Walinzi wa rais wetu fitness yao vipi?

mnachokitaka nyie ni mionekano ya vifua na sio utendaji kazi, IDD AMIN alikuwa komandoo mwenye mazoezi ya kutosha lakini alikuwa na kitambi, fanya uwaingilie katika jukum lao na mazoezi yako ya gym ili uone kitakachotokea mkuu
Ebu fatilia tu hata askari walio depo au maafusa wanafunzi walio mafunzo uone kama utamkuta mwenye kitambi,hawawez kuwa navyo sababu wanafanya mazoez na wanafanya mazoez ya kukimbia sana tu kwahyo hao jamaa muda wao wa nje ya kazi wanautumia kuweka miguu juu na kugonga bia na mbuzi ndio maana wamejaa matumbo
 
kwanini rais Bush alirushiwa kiatu akakikwepa yeye mwenyewe licha ya kuwa na walinzi makini wasio na vitambi? jibu tafadhali
Umenena vyema.
Kumbuka umbali aliokua amekaa Bush na walinzi wake na silaha aliyoamua kuitumia (ya kurusha kiatu) alirusha kutokea mbali.
halafu kumbuka umbali wa walinzi wa Mwinyi, Mpiga kibao na Mwinyi mwenyewe, jamaa alimfuata mtu na kugawa kelbu huku walinzi wapo hapo.

Chambua upya
 
Kwahiyo kwa wenzetu ni mbwembwe ila sisi ndo tunajua?
Watu wenye nia ya "kumdhuru" Rais huwa hawamsogelei kwa karibu, hivyo haihitaji kuwa na misuli ili kumlinda Rais.
Wenye misuli wanalinda "night clubs" mnawaita "mabaunsa".

Hawa walinzi wa Rais ni watu waliopewa mafunzo maalumu ya kufanya kazi ya kumlinda Rais, na kipimo kikubwa ni uwezo wa akili. Ndio maana utawaona mara zote wanapokuwa na Rais huwa wanawatazama watu kwa makini sana. Wamefundishwa kugundua hisia za wahalifu hata kwa kuwatazama tu. Hivyo ni kazi inayohitaji akili iliyotulia zaidi kuliko nguvu za mwili.

Tena fitness ya mtu haipimwi kwa kumwangalia kwenye picha. Muonekano wa mwili usikudanganye ukamfikiria mtu tofauti.
 
Pale kuna wanausalama zaidi ya 30, usidanganyike kwa kuwaona hao 2 hapo mbele, na kila unaemuona ana jukumu lake, amini usiamini kati ya hao unaowaona kuna wengine hawana hata silaha, kwa ufupi tu rais anapokua hapo usalama wataifa wanakuwa wametawanyika katika pande zote 4, ie N,E,W na S. Na kuna wengine kamwe hutawajua ingawa wapo hapo,
 
Wale jamaa niliambiwa wako fit na makini kweli kweli, na wakilenga hawakosi. Kuna siku moja nilikuja kugundua wanatumia sana akili tofauti na watu wanavyowaza au kufikiria kuwa wanatumia nguvu. Rais alikuwa na shughuli ya watu wengi nyumbani kwake, sasa akatoka sehemu aliyokaa akaenda karibu na mlango wa kuingia ndani kuongea na mkewe, akapanda ngazi lakini hakuzimaliza akasimama huku akiongea na mkewe, na walinzi wamemzunguka sasa yule aliyekuwa nyuma yake hakuishia tu kuangalia watu( walikuwa wamepeana mgongo na Mkuu) kwani alikuwa akigeuka kumungalia mzee hasa sehemu ya chini pale aliposimama kwenye ngazi ili ikitokea kama atakosea step au lolote achukue hatua, akageuka kama mara mbili hivi akaamua yeye sasa kusogea kuwa karibu zaidi alipo Rais, akafanya umbali kati ya Rais na yeye kuwa mdogo zaidi kiasi kwamba lolote likitokea hata kama atajisahau au atakosea step hawezi kudondoka kwani atakuwa amezuiwa na mwili wa mlinzi na kumpa nafasi nzuri mlinzi kumuokoa ikiwa ingetokea. Nawakubali sana hawa jamaa
 
Bulkiness of the bodyguards becomes essential in case the circumstance demands them to take the bullet for the president.
 
Mlinzi wa rais lazma awe multipurpose just in case,ebu tafuta hata zile movie kama oympus has fallen,au white house down uone hekaheka za walinzi wa rais zinavyokuwa haraf ujiongeze kama Kwa vitambi vile vya walinzi wetu wanaweza hata robo
Hoja yako haina mashiko kwa kulinganisha Movie na uhalisia. Kwenye movie kuna uwongo mwingi sana kuliko uhalisia. Movie ni kwa ajili ya entertainment tu.
Isitoshe uwezo wa mtu haupimwi kwa mtazamo wa nje tu.
 
Sizani kwamba kuna ulinzi zaidi yahuo unao uona namba moja maana hata hao unawaza kua wakimpamba rais ndo ulinzi mkali sio kweli maana kwetu unaweza sema mlinzi nimmoja ila huwezi pata nafasi yakufanya huu ujinga ulioko marekani kumkamata rais kwenye mazingira mabaya ya kukaangwa chips
 
nnachoweza kukujibu tu ni kuwa I practice martial arts, najua umuhimu wa mimi kuwa na uzito wa kawaida hasa kutokuwa na kitambi and I really hate it, lakini naamini kuwa yeyote aliyepewa jukumu hasa la kiulinzi ni mtu sahihi maana amepatikana kwenye kundi la walio bora, sifanyi tathimini ya ukomavu wao kwa kuangalia vitambi bali ni performance zao,
naamini taasisi za kiulinzi za nchi yetu hazikufanya makosa kuwaweka hao maafisa usalama kuchukua hilo jukumu, OSS
 
Nina knowledge ya baadhi ya sanaa za mapigano. Mtu mwenye kitambi kama wa kwenye hizo picha atakua na faida kama atakua anafanya jiu jitsu lakini ataweza kutamba akikutana na mtu anayefanya krav maga?
Vipi kama akikutana gurkha?

Sijui jeshi letu limespecialize kwenye staili gani ila zamani niliambiwa polisi wanafanya judo wanajeshi kara te.

Hawa waliochaguliwa miongoni mwa walio bora miili yao inawasaliti, labda kama wanavaa bullet proof vest tatu tatu.
 
Nina knowledge ya baadhi ya sanaa za mapigano. Mtu mwenye kitambi kama wa kwenye hizo picha atakua na faida kama atakua anafanya jiu jitsu lakini ataweza kutamba akikutana na mtu anayefanya krav maga?
Vipi kama akikutana na gurkha?

Sijui jeshi letu limespecialize kwenye staili gani ila zamani niliambiwa polisi wanafanya judo wanajeshi kara te.

Hawa waliochaguliwa miongoni mwa walio bora miili yao inawasaliti, labda kama wanavaa bullet proof vest tatu tatu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…