Waliomlazimisha Samia Suluhu kuwa Makamu na hatimaye Rais, walifanya makosa sana

Waliomlazimisha Samia Suluhu kuwa Makamu na hatimaye Rais, walifanya makosa sana

Wasio na mshahara wana sehemu tofauti za kununua mahitaji yao tofauti na wenye mishahara? Nadhani kuzuia inflation isiongezeke ndiyo sahihi zaidi kuliko kuongezea watu fulani mshahara..
Hayo ni maoni yako, na yale ni maoni yangu.
Inflation haijazidi wala kufika 23.3% ya mshahara iliyoongezwa na Samia Suluhu Hassan kiasi kwamba ifanye ongezeko la mshahara huo lisiwe na thamani
 
Kwa hiyo wakilala hadi saa nane ndio uibe kura halafu useme kiongozi aliyepatikana ni mapenzi ya Mungu..! mshahara wenu upo, wakati huo ndio utatia akili kichwani, sasa hivi akili haipo kichwani ipo kwenye tumbo.
Kilio kama hiki wamelia watu mpaka wakaondoka duniani huwa hakisaidii chochote kama hauamki na kuwa mstari wa mbele kubadilisha maisha yako.

SSH yupo Oman anatafuta wawekezaji, watakuja na kutajirika wakituacha tukizeeka na malalamiko yetu yasiyo na kichwa wala miguu.
 
Hayo ni maoni yako, na yale ni maoni yangu.
Inflation haijazidi wala kufika 23.3% ya mshahara iliyoongezwa na Samia Suluhu Hassan kiasi kwamba ifanye ongezeko la mshahara huo lisiwe na thamani
Ni vyema kwa kiongozi kutenda yale yanayoleta nafuu kwa watu wote..akidhibiti ongezeko la bei linagusa watu wote kuliko kuongeza mshahara kwa kundi fulani uamuzi unaosababisha ugumu zaidi wa maisha kwa wale wasio na mshahara..kiongozi haamui vile tu anataka kukufurahisha wewe ili uje kumsifia hapa.
 
Kilio kama hiki wamelia watu mpaka wakaondoka duniani huwa hakisaidii chochote kama hauamki na kuwa mstari wa mbele kubadilisha maisha yako.

SSH yupo Oman anatafuta wawekezaji, watakuja na kutajirika wakituacha tukizeeka na malalamiko yetu yasiyo na kichwa wala miguu.
Anafanya biashara ya wanyama kama kawaida
 
Kilio kama hiki wamelia watu mpaka wakaondoka duniani huwa hakisaidii chochote kama hauamki na kuwa mstari wa mbele kubadilisha maisha yako.

SSH yupo Oman anatafuta wawekezaji, watakuja na kutajirika wakituacha tukizeeka na malalamiko yetu yasiyo na kichwa wala miguu.
Hakuna kilio hapa, huu ndio ujumbe unapaswa kuusikia kila siku..hakuna mahali maskini wa fikra alitawala milele, ni suala la muda tu.
 
Hakuna kilio hapa, huu ndio ujumbe unapaswa kuusikia kila siku..hakuna mahali maskini wa fikra alitawala milele, ni suala la muda tu.
Wewe tajiri wa fikra utapotea tu kama upepo wa bahari unavyovuma, nii suala la muda pia.
 
Kwa mtazamo wangu, naona kabisa Mama Samia hakupaswa kuwa kiongozi mkubwa wa kitaifa. Kauli zake, mwenendo na maono yake vinadhihirisha wazi.

Ni kiongozi ambaye kwa kauli zake na maamuzi yake anaonesha wazi hakuwa na maono yoyote ya kuongoza taifa.

Teuzi za kulazimishana hufanyika sana hasa ndani ya vyama. Ifike mahali viongozi wa kiserikali wapewe fursa ya kuomba kuteuliwa na waeleze maono yao endapo watapewa nyadhifa hizo. Kuanzia ngazi urais, makamu, waziri mkuu na mawaziri wote.

Kabla mtu ajateuliwa, maombi yatumwe, na iundwe tume huru ya kuwafanyia usaili. Kuna watu wanaweza kupata teuzi ilihali hawana kabisa maono juu ya majukumu waliyopewa.

Matokeo yake wanakuwa kama bendera kufuata upepo!

NB: Haya ni maoni yangu tu kama Mtanzania. Sina chuki, wivu wala hasira na kiongozi yeyote. Tunachohitaji ni uzalendo wa kweli toka kwa viongozi wetu!
Una uhakika kulikuwepo kulazimisha? Ina maana kuna ushahidi alikataa cheo na akalazimishwa?
 
