Walioitwa 'stupid' na Rais bado wapo ofisini wanakula kiyoyozi!

Lile neno stupid kwenye nchi zilizostaarabika lilipaswa kuambatana na barua yakuomba kukaa pembeni Kwa watu wafuatao;

1. Waziri mwenye dhamana na sekta ya usafiri kwa Tanzania Makame Mbarawa.

2. Afisa Masuuri (Katibu Mkuu wa wizara husika).

3. Waziri wa Fedha ambaye ndiye mlipaji.

4. Maafisa wote waliohusika na mchakato wa ukokotoaji na upokeaji wa hiyo invoice hadi kuiandika ilipwe.

Lakini kutokana na kukuosekana kwa collective accountability hakuna hata mmoja aliyetaka kusikia kauli ya kuchukuzwa kwa Rais. Tafsiri ya kukaa pembeni siyo kwamba umefanya bali yalipokuwa yanafanyika ulikuwepo na ulipaswa kuyaona ila hukuona au ulichelewa kutoa opinion yenye maslahi kwa umma.

Ila kwa Tanzania hata Rais angewataja kwa majina hakuna ambaye angeondoka ofisini hadi Rais atengue Kwa mkono wake!

Hiki kiburi cha watumishi na wanasiasa Tanzania, hakuna uwajibikaji, lakini pia Mawaziri wengi na Makatibu Wakuu wanaishi kwa salary, hivyo kwa kuwa hakuna alternative source ya income ni vigumu wao kukubali kurudi kujitegemea maana watoto watafukizwa ada.

Madhara ya kiburi hiki ni kwamba, Rais anaonekana anasema lakini hakuna kuchukua hatua kwa wale wanaomchukiza.
Yawezekana aliyewambia stupid ndiyo alitakiwa ajiuzulu
 
Anaonyesha udhaifu mkubwa sana. Kwa alichokiongea pale ukumbini, ilipaswa barua ya utenguzi ifuate au kutamka moja kwa moja kuwa fulani, fulani nisikuone ofisini kesho......
Hakuna rais pale, eti anawaambia wajitafakari. Kujitafakari nini?! Mbona mwizi wa simu hawaambiwi wajitafakari
 
Kwa ai aina hii ya uongozi wa mama, hakika Magu ataendelea kukumbukwa kwa maamuzi yake ya papo kwa hapo.
Magu naye alikuwa na majizi yake aliyoyapa ushirikiano. Kuna walioficha hela za plea bargaining, kuna waliopora mchana kina Sabaya na Makonda. Kuna Kakoko na yeye mwenyewe Magufuli.
 
Ma.ma: You are our President, our guide and our leader. Tunakuamini na tunakukubali. Piga Kazi na usipuuze ushauri ushauri ila usiendekeze kila lisemwalo. They want to see you derail ili wafurahi....HASBIYA WALLAHI WANI' LMAL WAKIL...They will not succeed biidhnillah...RAMADHAN KARIM
 
Lile neno stupid kwenye nchi zilizostaarabika lilipaswa kuambatana na barua yakuomba kukaa pembeni Kwa watu wafuatao;

1. Waziri mwenye dhamana na sekta ya usafiri kwa Tanzania Makame Mbarawa.

2. Afisa Masuuri (Katibu Mkuu wa wizara husika).

3. Waziri wa Fedha ambaye ndiye mlipaji.

4. Maafisa wote waliohusika na mchakato wa ukokotoaji na upokeaji wa hiyo invoice hadi kuiandika ilipwe.

Lakini kutokana na kukuosekana kwa collective accountability hakuna hata mmoja aliyetaka kusikia kauli ya kuchukuzwa kwa Rais. Tafsiri ya kukaa pembeni siyo kwamba umefanya bali yalipokuwa yanafanyika ulikuwepo na ulipaswa kuyaona ila hukuona au ulichelewa kutoa opinion yenye maslahi kwa umma.

Ila kwa Tanzania hata Rais angewataja kwa majina hakuna ambaye angeondoka ofisini hadi Rais atengue Kwa mkono wake!

Hiki kiburi cha watumishi na wanasiasa Tanzania, hakuna uwajibikaji, lakini pia Mawaziri wengi na Makatibu Wakuu wanaishi kwa salary, hivyo kwa kuwa hakuna alternative source ya income ni vigumu wao kukubali kurudi kujitegemea maana watoto watafukizwa ada.

Madhara ya kiburi hiki ni kwamba, Rais anaonekana anasema lakini hakuna kuchukua hatua kwa wale wanaomchukiza.
Mimi kinachonishangaza ni ukimya wa vyo habari ..haya mambo ya auditing report y CAG hata hayawahusu
 
Mtu ashakunja mijihela hata ukimuita stupid,wala hajali

Ova
 
Ma-stupid wapo wengi sana maofisini.

Kuanzia sasa mtu akifanya ubadhirifu wa mali za umma tumuite stupid.
 
Mtu ameshaweka bilioni zake matakoni hata umwite stupid mwaka mzima haiwezi kumsumbua na hata ukimtumbua ataenda kufanya mambo yake maana tayari mtaji anao.
 
