PreGE2025 Waliodukua ukurasa wa Polisi X (Twitter), wadukua ukurasa wa CCM, Airtel, Simba SC, TRA, EWURA na zingine

PreGE2025 Waliodukua ukurasa wa Polisi X (Twitter), wadukua ukurasa wa CCM, Airtel, Simba SC, TRA, EWURA na zingine

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Katika tukio la kushangaza na kusikitisha, kurasa mbalimbali maarufu mtandaoni zimelengwa na wadukuzi wasiojulikana walioteka akaunti rasmi ya Polisi Tanzania kwenye mtandao wa X (zamani Twitter), ukurasa wa Airtel Tanzania kwenye X, akaunti ya YouTube ya klabu ya Simba SC, ukurasa wa X wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Mapato Tanzania (YouTube), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Chama cha Mapinduzi (CCM) pamona na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) zote YouTube.

Katika hujuma hizo, taarifa ya uongo kuhusu kifo cha Rais Samia, imesambazwa na wahalifu hao wa kimtandao.

Jeshi la Polisi wamsaka aliyesambaza taarifa za upotoshaji katika ukurasa wao wa X (Twitter)

Pia, Soma
Yote hii ni kwasababu ya kumuonea Lissu. Wamelikoroga watalinywa! Na bado hadi mbuyu uanguke pwaaa!
 
This could be an inside job. Nashauri waanze na social media managers wa hizo accounts. Wafuatiliwe kama security measures zote wanazifuata. Social meadia account kuwa hacked sababu kubwa ni kutokufuata kanuni za kulinda usalama wa account.
 
Sidhani hata kama unalewa kwa undani API zinavyofanya kazi, kasome (authentication na authorization), API kuwa public haimaanishi unaweza kuingia na kufanya unachotaka...

Kasome CRUD operations kwenye API utaelewa zaidi...

Shida yenu mkipata basics mnasumbua sana.

Unfortunately, sipo tayari kubeba jukumu la kukupa maarifa ya ndani ndani. You got to earn your experience. Period.
 
Shida yenu mkipata basics mnasumbua sana.

Unfortunately, sipo tayari kubeba jukumu la kukupa maarifa ya ndani ndani. You got to earn your experience. Period.
Huelewi chochote mzee, kwa aliyesoma computer science na masuala ya cybersecurity kanielewa...
API kua public basi kila mmoja angeingia kwenye account ya mtu yeyote na kufanya anachokitaka...

Huna maarifa yeyote ya ndani ndani tokana na maelezo uliyotoa yasiyo na mashiko...

Kwamba API zipo public ndio sababu ya kuwa hacked? unachekesha sana...

Ni sawa na kusema kisa bank milango yake ipo wazi basi kila mmoja anaweza kuingia na kuchukua pesa, au ATM machines...
 
Back
Top Bottom