Waliomlazimisha Samia Suluhu kuwa Makamu na hatimaye Rais, walifanya makosa sana

Huu ulikuwa mchongo wa JK
 

Mama Samia kuwa Makamu na hatimaye Rais alaumiwe JK​

 
Jiwe alifurahi sana kumpata mama SSH kama makamo wake ili kila kitu afanye yeye na, mwisho wa siku, sifa zote na utukufu kwa JIWE! ... ALIFANIKIWA!
LAKINI SASA MAMA ANAFANYA VIZURI KUMZIDI NA PIA AKIUSHIRIKISHA UMMA IPASWAVYO! ... HATA MIMI MPINZANI NAMKUBALI, ... SHIDA MATAGA MNATAKA KUONGOZWA NA MUNGU-MTU ILI MJIFICHE NYUMA YAKE KUENDELEZA UFISADI!
 
Wewe naona unazungumzia mambo ya katiba ya nchi na sio Samia, maana miaka yote mfumo wetu upo hivi hivi, wanaoteuliwa wengi kwa sababu ya connection zao na Rais
 
Wewe naona unazungumzia mambo ya katiba ya nchi na sio Samia, maana miaka yote mfumo wetu upo hivi hivi, wanaoteuliwa wengi kwa sababu ya connection zao na Rais
Ni kweli, suala kubwa ni mabadiliko ya katiba.
Ijapokuwa hata hii iliyopo kuna mahali haitekelezwi ipasavyo.
Na linapkuja suala la kupata viongozi kutoka upande wa pili wa muungano, mara nyingi upendeleo unakuwa mkubwa. Tofauti na wanaogombea kutoka bara.

Ukisiliza hotuba ya rais wa sasa wakati akiwa makamu anasema wazi kabisa kwamba hakuwa anatarajia kuwa na wadhifa huo na kwamba alikataa na kumwaga machozi. Mhe. Bilal akamtia moyo pamoja na viongozi wengine.

Kumlazimisha mtu kushika nafasi kubwa si jambo jema. Ndio maana nikasema watume maombi ya uteuzi!
 
Ungeanza kuuliza ilikuwaje mtu kama Jiwe akawa Rais. Au wewe ni sukuma gang?
 
Utayari ni upi? JK alikuwa na utayari wa kutosha ni nini aliwafanyia watanzania miaka 10 katiba ya nchi tu fedha nyingi zilipotea ikaishia kwenye makaratasi., mkapa nini aliwafanyia Watanzania? si aliwauwa wazanzibari kwa bunduki, JPM nini aliwafanyia watanzania? njaa, wizi, watu kutekwa, maiti kwenye viroba na matusi na kebehi.

Uongozi sio siasa na kupiga mdomo na kunyoosha maneno, uongozi ni kuwatumikia watu na muda mfupi kuona matokeo ya uongozi sio blaa blaa., wewe unataka kiongozi akisimama kwenye jukwaa akupe maneno mpaka uone ndani yake yana ladha ya sukari lakini watu wanaumia??

Mpeni muda mama, bongo kule wanasema mama anaupiga mwingi bado ni chuki tu ulizonazo., hatutaki kiongozi msanii.
 
Mbona Samia aliomba ridhaa kupitia CCM na alimaliza nafasi za juu kwenye ule mchujo
 
Nani anayefaa?
 
Hayo ungemuekeza tu mumeo ingetosha
 
Hakujawahi kuwa na rais aliyefaa Tanzania, inategemea na uwelewa wako binafsi na matarajio yako siku unakwenda kupiga kura.

Kuna mabilionea wanazaliwa awamu hii, kuna watu wanafurahia kufanya biashara ndani ya Tanzania ya sasa. Wewe unayelia kipindi hiki unayo haki ya kufanya hivyo pia.
 
Labda amuombe Mungu kila anapokwenda kanisani au msikitini ili atushushie malaika aje awe rais wetu. Kwa maana hakuna binadamu mwenye kufaa kuwa rais kwa akili hizi za kitanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…