 
Back
Top Bottom