Lanlady
JF-Expert Member
- Feb 27, 2019
- 1,836
- 6,303
Kwa mtazamo wangu, naona kabisa Mama Samia hakupaswa kuwa kiongozi mkubwa wa kitaifa. Kauli zake, mwenendo na maono yake vinadhihirisha wazi.
Ni kiongozi ambaye kwa kauli zake na maamuzi yake anaonesha wazi hakuwa na maono yoyote ya kuongoza taifa.
Teuzi za kulazimishana hufanyika sana hasa ndani ya vyama. Ifike mahali viongozi wa kiserikali wapewe fursa ya kuomba kuteuliwa na waeleze maono yao endapo watapewa nyadhifa hizo. Kuanzia ngazi urais, makamu, waziri mkuu na mawaziri wote.
Kabla mtu ajateuliwa, maombi yatumwe, na iundwe tume huru ya kuwafanyia usaili. Kuna watu wanaweza kupata teuzi ilihali hawana kabisa maono juu ya majukumu waliyopewa.
Matokeo yake wanakuwa kama bendera kufuata upepo!
NB: Haya ni maoni yangu tu kama Mtanzania. Sina chuki, wivu wala hasira na kiongozi yeyote. Tunachohitaji ni uzalendo wa kweli toka kwa viongozi wetu!