Waliomfitini Dr Mwele kwa Magufuli, wanajisikiaje?

Waliomfitini Dr Mwele kwa Magufuli, wanajisikiaje?

Kuhamia Dodoma yalikuwa maamuzi ya hovyo with the loose of multibillion USD , Dr mwele ni moja ya watu wa hovyo zaidi ndo mana alifukuzwa na hakuna haja ya kuandika upuuzi wake humu , alale Kwa Amani huko Aliko , kuna mambo Maghufuli aliyafanya kiume hakuna Raisi wa kumfikia labda azaliwe mwingine hayo nitamtetea whatever the case , na kuna mambo alichochora vibaya mno hayo pia nitamponda
Una wivu wa kike.
Kasome na wewe upate PhD ya wizi na umtafiti mwendazake.
 
Dr Mwele alikuwa kipenzi cha watu.
Hakuwahi kufanya siasa kwa muda mrefu, lakini uthubutu wake, hasa akiwa mwanamke msomi na mwanasayansi uliwagusa wengi.

Kuna ambao hawakumpenda kwa sababu hizo.
Lakini huu msiba wake umeonyesha alivo moyoni mwa watu.

Magufuli alimfukuza kazi Dr Mwele, saa sita za usiku.
Magufuli lazima alipelekewa umbeya wa kufitinisha, naye kwa vile kulikuwa na kitu rohoni mwake akasema hapahapa, wala hakukuchi!

Lakini dunia ni mviringo, sijui wafitini, na wanajulikana, wanajisikiaje sasa.
Roho Mbaya ya Mwendakuzimu tu ndio lisababisha Dr Mwele afukuzwe kazi
 
Unalosema ni sawa. Utafiti wao ulihusisha watoto 80 wenye mwonekano kama hao unaosema wa Brazil. 35% wakawa positive. Shida ilikuja pale aliposema Zika ni endemic Tanzania.

Huwezi tumia sample sample size ndogo hivyo tena purposefully selected (wenye features zinazoendana na zika) then ukaja na conclusion ya general population, kwamba Zika ni endemic in Tanzania.

Bora useme wewe
 
Dr Mwele alikuwa kipenzi cha watu.
Hakuwahi kufanya siasa kwa muda mrefu, lakini uthubutu wake, hasa akiwa mwanamke msomi na mwanasayansi uliwagusa wengi.

Kuna ambao hawakumpenda kwa sababu hizo.
Lakini huu msiba wake umeonyesha alivo moyoni mwa watu.

Magufuli alimfukuza kazi Dr Mwele, saa sita za usiku.
Magufuli lazima alipelekewa umbeya wa kufitinisha, naye kwa vile kulikuwa na kitu rohoni mwake akasema hapahapa, wala hakukuchi!

Lakini dunia ni mviringo, sijui wafitini, na wanajulikana, wanajisikiaje sasa.
Mwele alidanganya kwamba Kuna zika wakati haipo. Thanks jpm
 
Ukipata mgonjwa ana vimelea na madhira ya ugonjwa ambao kinga yake ni ya maisha ni janga?

Brazil wasingefikia mwafaka kuwa ile ni Zika, leo wakafikia mwafaka kuwa ni Zika, kwa sasa wanatangaza janga??

Mtu akipima polio ikawa/akakutwa na majibu chanya tayari ni janga??

Mbona una zunguka zunguka? Kwani lengo la ule utafiti ilikuwa nini? Na lengo la kutangaza matokeo ya utafiti ilikuwa nini? Mbona Press yake ilikuwa clear anaitangazia dunia kugundulika virus wa zika Tanzania?
Kwenye hili uwezi kumtetea Mwele kamwe alikosea na alikuwa punished kutokana na makosa yake tena ya kizembe na kujitakia
 
Unalosema ni sawa. Utafiti wao ulihusisha watoto 80 wenye mwonekano kama hao unaosema wa Brazil. 35% wakawa positive. Shida ilikuja pale aliposema Zika ni endemic Tanzania.

Huwezi tumia sample sample size ndogo hivyo tena purposefully selected (wenye features zinazoendana na zika) then ukaja na conclusion ya general population, kwamba Zika ni endemic in Tanzania.

Sikumbuki juu ya kusema Zika ni endemic(I stand to be corrected), ila nakumbuka kusema hii inafungua mlango kwa tafiti nyingine kufanyika.