Acha kufuru., Kwani nani alitegemea JPM atafariki, Mbona Samia alipokuwa Makamo wa Rais hukusema haya maneno kwamba hakupaswa kuwa, Siku aliyochaguliwa kuwa Makamo watanganyika wote walipigwa makofi na kwakwa kwamba tumepata mahali pa kuwadanganya danganya wazanzibari kwamba mtu wao amepewa umakamo hivyo angalau watanyamaza, au kwa sababu sasa ni Rais unataka atokee mtu awe na mtazamo wa kuona baadae wakati hakuna zaidi ya mwenyewe Mungu

Tunasema ni majaliwa ya Mungu mama kuwa Rais., wewe unafkiri kuna mtanganyika angekubali Rais wa JMT atokee Zanzibar??? lakini unaonaje sasa uwezo wa Mungu? Je kuna mtu anaweza kuzuia?

Shida kubwa ni chuki dhidi ya Rais Mama samia kwamba ni mwanamke lakini ametoka Zanzibar anaiongoza vizuri NCHI., mumepigwa na mshangao kuona mwanamke muda mfupi anajaribu kunyoosha nchi iliyokuwa imevurugwa vurugwa na mwendazake., emu tafuta ile clip ya Benard Membe aliyosema hivi karibuni kuhusu Mama.
Watu wana chuki binafsi tu na mama huo ndiyo ukweli , ukiwaambia walete hoja wote mitini
 
Ulitakiwa kuainisha mapungufu yake ili tujiridhishe badala ya kuandika maneno ya wivu.
 
Inawezekana umekurupuka au una mihemko.
Hapa suala sio mtu kuwa kiongozi, isipokuwa ni utayari wa kuwa kiongozi.
Ukisikiliza hotuba nyingi za mama utagundua kwamba hakuwa na utayari kwa nafasi alizoteuliwa.
Huenda hatambui kwamba kauli zake kisiasa zinamfunga, au anaogopa lawama za moja kwa moja.

Kuna watoto wako shule za awali, msingi, sekondari nk, ukiwauliza ndoto zao watakwambia wanataka kuwa viongozi wakubwa wa kiserikali. Hayo ni maono yao. Na hao wakipewa fursa wanaweza kuwa viongozi bora tofauti na wale wanaoteuliwa kwa lazima au kwa kujuana. Hiyo ndio hasa hoja yangu.

Wakati niko chuo fulani, kuna dada alilazimishwa kuwa katibu wa bunge pasipo matakwa yake. Alisema wazi yeye hajui chochote khs majukum hayo ya ukatibu na hakuitaka hiyo nafasi. Lakini kwasababu viongozi wa tume hawamkutaka aliyekuwa anagombea nafasi hiyo, wakamlazimisha agombee kwa maslahi yao. Katika nchi yetu huu ni mfumo.

Na ukumbuke kwamba uongozi wa serikali yetu sio wa kifalme, kusema kwamba unafuata ukoo!
Ni muhimu kuzingatia utayari wa anayeteuliwa. Kuna watanzania wengi sana wenye maono juu ya taifa lao.
Kwa hiyo kosa ni la nan? Maana wakati ni makamu wa Rais hakuna aliyemlonda ukiwamo wewe
 
Jiwe alifurahi sana kumpata mama SSH kama makamo wake ili kila kitu afanye yeye na, mwisho wa siku, sifa zote na utukufu kwa JIWE! ... ALIFANIKIWA!
LAKINI SASA MAMA ANAFANYA VIZURI KUMZIDI NA PIA AKIUSHIRIKISHA UMMA IPASWAVYO! ... HATA MIMI MPINZANI NAMKUBALI, ... SHIDA MATAGA MNATAKA KUONGOZWA NA MUNGU-MTU ILI MJIFICHE NYUMA YAKE KUENDELEZA UFISADI!
Hakika
 
Hata mwenda... hakua na sifa wala uwezo wa kua rais sema timu Lowasa ndio walimuweka kwa hasira ya kukatwa mtu wao, matokeo yake badala ya kutuletea rais bora wakatuletea takataka ituongoze
Babako ndio alikuwa na sifa?
 
Wewe tajiri wa fikra utapotea tu kama upepo wa bahari unavyovuma, nii suala la muda pia.
Hakuna binadamu ameumbwa afurahie umaskini unaotokana na uduni wa kufikiri kama wako..ndio maana nakupa hii taarifa unachokifurahia hakitadumu..mgonjwa wa akili ndiye anaweza tetea kiwango cha kufikiri duni kama hiki..wote tungefikiri kama wewe na kuridhika na uduni sidhani leo hii ungekuwa umevaa nguo ulizovaa, binadamu bila kujali muda tunahitaji vitu bora zaidi..
 
Wewe mzima wa akili mbona unalialia tu humu JF?. Mbona hakuna cha maana unachofanya kubadilisha hali yako ya sasa ili iwe nzuri?.
 
Back
Top Bottom