Waliomuua Dkt. Isack wa Nyamongo HC wakamatwe haraka

BINTI 'ZUCHU' ADAIWA KUWA NA DR. ISACK SIKU NZIMA KABLA HAJAUAWA NYAMONGO!

Mpendwa,
Mimi ni mkazi wa Nyamongo katika Wilaya ya Tarime. Ninaomba kupitia kwako umma ujue mambo ya msingi kuhusu tukio la kutekwa na kuuawa kwa Dr. Isack Daniel Athumani.

Kwanza tunaomba ifahamike kuwa watu wa jamii ya Nyamongo tuliokuwa tunahudumiwa na Dr. Isack hatukuwa na tatizo naye. Ni kijana mmoja aliyekuwa na moyo wa kujituma kwenye kazi yake, alikuwa na moyo wa kujitoleo sana. Kama jamii hatukuwa na shida naye kwani ni mtu ambaye alikuwa social sana na wananchi. Kama jamii hatukuwahi kuona kitisho chochote kwa Dr. Isack alipokuwa miongoni mwetu, na tulishirikiana naye vyema hata kwenye matukio mengine ya kijamii hapa kijijini.

Marehemu Dr. Isack alikuwa anafanya kazi kama Mganga Mfawidhi katika Kituo cha Afya cha Nyamongo katika kijiji cha Kerende, Kata ya Kemambo, na alikuwa anaishi hapo hapo kituoni yeye na familia yake.

Siku ya tukio, Daktari alionekana akiwa kituoni hadi majira ya saa 3 usiku. Baada ya hapo, alielekea kwenye Bar moja iliyopo hapo Kijijini Kerende kwa jina la "Charles Bar and Guest House." Hiyo ni Bar ambayo ipo umbali chini ya kilomita 1 kutoka hapo Kituo cha Afya. Taarifa za watu waliokuwa naye pale Bar zinasema kuwa ilipofika majira ya saa 5 usiku, aliwaaga kwamba anaondoka kwenda kutafuta chakula Nyangoto (hii ni Senta kubwa iliyopo mbali kidogo na Kijiji cha Kerende).

Wakati anaondoka pale Bar aliondoka na binti mmoja maarufu kwa jina la "Zuchu" ambaye inasemekana kuwa ni Msukuma na alikuwa Mhudumu wa ile Bar. Pia taarifa zinasema kuwa marehemu alikuwa na mahusiono ya kimapenzi ya muda na huyo mhudumu wa Bar. Siku hiyo hiyo kabla daktari hajaondoka kituoni saa tatu usiku, huyu mhudumu alionekana pale hospitali kwenye Benchi akiwa anamsubiria daktari. Majirani wa eneo lile wanasema kuwa ilikuwa ni kawaida yake kwenda pale kumwona Dr. Isack. Wakati anaondoka pale Bar alitumia pikipiki yake ambayo ni mali ya serikali.

Wakati Dr. Isack anavamiwa, watu wa kwanza kufika eneo la tukio majira ya saa tano usiku, walimkuta huyo binti naye ametekwa pamoja na Dr. Isack. Kwa taarifa za awali ilionekana huyo binti alibakwa na wale watekaji na suruali yake ilichanwa na aidha kisu au panga. Japo kuna watu wanaojiuliza ni wabakaji wachane suruali ya binti yule bila hata kumchubua ngozi. Kama alibakwa au la hilo litabaki kuwa ni suala la kitabibu zaidi.

Usiku uleule Dr. Isack na yule binti walipelekwa Kituo cha afya Nyangoto kwa ajili ya kupatiwa msaada wa kuokoa maisha yao. Ilisemekana baada ya taratibu za kitabibu, binti alikabidhiwa mikononi mwa Jeshi la Polisi ambalo baadaye lilimwachia na kurudi kijijini. Wakati bado tupo msibani na taharuki, taarifa zinasema Polisi walimfuata yule binti, baada ya muda akarudi tena kwa boda boda. Lakini sisi hatukujua tena kilichokuwa kinaendelea.

