Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Usiangalie kauli angalia matendo yake na utimizaji wa ahadi zake. Maneno yanaweza kuwa mepesi kwako, lakini tambua ni sehemu ya malezi yake, hakufundishwa kufokea wala kukebehi watu.Inawezekana umekurupuka au una mihemko.
Hapa suala sio mtu kuwa kiongozi, isipokuwa ni utayari wa kuwa kiongozi.
Ukisikiliza hotuba nyingi za mama utagundua kwamba hakuwa na utayari kwa nafasi alizoteuliwa.
Huenda hatambui kwamba kauli zake kisiasa zinamfunga, au anaogopa lawama za moja kwa moja.
Kuna watoto wako shule za awali, msingi, sekondari nk, ukiwauliza ndoto zao watakwambia wanataka kuwa viongozi wakubwa wa kiserikali. Hayo ni maono yao. Na hao wakipewa fursa wanaweza kuwa viongozi bora tofauti na wale wanaoteuliwa kwa lazima au kwa kujuana. Hiyo ndio hasa hoja yangu.
Wakati niko chuo fulani, kuna dada alilazimishwa kuwa katibu wa bunge pasipo matakwa yake. Alisema wazi yeye hajui chochote khs majukum hayo ya ukatibu na hakuitaka hiyo nafasi. Lakini kwasababu viongozi wa tume hawamkutaka aliyekuwa anagombea nafasi hiyo, wakamlazimisha agombee kwa maslahi yao. Katika nchi yetu huu ni mfumo.
Na ukumbuke kwamba uongozi wa serikali yetu sio wa kifalme, kusema kwamba unafuata ukoo!
Ni muhimu kuzingatia utayari wa anayeteuliwa. Kuna watanzania wengi sana wenye maono juu ya taifa lao.
Tazama matendo yake, tazama lugha yake ilivyo na uwezo wake wa kukubalika kimataifa ulivyo. Tazama convincing power aliyonayo katika taasisi nyeti za kidunia. Tazama aina ya teuzi zake zinavyokuwa makini.
Jana umesainiwa mradi mkubwa wa gesi, nadhani unaelewa faida zake kwa taifa hili kwa miaka mingi ijayo.