Waliomuua Dkt. Isack wa Nyamongo HC wakamatwe haraka

Waliomuua Dkt. Isack wa Nyamongo HC wakamatwe haraka

Watu wa huko wanapenda sana shari asee…Kun siku nipo tarime nikaenda sehemu ya kula,nimeagiza msosi Ugali na nyama wakanilitea na kichuri ni kauli za hiki ni nini,yule mhudumu akanijibu kama hutaki acha!!! Nilishangaa sana.Kama mimi mteja najibiwa hivyo
 
Mkuu haya yote yalishafanyika, mpaka ukaanzishwa mkoa wa kipolisi Tarime-Rorya,

Kumbuka pia kambi ya jeshi ipo pale (Nyandoto), Jasiri haachi asili

Lakini Tarime ya miaka hiyo siyo Tarime hii, angalau kuna mabadiliko makubwa, vimebaki visa vichache vichache kama hiki cha huyu mpendwa wetu,

Kusema ukweli inauma sana.

nayajua hayo maeneo vizuri tena zama zile ambazo ilikuwa mbaya, hiyo kanda maalum ilikuwa busy na wizi wa dhahabu na upigaji wa hela pale Nyamongo sio kudeal na jamii korofi kama ilivyokuwa sababu kuu ya kuanzishwa kwake.

Bila shaka unafahamu matukio yaliyotokea Kibiti na action zake ambazo Serikali ilichukua, bila shaka unafahamu yaliyotokea pemba na action zake ambazo serikali ilichukua na mpaka wa leo hakuna mtu anayethubutu kurudia yale, unakumbuka vurumai za mabucha ya nguruwe na balaa la pale mwembechai?..

Ninaposema wanadekezwa na kuchekewa namaanisha, Niambie ni lini hawa watu na kujifanya kwao wakorofi walishafanya kama yale ya wahuni wa Kibiti au wapemba kule Zenji?... ukiangalia matukio yao meengi ni ya kishambashamba na kijingakijinga yalio na motives za kipumbavu tu... SERIKALI INAPASWA KUWA SERIOUS NA KUACHA KUWADEKEZA HAWA WAJINGAWAJINGA.
 
Naunga mkono hoja
 
Kibiti ulikuwa mchezo wa kihuni ambao ulikuwa organized, ni rahsi kudeal nao , sio rahs kudeal na matukio ya kisasi ambayo hayapo organized , Yani mnakaa Kwa Amani mara pap mtu kapigwa tukio , na zinakuwa sababu binafs na sio organized militants..... Haya unadeal nayo vipi??

Jamii za kanda ya ziwa mtu akiona unamzidi kila kitu na umemuonea sehemu sababu ya power uliyo nayo anachokifanya ni kutafta namna akudhuru , ndo wapo hvo yaan , hata ukipeleka jeshi likae kule jua tuu mkitofautiana na mtu anakuvizia akufanye kitu mbaya , sa sjui hlo jeshi litakuwa linakulinda mpak toilet

Mfano wewe ni umetokea DSM , ngozi soft joto limekung'arisha na uhandsome upo , na kama kawaida DSM watu wamezoea kutumia pesa na kuhonga ni kawaida , unafika huko Tarime mademu wanaanza kukushobokea na wewe unaona hapa ndo penyewe upite nao mmoja baada ya mwingine , aisee washkaji wa huko wenye hao mademu wakiona unawazid kila kitu ( muonekano + Pesa ) lazima wakufanye kitu mbaya , Yani ukiwa na demu hakikisha huyo demu yupo free na sio demu wa kubattle
 
Nashukuru umenisaidia kumjibu huyu rafiki yetu,
huwezi kufananisha matukio ya kigaidi na vimatukio vya wizi wa ng'ombe na matukio mengine madogo madogo yenye motives za mapenzi na visasi,

kule kuna wakati watu walikua wanagombana kwa sababu ya ardhi, koo fulani na koo fulani, koo moja ikishindwa inatafuta namna ya kulipiza kisasi, na kisasi cha Tarime mara nyingi ni Kifo, au kilema kisichopona

Shida ya Tarime wala si ugaidi, Tarime matukio yako disorganised kwakua kila tukio lina motive behind, ni ngumu kudeal na vitu vya namna hiyo
Kama ilivyo kwa maeneo kama Iringa kwa watani zetu wale ambapo ni rahisi kukuta mtu kajitundika(kujinyonga), Tarime ni rahisi kukuta mtu kachinjwa kama kuku

Ishu inakuja sasa, ni namna gani bora ya kuibadilisha jamii ile iache kufikiria kua njia pekee ya kumaliza tatizo ni kulipiza kisasi tena kwa namna mbaya zaidi ya kuua,
 
Ndugu yetu, Dr. Isack amezikwa leo kijijini kwao huko KASELYA - SINGIDA.

Lakini cha ajabu tukio hili halijaripotiwa katika chombo chochote cha habari na Serikali imepotezea kimya kimya.
IMG-20230506-WA0024.jpg
 
Huyu kijana nilimfahamu toka 2020.
Anaitwa ISACK DANIEL SIMA.
Ni Mnyaturu kwa kabila, mzaliwa wa Kijiji cha Kaselya wilaya ya Iramba.
Alizaliwa 1993 akasomea Shahada ya udaktari katika chuo cha st. Francis.
Ameacha Mke na mtoto mmoja.

Alikua ndo mtoto tegemezi katika familia yao.

Tukio limetokea Jana saa 5 usiku akiwa kwenye pikipiki na Mdada mmoja ambaye amebakwa na kulazwa hospital.

Waharifu wakaamua kumcharanga mapanga kijana wetu.

