Walinzi wa kampuni ya SUMA JKT GUARD wana matatizo ya kisaikolojia

Dunia ya sasa si ya kusema usamehe.
 
Hakika mkuu.
 
Kwani wao ndio wenye stress tu peke Yao ?

Wajinga tu hao
 
Ila kusema kweli hawa jamaa hawako vizuri kisaikolojia kabisa, Nikiwa TIBA_UDOM ndio wanaletwa kwa mara ya kwanza et ikifika sa5 wanakuja Kwwnye madarasa wansema muda umeisha turudi Hostel, aseeh Mbaya zaidi et Mwanafunzi katoka usiku huko alipokuwa anazuiliwa asiingie hostel!!!
 
Usiombe uwakute wale wanaopangwa kulinda ATMs, wanapiga mizinga hatari
 

mkuu nadhani hii ilitokea kituo cha shekilango cha UDART mana pale walikuwa wawili sasa walitaka kupita kibabe bila kulipa nauli kumbe nao wale walinzi wa mwendokasi wamevaa kiraia lakina nadhani nao ni wanajeshi wale mana walianza kuwapiga mitama mpaka raia wakaja kuingilia kati ili waachiwe huru

sas ndio mmoja wa wale walinzi wakawa wanawapa habari raia kuwa hawa wanataka kupita bure tena kwa mabavu kama hawana hela wangeniomba kiustaarabu ili niwaruhusu wapite ila hawakufanikiwa kupita wakaenda zao

naunga mkono hoja kuwa hawa watu hawapo sawa kiakili mana pia wanapenda kutumi nguvu sana hata kwa wanafunzi wa vyuoni
 
Hawa hawa ndio watakuja kuleta mpasuko tu katka taifa, ni suala la muda.....


Yaani kuna uhuni hicho kikampuni cha ulinzi n kivuli cha watu fulani...

Kila kichwa kinaandikiwa kinalipwa kilo 5 halafu kinakuja kupewa kilo unusu.....

Wafikirieni kuwa nao n watu
 
... ni kakitengo fulani ka uzalishaji mmiliki akiwa JKT; mishahara yao inatokana na wanachozalisha - ulinzi, matofali, kokoto, maji ya Uhuru, n.k.
Duuu unaongea ukweli mtupu pia mtoa mada amesahau kuwa wengine wapewa ajira na taasisi nzuri km Tanapa,Tawa na Ncaa halafu wao wapo kiKK guard lazima stress

Sent from my SM-G531H using JamiiForums mobile app
 
Hahahaaa ngoja nikubali tu mkuu. Kwa vyovyote itakuwa umeshakutana nao kwenye kona ngumu.
Waliwahi niweka mtu kati kuanzia sa8 usiku Hadi sa3 asubuhi!! Utawala wa College of Education kisa chenyewe hakina kichwa Wala miguu, Mbaya zaidi mmoja wao akanipa namba yake aseeeh, Nilimtukana sijawahi tukana Wala kudharau kazi ya mtu Kama nilivyofanya kwa huyo, SUMAJKT
 
realy wana shida af na ao wanajiona ni wanajeshi kam wa jkt ilingalii ni coz ya miezi sita ndo inawafanya wanasumbua ila watawasumbua wasio wajua kwetu wata ungua na jua
 
Inawezekana ni kweli hawako sawa nakumbuka tukio moja

Kuna mmoja alipanda daladala kadaiwa nauli akavimba anataka kupigana na konda kwakua nilikua seat ya karibu na mlango nikashuka fasta kuachanisha, ikabd nimlipie nauli kwakua ni bei che tu nkashangaa ananibadilikia na mm ananiambia braza sijakuomba unilipie nauli na usiingilie ugomvi usio kuhusu..

ilibid nimpige biti ya hatar maana alikua hana ubavu wa kusukuma ngumi hata 3 mbele yangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…