Aliyewaita kuwa stupids kaishia hapo, wakati ana mamlaka ya mwisho kabisa kuwawajibisha. Kwanini wao wahangaike?

Huko walipo wanajifariji kinafiki kwamba sio Mimi ni Fulani, hivyo hawawezi hata kujisuta nafsini mwao, watawezaje kujiuzulu?
Naomba Nikuambie kuwa Ile Kauli ya Rais Kuwa "Watupishe" ni AMRI na hao wahusika kama bado hawajatupisha inamaanisha kuwa hawajaitii AMRI Ya Rais. Hivyo basi Vyombo husika vya kuwachomoa huko ofisini vinapaswa kufanya kazi yake labda kama pia vinadharau Hiyo AMRI Ya Rais.

Kile kipindi Cha EPA Rais Kikwete alitamka "Watupishe" na mara hiyo hiyo kina Tubaijuka "walitupisha".
 
Hao viongozi ni washenzi tu mwisho wao ni aibu kubwa. Hongera Rais kwa kuwakemea bila ya kuwaonea aibu.
 
Tatizo la nchi hii Sio Samia Tatizo la nchi hii ni CCM. Bila ya CCM kuondoshwa madarakani Nothing will change.
 
Kuna mwingine kanunua LC 300 Landcruiser kamnununuloa demu wake yule wa simba baada ya kujifungua almost mil 400, huyo waziri wanasema kipara na ndiye mhujumu mkubwa wa mama kwenye mwanga wa usiku ule wa binaadamu yaani hata kuzima zima pale taifa siku ya mecho alihusika
Fungua codes vizuri tufaidike
 
"stupid" ni tayar onyo wamepew sasa unatak wapew adhabu mara Ngap mkuu

Na hili mkalitazame[emoji1783]
 
Lile neno stupid kwenye nchi zilizostaarabika lilipaswa kuambatana na barua yakuomba kukaa pembeni Kwa watu wafuatao;

1. Waziri mwenye dhamana na sekta ya usafiri kwa Tanzania Makame Mbarawa.

2. Afisa Masuuri (Katibu Mkuu wa wizara husika).

3. Waziri wa Fedha ambaye ndiye mlipaji.

4. Maafisa wote waliohusika na mchakato wa ukokotoaji na upokeaji wa hiyo invoice hadi kuiandika ilipwe.

Lakini kutokana na kukuosekana kwa collective accountability hakuna hata mmoja aliyetaka kusikia kauli ya kuchukuzwa kwa Rais. Tafsiri ya kukaa pembeni siyo kwamba umefanya bali yalipokuwa yanafanyika ulikuwepo na ulipaswa kuyaona ila hukuona au ulichelewa kutoa opinion yenye maslahi kwa umma.

Ila kwa Tanzania hata Rais angewataja kwa majina hakuna ambaye angeondoka ofisini hadi Rais atengue Kwa mkono wake!

Hiki kiburi cha watumishi na wanasiasa Tanzania, hakuna uwajibikaji, lakini pia Mawaziri wengi na Makatibu Wakuu wanaishi kwa salary, hivyo kwa kuwa hakuna alternative source ya income ni vigumu wao kukubali kurudi kujitegemea maana watoto watafukizwa ada.

Madhara ya kiburi hiki ni kwamba, Rais anaonekana anasema lakini hakuna kuchukua hatua kwa wale wanaomchukiza.
Inawezekana mh raisi aliongea tu hilo neno kwa hasira lakini hakujua anamtukana nani,
Na baada ya kuwajua yeye tena anaweza kuwaomba msamaha wakati sisi tunasubili matokeo😁😁😁😁
 
Naomba Nikuambie kuwa Ile Kauli ya Rais Kuwa "Watupishe" ni AMRI na hao wahusika kama bado hawajatupisha inamaanisha kuwa hawajaitii AMRI Ya Rais. Hivyo basi Vyombo husika vya kuwachomoa huko ofisini vinapaswa kufanya kazi yake labda kama pia vinadharau Hiyo AMRI Ya Rais.

Kile kipindi Cha EPA Rais Kikwete alitamka "Watupishe" na mara hiyo hiyo kina Tubaijuka "walitupisha".
Na iwe hivyo ndugu...Ndicho tunachotaka.

Shida " Watupishe" yake inaonekana inakosa mamlaka fulani hivi, ndio maana watu wanahoji kama imeishia pale ama laa. Chanzo ni Kauli za Mama juu ya Wezi kumuogopa Mungu.

Kimsingi mpaka leo ilipaswa tuwe tumewajua tayari, lakini ajabu hawajulikani bado.
 
Aliyewaita kuwa stupids kaishia hapo, wakati ana mamlaka ya mwisho kabisa kuwawajibisha. Kwanini wao wahangaike?

Huko walipo wanajifariji kinafiki kwamba sio Mimi ni Fulani, hivyo hawawezi hata kujisuta nafsini mwao, watawezaje kujiuzulu?
Mama hajaishia hapo lazima wawajibishwe wait and see
 
Au mama nae huwa anapewa 10% nini? kwanini anawaambia mtupishe badala ya kuwafungulia kesi, kuwafilisi na kuwafunga?
 
Back
Top Bottom