Jambo la msingi tunalohitaji kutoka kwenye vyombo vya dola ni kuhakikisha kuwa wahalifu wanapatikana na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Kwa kuwa siku ya kuaga mwili hapa Kerende, OCD wa Wilaya ya Kipolisi Nyamwaga alitamka hadharani kwamba wameanza kupata muelekeo wa kuwapata washukiwa wa uhalifu huo, tunaomba hiyo aliyosema OCD yatimie ili tumalize vitendo vya uhalifu katika jamii yetu.

Mwananchi wa Nyamongo
Tarime, Mara; 7 Mei 2023
Watu wa tarime wana roho mbaya sana

USSR
 
Ahsante sana kwa uzi huu uliotoa mwanga kidogo kuhusiana na kifo hiki cha Doctor, my blame ni kwa police, hawa jamaa ni bado sana na hawataki kwenda na technology ili isaidie case kama hii,why mpaka leo police hawana foresinc lab yao?,nini police walikikusanya pale kwenye crime scene?,je ilikuwa secured vema ili evidence isipotee?,home affairs pls anza mchakato wa kutoa IDs kwa watanzania wote including to capture finger prints na kuzihifadhi kwenye systems, pikipiki ni mine gold ya evidence, huyu dada ni key witness to Crack hii case, ningekuwa na uwezo jeshi lote la police ningelifumua,all above 40yrs wastaafu, ingiza graduates wengi wa 25yrs to 30yrs
 
Graduates wenye akili hamuwachukui ktk recruitment mnakesha kuweka vigezo vya JKT na upumbavu kama huo. Hutapata wenye akili ktk Pool..
 
Ahsante sana kwa uzi huu uliotoa mwanga kidogo kuhusiana na kifo hiki cha Doctor, my blame ni kwa police, hawa jamaa ni bado sana na hawataki kwenda na technology ili isaidie case kama hii,why mpaka leo police hawana foresinc lab yao?,nini police walikikusanya pale kwenye crime scene?,je ilikuwa secured vema ili evidence isipotee?,home affairs pls anza mchakato wa kutoa IDs kwa watanzania wote including to capture finger prints na kuzihifadhi kwenye systems, pikipiki ni mine gold ya evidence, huyu dada ni key witness to Crack hii case, ningekuwa na uwezo jeshi lote la police ningelifumua,all above 40yrs wastaafu, ingiza graduates wengi wa 25yrs to 30yrs
Siye above 40 tumewakosea nini jamani???..

Kwanza hao akina 25 na 30 ndo wana njaa balaa, yaani wakianza tu kazi wanawaza kutafuta hizo CROWN, X1 na mijengo. By the time wako 40 kama siye we are in the same boat..

Ishu ya Uwajibikaji kwa nchi yetu ni la kimfumo zaidi na wala si umri.

Ishu tu ya mwanafunzi wa UDOM wanaomba taarifa badala ya kufanya UCHUNGUZI...
 
Wote waliohusika na mauaji na ubakaji watashikwa tu. Jeshi la police Tanzania lina weledi sana linapofanya kazi kwa uhuru bila kuibgiliwa. Naliamini sana jeshi letu la police ni werevu na intelligent kuliko hata police wa ulaya na Marekani. Kwa nini nasema hivi kwasababu police wetu hawatumii technology kubwa sijui mbwembwe za forensic science sijui psychology sijui kuzungushia utepe sijui miDNA lakini wanapeleleza matukio hadi kuwashika watuhuumiwa.
 
Weledi wa Jeshi la poliso ndipo unapohitajika sasa...
Naingia chimbo hadi kesho asubuhi watashikwa wote kwasababu nataka kuisaidia Polisi.

Ni hivi Dokta itakuwa alikuwa anamgonga mke wa mtu. Wauaji wakaamua kumtumia huyo bar maid kumsogeza dokta wakamcharaza mna kumpigwaa miti kwa hiari na kuchana nguo maksudi kusingiziwa kabakwa
 
Siye above 40 tumewakosea nini jamani???..

Kwanza hao akina 25 na 30 ndo wana njaa balaa, yaani wakianza tu kazi wanawaza kutafuta hizo CROWN, X1 na mijengo. By the time wako 40 kama siye we are in the same boat..

Ishu ya Uwajibikaji kwa nchi yetu ni la kimfumo zaidi na wala si umri.

