Waliojipatia Milioni 280 kwa njia ya Mtandao watozwa Faini ya Laki Tano

Yaani matapeli wanawaibia watu milioni 280, wanatozwa faini ya laki 5! Halafu yule masikini aliyekamatwa na nyama ya porini, alihukumiwa miaka 20 na yule Hakimu wa Mafinga!!

Hii nchi kwa hapa tulipofikia, tunahitaji Katiba Mpya.
Katiba hauwezi ipata mana wanaohusika na kuiandaa hawataki ,Jambo la msingi ni kuingia barabarani tu
 
Kama ni hivi wacha nijiajiri kwenye sector ya uwizi tu.
 
Kituko kingine Tz na waliposema ni nchi ya pili kwa kuwa na vivutio vya utalii ndio hivi
 
This is very fair!. Watanzania tunahitaji kuelimishwa kuhusu katiba, sheria na haki, ikiwemo plea bargain. Ukiiba hata mabilioni kama yale ya EPA, ukakubali ni kweli umeiba, mkakubaliana na DPP utarudisha ulichoiba, then unapunguziwa adhabu!. Mfano mzuri ni yale majizi ya EPA, Kagoda Haina Kesi, hawafikishwi Mahakamani Ng'o!
P
 
Wazee wa Tuma hela kwenye namba hii wanajiamini sana kwa kuwa wanajua wanetengeneza Chain nzuri kuanzia Polisi hadi Mahamani na TCRA wakiwa busy na VPN wakiacha kabisa mambo ya kitapeli...
 
Ndiyo maana ya "plea bargain" hiyo. Ni sheria yetu wenyewe, haina tatizo.
 
Kuna mtu alichoma moto nyumba ya mwenzie alipofika mahakamani faini haikufika hata laki 2
 
Nyuma ya pazia zimewatoka za kutosha sana japo wana mtaji wa kuanzia maisha bado

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dpp na hakimu wanagaiwa ngapi ngapi?

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Mauzauza hoyee!
Huoni kila mwaka Serikali inasomewa wizi wake na bado hakuna anayeeajibishwa, na mwaka unsoguata wa fedha, wanapelekewa tena pesa, nao wanazitafuna tena! Mfumo mzima ni wizi na rushwa kuanzia ofisi namba moja mpaka kwenye tarafa!

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…