Waliomteka Baba Wa Mikel Obi walijuta baada ya habari kumfikia Abramovic

Waliomteka Baba Wa Mikel Obi walijuta baada ya habari kumfikia Abramovic

[emoji1184][emoji2788] John Obi Mikel:
Baba yangu alitekwa nyara wakati nilipokuwa nikiichezea Nchi yangu Nigeria katika Kombe la Dunia la Mwaka 2018 lililopigwa nchini Urusi.

Tulikuwa tunakaribia kucheza dhidi ya Argentina.
Masaa mawili kabla ya mchezo nilipata simu kutoka kwa Ndugu yangu akisema baba yangu alitekwa.

Zamani aliwahi kutekwa nyara, ilitushangaza, lakini hii ya mara ya pili ilikuwa ya kushangaza na kustusha zaidi kwa sababu nilikuwa karibu kwenda kukiputa katika moja ya mchezo mkubwa maisha mwangu.

Sikuweza kuondoka kwenye chumba.
Sikuweza kumwambia mtu yeyote.
Nilikuwa peke yangu katika chumba kwa muda wa dakika 30 huku nikifikiria nifanye nini?

Timu nzima ya Nigeria tulikuwa kwenye maandalizi makubwa kwa maana tulikuwa karibu kuingia katika mchezo mkubwa wa maisha yetu. Tulikuwa karibu kucheza dhidi ya Lionel Messi na Argentina.

Sikuweza kumwambia Mtu yeyote katika Timu yetu kwa maana ningeweza kuwavuruga wenzangu na kuwatoa kwenye mawazo ya Mchezo.

Lakini akili ya haraka ikanijia na nikakumbuka kumpigia Simu Mwamba Roman Abramovich na kumueleza juu ya yote yaliomkuta Baba yangu.

Mwamba ni Mwamba tu, Roman aliniuliza je umeshaongea na Mtu yeyote kwa msaada?!

Nami nikamjibu hapana, na kumwambia baada ya kupokea Simu toka kwa Ndugu yangu sijaongea na Mtu yeyote zaidi yako.

Kisha Roman akaniuliza Je, unataka mimi kuwatuma watu kwenda kumuokoa Baba yako akiwa hai?!

Nilipigwa na butwaa, sikuweza ongea chochote wala kujibu lolote.

Kisha Roman akaniambia usiwe na wasiwasi juu ya hilo. Nijulishe kama unataka chaguo hilo, naweza kufanya hivyo muda wowote kuanzia hivi sasa.

Siku 4 baada ya mchezo dhidi ya Argentina, baba yangu aliachiliwa huru bila gharama yoyote, na hata waliomteka hawajajulikana mpaka Leo.

View attachment 2811907View attachment 2811908
Unyama mwingi ...
 
Hiyo ndiyo maana ya utajiri na umafia...
Usikute yeye aliwapigia tu jamaa zake ambao wapo CIA na KGB wakamwambia kesi ndogo hiyo, hiyo ndiyo maana ya connection sio konekishen sijui ya video ya nani imevuja watu waone papachu za watu halafu wajichukulie sheria mkononi.
Kabisa! Ni kama aliyekuwa CEO wa Nissan/Renault Carlos Ghosn alivyotoroshwa Japan akisubiri kesi ya ubadhirifu wa fedha. Mchezo ulichezwa na mtu mmoja tu, Ghosn akapakiwa kwenye sanduku la vyombo vya muziki akapandishwa ndege ya kukodi mpaka kwao Lebanon. Hapa duniani ukiwa na hela hushindwi kitu.
 
Hiyo ndiyo maana ya utajiri na umafia...
Usikute yeye aliwapigia tu jamaa zake ambao wapo CIA na KGB wakamwambia kesi ndogo hiyo, hiyo ndiyo maana ya connection sio konekishen sijui ya video ya nani imevuja watu waone papachu za watu halafu wajichukulie sheria mkononi.
Nimecheka hapo kwenye sheria mkononi [emoji1787][emoji1787]
 
Uyu mwamba ni Russian Spetsnaz,usa retired special forces ,Italian mafia...Japan kakamucho , Tanzania matofali komando
umesahau kuongeza kwamba ni Mojawapo wa wayahudi matajiri wenye uraia wa Urusi. yeye mwenyewe ana uraia wa Israel pia na nyumba Israel anayo pia.
 
Sasa hao watekaji walijuta vipi. Mbona uyo Obi Mikel alisema aliwalipa hela hao jamaa wamuachie mshua
 
Ukisikia ikisemwa Wabongo wape kichwa cha habari ndo hii sasa!

Hii habari binafsi nimeisoma toka kwa Source yake kabisa ikiwa kwenye lugha ya Malkia!

Hiyo Sentensi ya mwisho ya kusema baada ya siku 4 Mzazi wa Obi alipatana ....... Ni uongo... Wabongo kama kawaida yao wameiongeza.

Obi hakueleza namna mzazi wake alipatikana..
 
Hiyo ndiyo maana ya utajiri na umafia...
Usikute yeye aliwapigia tu jamaa zake ambao wapo CIA na KGB wakamwambia kesi ndogo hiyo, hiyo ndiyo maana ya connection sio konekishen sijui ya video ya nani imevuja watu waone papachu za watu halafu wajichukulie sheria mkononi.
Na zenyewe ni chafu hazijanyolewa cc Uwoya😂
 
Ndugu yangu. Issue ndogo tu hizi unanitukana tusi zito kama hilo. Katika maisha yangu yote sijawahi kuambiwa neno baya kama hili. Sawa ndugu
Pole hii tabia ya matusi mods wanailea Sana, ukute kajitu kanakokutukana hakana Mbele Wala nyuma kanaishi kwa kuombaomba pesa hata za bando.
 
Back
Top Bottom