Ni vitu gani hivyo kwa faida ya wengi
edward93
1.KIWANJA
Hakikisha unachagua kiwanja kizuri in terms of landscape na accessibility! Chaguzi sahihi ya kiwanja upunguza gharama za ujenzi so kuwa makini mwanzo kabsa wakt unanunua kiwanja.
2.RAMANI
Watu wengi upenda kuchukua ramani(copy n paste) na kuanza ujenzi bila ya kufanya uchunguzi wa ramani husika kutokana na uwezo wake au mahitaji yake! Hakikisha kama sio mtaalamu mtafute hata mtaalamu mkae muitafsiri ramani na kujadiliana juu ya ramani zima iendane na mahali unapojenga!
3.KONA
Make sure unapunguza nyumba yako kuwa na kona nyingi zisizo na ulazima kwan kona nyingi uongeza kuta, idadi ya bati na mbao za kenchi, na kufanya gharama za nyumba kupanda.
4.MABADILIKO NJIANI
Hakikisha kbla ya kuanza ujenzi ushajua nyumba yako itakuaje na ukubaliane nayo! Epuka kufanya changes midway(kubadilisha wakati ushaanza)
5. FUNDI
Hakikisha unapata fundi mzuri wa kufanya kazi yako na unapochagua fund factor yako isiwe bei tu, usimpe fundi kaz eti kisa ana bei ndogo go extra mile (kwenye engineering tunaamin kuna mahusiano makubwa kati ya cost n safety hvo vitu ni direct proportional)
Pia jitahidi fundi wako atoke maeneo ya unapofanyia ujenzi kuliko kumtoa mbali
6. KUKODI BADALA YA KUNUNUA
Makes sure baadhi ya vitu ambavyo unaweza kuvpata kwa kukodi unafnya hvyo instead ya kuvinunua mfano Mbao za formwork, mapipa ya maji, formwork za nguzo, sahani kwa ajili ya madirisha, mirunda etc
7.UWEPO SITE MUDA MWINGI
Hata kama ujui abc za ujenzi hakikisha wakat wa ujenzi unatenga muda mwingi wa ww mwnyewe kuwepo site na kuobserve kila kitu kama unaweza kupata hyo nafasi.
8.KUTOJENGA KWA AWAMU NYINGI
Ni kwel ujenzi gharama sana lakni hakikisha ukianza ujenzi usijenge kwa awamu nying sana kama una kipato kidgo bas nunua hata material kwanza then ukianza at least ujenge kwa awamu nne (msingi,boma,kupaua,finishing) kujenga kwa muda mrefu au ile ukipata laki unaita fundi ni gharama zaidi.
9.BAJETI
Hakikisha kabla ujaanza unajua bajeti aghalau ya makadirio ya nyumba yako mpka kukamilika na kama una uwezo huo! So ili ujenzi usikusumbue zaidi hakikisha unajenga nyumba ya kipato chako.
10.LAYOUT
Hapa namaanisha mpangilio wa vyumba, hakikisha unaweka vyumba vinavyofanana sehemu moja, nakupa mfano vyoo (master na public),jiko,dining kwa sababu lazima viwe connected na mfumo wa maji taka ni vzr uviweke kwenye sehemu moja au karbu hi itakupunguzia cost wakat wa plumbing kuliko kuviweka mbali mbali.
Kwa maneno rahis vyumba vyenye tabia za kufanana vikae karibu.
11.MATERIAL
Uchaguzi sahihi wa material za kujengea! Mfano ni vizur kujengea ile kokoto nyeusi ambayo haina vumbi( utumia saruji kidgo zaidi kutengeneza zege zuri kuliko ile kokoto nyekundu), mchanga(ukitaka kujua mchanga mzuri uchukue mkononi then ingiza mkono wako ndani ya ndoo kama mchanga ujaondoka wote kiganjani kwako au aujakuwa tope basi ni mzuri) Maji ya chumvi sio mazuri kujengea etc
So hizo ni baadhi ya tips na wengne naamini watashare tupate kujifunza zaidi