Na waliokuja kukanusha wakasema, ni vifaa vilivyokuwa vyinafanyiwa utafiti ili kujua kana vinaweza kupima. Bado ni eneo linahitaji utafiti pia.
 
Dr Mwele alikuwa kipenzi cha watu.
Hakuwahi kufanya siasa kwa muda mrefu, lakini uthubutu wake, hasa akiwa mwanamke msomi na mwanasayansi uliwagusa wengi.

Kuna ambao hawakumpenda kwa sababu hizo.
Lakini huu msiba wake umeonyesha alivo moyoni mwa watu.

Magufuli alimfukuza kazi Dr Mwele, saa sita za usiku.
Magufuli lazima alipelekewa umbeya wa kufitinisha, naye kwa vile kulikuwa na kitu rohoni mwake akasema hapahapa, wala hakukuchi!

Lakini dunia ni mviringo, sijui wafitini, na wanajulikana, wanajisikiaje sasa.
Mtoa mada ile zika aliyozusha uliiona tena? Maana kisa cha yeye kuondolewa kutangaza kuwa kuna ugonjwa wa zika wakati yeye hakuwa na mamlaka ya kutangaza ugonjwa.
 
Pale Dr. Mwele hakutangaza outbreak ya Zika. Alikuwa anaelezea matokeo ya tafiti zilizofanyika. Moja ikihusisha watoto wenye mwonekano kama wale wa wazazi waliopata Zika kule Brazil.

Na matokeo yalikuwa chanya, yakiwa yamefanywa kwa PCR machine. Hii ilionyesha kuwa nasi hatujajitenga na haya matatizo kwani karibu nasi kuna nchi ambazo zilikwishapata Zika (mipaka yetu haina makomeo ya ugonjwa).

Uongozi wa juu ukapaniki, kwani haya ni mambo ya science, Zika ni lifelong/matatizo na uwepo wake unaweza kutambuliwa hata ndani ya miaka yote ya maisha yako. Hivyo, mtu akipata unaweza kupata ushahidi wakati wowote.

Hakumaanisha tulikuwa na outbreak, katafute kwenye kile kikao kama kuna neno outbreak au tuna janga la Zika.
Ila kupaniki kwa uongozi kulisukumwa na kilichokuwa kinaendelea Brazil na nchi za karibu na huko.
Kuna taratibu za kutangaza matokeo ya tafiti hasa zinazohusiana na maisha ya watu.
 
Hebu acha uongo Dr Mwele hakufitiniwa na mtu yeyote yule alijifitini yeye mwenyewe! Jiulize ile Zika ilikwenda wapi? Dr Mwele hakufata utaratibu wowote wa kufanya aliyoyafanya maana hata waziri wake hakuwa na taarifa! Uwezi tangaza janga kwenye nchi halafu bila kuzishirikisha mamlaka! Dr Mwele aliwajibika kwa makosa yake mwenyewe tuache kusingizia watu na kuwabebesha watu lawama wasizostahili!
Hapana. Dr. Mwele alikuwa anatoa matokeo ya utafiti walioufanya NIMR ndipo katika waliyogundua ilikuwa ni pamoja na huo ugonjwa. Hakuwa anatangaza kama unavyodai. Nadhani taarifa za tafiti zao huwa zinapelekwa Wizarani. Kama Waziri hakuwa na taarifa hilo HALIKUWA kosa la Dr. Mwele
 
Umeeleza vizuri sana. Kuna watu wajinga wasioheshimu sayansi kwahiyo ukifanya utafiti kwa mambo wasioyaoyapenda hawataki kusikia matokeo yake. Iwapo angefanya utafiti kuwa watu wangapi na wa marika gani wanampenda Magufuli na akatoa matokeo yake angepandishwa na cheo
Yeah, umenena, na sio atoe matokeo halisi ya utafiti bali achakachue aseme 99% wanampenda magufuli. BTW,
hivi ni maabara gani ilipima mapapai, oil chafu na nyama ya mbuzi vikakutwa na corona?
 
Mtoa mada ile zika aliyozusha uliiona tena? Maana kisa cha yeye kuondolewa kutangaza kuwa kuna ugonjwa wa zika wakati yeye hakuwa na mamlaka ya kutangaza ugonjwa.
Waliorithi kazi NIMR kwani wana ubavu wa kongea juu ya tafiti zao?
Imeingio Covid-Omricon hapa watu kimyaa!
 
Back
Top Bottom