Mungu wangu tunaomba uoneshe hasira yako juu ya hawa shetani.

View attachment 2609933View attachment 2609934View attachment 2609935
Kwenye hii dunia huwezi amini km kuna matumbo ya kina mama yametoa viumbe makatili wanaofikia kudhulumu wenzao km vile wanaua sisimizi tu 🥲
 
Watu wa huko wanapenda sana shari asee…Kun siku nipo tarime nikaenda sehemu ya kula,nimeagiza msosi Ugali na nyama wakanilitea na kichuri ni kauli za hiki ni nini,yule mhudumu akanijibu kama hutaki acha!!! Nilishangaa sana.Kama mimi mteja najibiwa hivyo
Ha ha haaaaaaaaa.

Mie nilozoea kuishi maisha ya yakheee ndio nitakuweza huko!!
 
Hawa washamba ni kuwabadilisha tu mindset..

Hata ukiibiwa demu huna haja ya kulipiza kisasi kama wewe ni mtu mwerevu..unakaa chini unaangalia ulipozidiwa then unachapa mwendo.
 
BINTI 'ZUCHU' ADAIWA KUWA NA DR. ISACK SIKU NZIMA KABLA HAJAUAWA NYAMONGO!

Mpendwa,
Mimi ni mkazi wa Nyamongo katika Wilaya ya Tarime. Ninaomba kupitia kwako umma ujue mambo ya msingi kuhusu tukio la kutekwa na kuuawa kwa Dr. Isack Daniel Athumani.

Kwanza tunaomba ifahamike kuwa watu wa jamii ya Nyamongo tuliokuwa tunahudumiwa na Dr. Isack hatukuwa na tatizo naye. Ni kijana mmoja aliyekuwa na moyo wa kujituma kwenye kazi yake, alikuwa na moyo wa kujitoleo sana. Kama jamii hatukuwa na shida naye kwani ni mtu ambaye alikuwa social sana na wananchi. Kama jamii hatukuwahi kuona kitisho chochote kwa Dr. Isack alipokuwa miongoni mwetu, na tulishirikiana naye vyema hata kwenye matukio mengine ya kijamii hapa kijijini.

Marehemu Dr. Isack alikuwa anafanya kazi kama Mganga Mfawidhi katika Kituo cha Afya cha Nyamongo katika kijiji cha Kerende, Kata ya Kemambo, na alikuwa anaishi hapo hapo kituoni yeye na familia yake.

Siku ya tukio, Daktari alionekana akiwa kituoni hadi majira ya saa 3 usiku. Baada ya hapo, alielekea kwenye Bar moja iliyopo hapo Kijijini Kerende kwa jina la "Charles Bar and Guest House." Hiyo ni Bar ambayo ipo umbali chini ya kilomita 1 kutoka hapo Kituo cha Afya. Taarifa za watu waliokuwa naye pale Bar zinasema kuwa ilipofika majira ya saa 5 usiku, aliwaaga kwamba anaondoka kwenda kutafuta chakula Nyangoto (hii ni Senta kubwa iliyopo mbali kidogo na Kijiji cha Kerende).

Wakati anaondoka pale Bar aliondoka na binti mmoja maarufu kwa jina la "Zuchu" ambaye inasemekana kuwa ni Msukuma na alikuwa Mhudumu wa ile Bar. Pia taarifa zinasema kuwa marehemu alikuwa na mahusiono ya kimapenzi ya muda na huyo mhudumu wa Bar. Siku hiyo hiyo kabla daktari hajaondoka kituoni saa tatu usiku, huyu mhudumu alionekana pale hospitali kwenye Benchi akiwa anamsubiria daktari. Majirani wa eneo lile wanasema kuwa ilikuwa ni kawaida yake kwenda pale kumwona Dr. Isack. Wakati anaondoka pale Bar alitumia pikipiki yake ambayo ni mali ya serikali.

Wakati Dr. Isack anavamiwa, watu wa kwanza kufika eneo la tukio majira ya saa tano usiku, walimkuta huyo binti naye ametekwa pamoja na Dr. Isack. Kwa taarifa za awali ilionekana huyo binti alibakwa na wale watekaji na suruali yake ilichanwa na aidha kisu au panga. Japo kuna watu wanaojiuliza ni wabakaji wachane suruali ya binti yule bila hata kumchubua ngozi. Kama alibakwa au la hilo litabaki kuwa ni suala la kitabibu zaidi.

Usiku uleule Dr. Isack na yule binti walipelekwa Kituo cha afya Nyangoto kwa ajili ya kupatiwa msaada wa kuokoa maisha yao. Ilisemekana baada ya taratibu za kitabibu, binti alikabidhiwa mikononi mwa Jeshi la Polisi ambalo baadaye lilimwachia na kurudi kijijini. Wakati bado tupo msibani na taharuki, taarifa zinasema Polisi walimfuata yule binti, baada ya muda akarudi tena kwa boda boda. Lakini sisi hatukujua tena kilichokuwa kinaendelea.

Jambo la msingi tunalohitaji kutoka kwenye vyombo vya dola ni kuhakikisha kuwa wahalifu wanapatikana na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Kwa kuwa siku ya kuaga mwili hapa Kerende, OCD wa Wilaya ya Kipolisi Nyamwaga alitamka hadharani kwamba wameanza kupata muelekeo wa kuwapata washukiwa wa uhalifu huo, tunaomba hiyo aliyosema OCD yatimie ili tumalize vitendo vya uhalifu katika jamii yetu.

Mwananchi wa Nyamongo
Tarime, Mara; 7 Mei 2023
 
Back
Top Bottom