Ishu tu ya mwanafunzi wa UDOM wanaomba taarifa badala ya kufanya UCHUNGUZI...
Lengo ni kulifanya jeshi letu la police liwe la vijana weledi, dunia ya sasa ni technology sio mibavu, hawa vijana watakua trained vema na watakuja na attitude mpya,mfano tunapeleka vijana 500 Botswana wakajifunze kuwa traffic officer's,,(nchi hii almost ina zero corruption ),vijana 300 peleka pale USA wakajifunze kuhusu foresinc investigation, crime profile, 200 peleka pale UK, 350 peleka pale Israel wajifunze ili wawe special unit ya public order, hostages, ndio maana tunahitaji young graduates
 
Ahsante sana kwa uzi huu uliotoa mwanga kidogo kuhusiana na kifo hiki cha Doctor, my blame ni kwa police, hawa jamaa ni bado sana na hawataki kwenda na technology ili isaidie case kama hii,why mpaka leo police hawana foresinc lab yao?,nini police walikikusanya pale kwenye crime scene?,je ilikuwa secured vema ili evidence isipotee?,home affairs pls anza mchakato wa kutoa IDs kwa watanzania wote including to capture finger prints na kuzihifadhi kwenye systems, pikipiki ni mine gold ya evidence, huyu dada ni key witness to Crack hii case, ningekuwa na uwezo jeshi lote la police ningelifumua,all above 40yrs wastaafu, ingiza graduates wengi wa 25yrs to 30yrs
Tena kwa kukwambia tu, mimi kama mwajiri hao above 40, iwe ualimu, afya, polisi ndio wachapakazi. Hawa vijana wa under 30, hata kuandika hawajui.
 
Nakaribia kupata kitu sasa.

Siyo kila mtu anasema lake na kulaumu ovyo hadi wale waganga na manesi wenzake wanaongea hovyo huko tweeter eti 'ooh tuondoke wote' au tuwanyime huduma' nk.

Naendelea kujifunza tabia ya mwanadamu na kunapotokea jambo ni kuwa na subra kabla ya kukurupuka!.
 
Naingia chimbo hadi kesho asubuhi watashikwa wote kwasababu nataka kuisaidia Polisi.

Ni hivi Dokta itakuwa anamgonga mke wa mtu. Wauaji wakaamua kumtumia huyo Var maid kumsogeza dokta na kumpigwaa miti kwa hiari na kuchana nguo maksudi kusingiziwa kabakwa
yaweza kuwa ila cha kuongezea{ngoja nimalizie kaz hapa niwape wasichokijua}
 
Ahsante sana kwa uzi huu uliotoa mwanga kidogo kuhusiana na kifo hiki cha Doctor, my blame ni kwa police, hawa jamaa ni bado sana na hawataki kwenda na technology ili isaidie case kama hii,why mpaka leo police hawana foresinc lab yao?,nini police walikikusanya pale kwenye crime scene?,je ilikuwa secured vema ili evidence isipotee?,home affairs pls anza mchakato wa kutoa IDs kwa watanzania wote including to capture finger prints na kuzihifadhi kwenye systems, pikipiki ni mine gold ya evidence, huyu dada ni key witness to Crack hii case, ningekuwa na uwezo jeshi lote la police ningelifumua,all above 40yrs wastaafu, ingiza graduates wengi wa 25yrs to 30yrs
Watakuwa wamesoma mkuu. Hata sheria za uendeshaji wa makosa ya jinai zinahitaji maboresho. Ni lazima pia waache kufanya kazi kwa mazoea na pia kazi ya NIDA ilikuwa nini?
 
Vijana acheni umalaya Dr una mke unahamgaika na baamedi you don't care even about ur health, majanga mengine yakujitakia licha ya usomi shule haijamkomboa
 
Nakaribia kupata kitu sasa.

Siyo kila mtu anasema lake na kulaumu ovyo hadi wale waganga na manesi wenzake wanaongea hovyo huko tweeter eti 'ooh tuondoke wote' au tuwanyime huduma' nk.

Naendelea kujifunza tabia ya mwanadamu na kunapotokea jambo ninkiwa na subra kabla ya kukurupuka!.
Bado hakuna palipoonesha kosa la Doctor hapo kuondoka na mwanamke ndio kosa
 
Back
Top Bottom