Waliomlazimisha Samia Suluhu kuwa Makamu na hatimaye Rais, walifanya makosa sana

Waliomlazimisha Samia Suluhu kuwa Makamu na hatimaye Rais, walifanya makosa sana

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,836
Reaction score
6,303
Kwa mtazamo wangu, naona kabisa Mama Samia hakupaswa kuwa kiongozi mkubwa wa kitaifa. Kauli zake, mwenendo na maono yake vinadhihirisha wazi.

Ni kiongozi ambaye kwa kauli zake na maamuzi yake anaonesha wazi hakuwa na maono yoyote ya kuongoza taifa.

Teuzi za kulazimishana hufanyika sana hasa ndani ya vyama. Ifike mahali viongozi wa kiserikali wapewe fursa ya kuomba kuteuliwa na waeleze maono yao endapo watapewa nyadhifa hizo. Kuanzia ngazi urais, makamu, waziri mkuu na mawaziri wote.

Kabla mtu ajateuliwa, maombi yatumwe, na iundwe tume huru ya kuwafanyia usaili. Kuna watu wanaweza kupata teuzi ilihali hawana kabisa maono juu ya majukumu waliyopewa.

Matokeo yake wanakuwa kama bendera kufuata upepo!

NB: Haya ni maoni yangu tu kama Mtanzania. Sina chuki, wivu wala hasira na kiongozi yeyote. Tunachohitaji ni uzalendo wa kweli toka kwa viongozi wetu!
 
Mtoa mada yote uliyoyasema ni mambo ya katiba mpya, katiba mpya ndio itakayotuletea taasisi imara na huru, President Samia she is doing a good job, tumpe muda na support, kwangu so far so good, awamu iliyopita ilikua ya mauaji, no respect kwa human rights, yes Mwenyezi Mungu ilibidi aingilie kati otherwise tulishaanza kuwa Zimbabwe in the making, welldone my President Samia
 
Acha kufuru., Kwani nani alitegemea JPM atafariki, Mbona Samia alipokuwa Makamo wa Rais hukusema haya maneno kwamba hakupaswa kuwa, Siku aliyochaguliwa kuwa Makamo watanganyika wote walipigwa makofi na kwakwa kwamba tumepata mahali pa kuwadanganya danganya wazanzibari kwamba mtu wao amepewa umakamo hivyo angalau watanyamaza, au kwa sababu sasa ni Rais unataka atokee mtu awe na mtazamo wa kuona baadae wakati hakuna zaidi ya mwenyewe Mungu

Tunasema ni majaliwa ya Mungu mama kuwa Rais., wewe unafkiri kuna mtanganyika angekubali Rais wa JMT atokee Zanzibar??? lakini unaonaje sasa uwezo wa Mungu? Je kuna mtu anaweza kuzuia?

Shida kubwa ni chuki dhidi ya Rais Mama samia kwamba ni mwanamke lakini ametoka Zanzibar anaiongoza vizuri NCHI., mumepigwa na mshangao kuona mwanamke muda mfupi anajaribu kunyoosha nchi iliyokuwa imevurugwa vurugwa na mwendazake., emu tafuta ile clip ya Benard Membe aliyosema hivi karibuni kuhusu Mama.
 
Kwa mtazamo wangu, naona kabisa mama SSH, hakupaswa kuwa kiongozi mkubwa wa kitaifa. Kauli zake, mwenendo na maono yake vinadhihirisha wazi.

Ni kiongozi ambaye kwa kauli zake na maamuzi yake anaonesha wazi hakuwa na maono yoyote ya kuongoza taifa.

Teuzi za kulazimishana hufanyika sana hasa ndani ya vyama. Ifike mahali viongozi wa kiserikali wapewe fursa ya kuomba kuteuliwa na waeleze maono yao endapo watapewa nyadhifa hizo. Kuanzia ngazi urais, makamu, waziri mkuu na mawaziri wote.

Kabla mtu ajateuliwa, maombi yatumwe, na iundwe tume huru ya kuwafanyia usaili. Kuna watu wanaweza kupata teuzi ilihali hawana kabisa maono juu ya majukumu waliyopewa.

Matokeo yake wanakuwa kama bendera kufuata upepo!

NB: Haya ni maoni yangu tu kama mtanzania. Sina chuki, wivu wala hasira na kiongozi yeyote. Tunachohitaji ni uzalendo wa kweli toka kwa viongozi wetu!
Hilo liko wazi
 
Acha kufuru., Kwani nani alitegemea JPM atafariki, Mbona Samia alipokuwa Makamo wa Rais hukusema haya maneno kwamba hakupaswa kuwa, Siku aliyochaguliwa kuwa Makamo watanganyika wote walipigwa makofi na kwakwa kwamba tumepata mahali pa kuwadanganya danganya wazanzibari kwamba mtu wao amepewa umakamo hivyo angalau watanyamaza, au kwa sababu sasa ni Rais unataka atokee mtu awe na mtazamo wa kuona baadae wakati hakuna zaidi ya mwenyewe Mungu

Tunasema ni majaliwa ya Mungu mama kuwa Rais., wewe unafkiri kuna mtanganyika angekubali Rais wa JMT atokee Zanzibar??? lakini unaonaje sasa uwezo wa Mungu? Je kuna mtu anaweza kuzuia?

Shida kubwa ni chuki dhidi ya Rais Mama samia kwamba ni mwanamke lakini ametoka Zanzibar anaiongoza vizuri NCHI., mumepigwa na mshangao kuona mwanamke muda mfupi anajaribu kunyoosha nchi iliyokuwa imevurugwa vurugwa na mwendazake., emu tafuta ile clip ya Benard Membe aliyosema hivi karibuni kuhusu Mama.
Inawezekana umekurupuka au una mihemko.
Hapa suala sio mtu kuwa kiongozi, isipokuwa ni utayari wa kuwa kiongozi.
Ukisikiliza hotuba nyingi za mama utagundua kwamba hakuwa na utayari kwa nafasi alizoteuliwa.
Huenda hatambui kwamba kauli zake kisiasa zinamfunga, au anaogopa lawama za moja kwa moja.

Kuna watoto wako shule za awali, msingi, sekondari nk, ukiwauliza ndoto zao watakwambia wanataka kuwa viongozi wakubwa wa kiserikali. Hayo ni maono yao. Na hao wakipewa fursa wanaweza kuwa viongozi bora tofauti na wale wanaoteuliwa kwa lazima au kwa kujuana. Hiyo ndio hasa hoja yangu.

Wakati niko chuo fulani, kuna dada alilazimishwa kuwa katibu wa bunge pasipo matakwa yake. Alisema wazi yeye hajui chochote khs majukum hayo ya ukatibu na hakuitaka hiyo nafasi. Lakini kwasababu viongozi wa tume hawamkutaka aliyekuwa anagombea nafasi hiyo, wakamlazimisha agombee kwa maslahi yao. Katika nchi yetu huu ni mfumo.

Na ukumbuke kwamba uongozi wa serikali yetu sio wa kifalme, kusema kwamba unafuata ukoo!
Ni muhimu kuzingatia utayari wa anayeteuliwa. Kuna watanzania wengi sana wenye maono juu ya taifa lao.
 
Back
Top Bottom