Walioitwa 'stupid' na Rais bado wapo ofisini wanakula kiyoyozi!

Walioitwa 'stupid' na Rais bado wapo ofisini wanakula kiyoyozi!

Watu wanapiga pesa ndefu vile unabaki kulalama kwenye tv eti stupid. Amri jeshi mkuu unalia, halafu kesho mnaenda kukopa na kuongeza tozo wa Raia. Very stupid in deed.
Naona tumeanza kulia tena. Wakati wa Kikwete tulilia hivi hivi, tukawa tunatamani tupate rais mkali mwenye mkono wa chuma, tukapata mwamba Magu (rip), sisi hawa hawa tukaanza kulalamika vyuma vimekaza.
Amekuja Samia, mpole, hana maneno mengi, ana lugha nzuri ya ushawishi; wahuni wametupiga, sasa mnaanza kusema Amiri jeshi mkuu achukue hatua!
Tutageukageuka mpaka lini?
 
Watu wenye akili hao!

Somewhere duniani yupo mwanamama aliyechafua mitaa kwa mabango kila mahali akijitangaza ni mwanamke shupavu anayeweza kila kitu but watu wamepiga kumeonekana hadi mikono ya wateuzi wake ila still hajui afanye nini.

Ameishia kuhodhi kazi za viongozi wa dini kuwakumbusha hao wezi kwamba hela wanazoiba wasifikiri watazikwa nazo,unamtisha mwizi wa kiAfrica kaburi... ulisikia wapi?
Yeye kashindwa kujiuzulu ?

View attachment 2572730
 
  • Thanks
Reactions: TPP
Wabongo kujiuzulu hawakubali, hadi afukuzwe au akamatwe afungwe au anyongwe ndio wataachia nafasi zao, sbb hao watu ni wezi sugu, sasa mwizi sugu ajiuzulu? Yaani waachie nafasi yao kirahisi, ni ngumu mno, dawa ni kuwafukuza na kuwafungulia mashtaka ya uhujumu uchumi.
 
Back
Top Bottom