Walioelewa hiki kibonzo cha Masoud Kipanya naomba tafsiri yake

View attachment 3492392
Siku ya leo katika mitandao ya kijamii kuna hii katuni nimekutana nayo, imenitafakarisha sana lakini nimeshindwa kuelewa umaana wake hivyo nimeona haja ya kuileta hapa jukwaani nieleweshwe
Wadhalimu wamedhibitiwa na umma wa wananchi. Usichezee wananchi ambao nguvu yao ni wingi na umoja wao.
Hata uwe na mitutu mingapi, wananchi waliodhamiria watakung'oa tu.
 
Si mlisema masoud hana ithibati ya mambo ya habari, au uchoraji katuni hauna ithibati za JAB?
 
So kigogo ni wananchi? Na mbona upande mwingine kuna tofali limeegama kutaka kuanguka linaashiria nini
 
Si mlisema masoud hana ithibati ya mambo ya habari, au uchoraji katuni hauna ithibati za JAB?
Ni vile tafsiri zake anazifumbafumba, angekuwa direct angeshapigwa stop zamani sana😁. By the way skuizi naona anaendeleza mapambano kama afisa usafirishaji wa mtandaoni #request
 
ChatGPT
 
Attachments

  • IMG_2682.jpeg
    IMG_2682.jpeg
    251.9 KB · Views: 20
Imaweza kuwa maandamano yamegota
Ingawa wengi hawatapenda tafsiri hii

Labda vingine sijui
Tunatabiri tu jamani
Yatakuwa "yamegota" vipi wakati kizingiti kimeshalazwa chini, na tayari wa nyuma yake wapo tayari kuvuka?

Nadhani umeipa tafsir ya upande unaoutaka wewe. Ila ni vizuri umesema hujui. (angalao).
 
wabongo ni kama nyumbu 100 wanafukuzwa na simba 2, ila ukweli nyumbu wakiamua kupigana, 100% watashinda na kuua simba wote, ni swala la muda tuu wananchi watajua wana nguvu kuliko bi ushungi na genge lake
 
Nimeona sehemu ndugu zetu wakenya wanasema maandamano ni very addictive kiasi kwamba yakishaanza siyo rahisi kuisha
 
Yatakuwa "yamegota" vipi wakati kizingiti kimeshalazwa chini, na tayari wa nyuma yake wapo tayari kuvuka?

Nadhani umeipa tafsir ya upande unaoutaka wewe. Ila ni vizuri umesema hujui. (angalao).
Niliandika nikafuta
 
Back
Top Bottom