Waliomuua Dkt. Isack wa Nyamongo HC wakamatwe haraka

Waliomuua Dkt. Isack wa Nyamongo HC wakamatwe haraka

Nawasalimu wote wakubwa kwa wadogo,

Ni usiku wa kuamkia leo nimepokea taarifa kutoka kwa watu wangu wa karibu kua kuna daktari ameuawa kwa kukatwa katwa mapanga katika mji wa Nyamongo wilaya ya Tarime.

Daktari huyo kijana mdogo kabisa aliyekuwa akifanya kazi katika kituo cha Afya Nyamongo(Nyamongo HC) amekutwa na umauti huo wakati akiwa anaendesha pikipiki yake kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine katika mji huo.

Bado chanzo cha mauaji hayo hakijajulikana, na wala sina taarifa yoyote kuhusiana na kukamatwa kwa wahusika wa tukio hilo.

Ni aibu kubwa Kwa mji huo kumuua mtumishi tena kwa kumkata kata kwa mapanga wakati huu ambao kumekua na uhaba wa watumishi hasa kada ya afya katika maeneo ya pembezoni ya nchi. Je, ni nani atakubali kwenda kufanya kazi katika eneo kama hilo ambalo linaonekana si salama tena kwa watumishi na ukizingatia ajira za TAMISEMI zimetangazwa juzi.

Haijalishi sababu ya kifo itakuwa nini lakini huu ni ukatili wa hali ya juu.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Dr Isack Sima Mahala pema peponi, Amina.
Siyo mke wa Mkurya,itakuwa ni binti wa Mkurya ndo chanzo. Kuna maeneo ya kuruka utakavyo pindi upendo kujifanya kijogoo lkn siyo TARIME.
 
Mbeya kuna kipindi zilikua zinatembea Nondo tu na mapanga.
Sa tatu lazima mjifungie?
Likizo niko huko nikaleta zarau Nikaenda kula ubwii kagrosari jirani e bana wale wauaji hawa hapa sa tatu.
Walinikosakosa ila tulitimuana sana hapo.
Hawajui hata niliwaachaje, nikarudi home mzima
 
Hatari sana kuna madogo walipigwa jembe za kichwa.Kuja kupata habari kumbe walikuwa wameenda kufatilia mchongo kwa mturuki-Tabora.Wakakutana na Mangosha na vijinzi vyao vya kubana ,jamaa wakawaungia kuwa watakua wezi wa ng'ombe tu.Watu wakanda ya ziwa wakiwa town kama mafala wakute chaka sasa.
[emoji1787]
 
Huyu kijana nilimfahamu toka 2020.
Anaitwa ISACK DANIEL SIMA.
Ni Mnyaturu kwa kabila, mzaliwa wa Kijiji cha Kaselya wilaya ya Iramba.
Alizaliwa 1993 akasomea Shahada ya udaktari katika chuo cha st. Francis.
Ameacha Mke na mtoto mmoja.

Alikua ndo mtoto tegemezi katika familia yao.

Tukio limetokea Jana saa 5 usiku akiwa kwenye pikipiki na Mdada mmoja ambaye amebakwa na kulazwa hospital.

Waharifu wakaamua kumcharanga mapanga kijana wetu.

Mungu wangu tunaomba uoneshe hasira yako juu ya hawa shetani.

View attachment 2609933View attachment 2609934View attachment 2609935
Havoc.....
 
Kuna mtaa ulkua unaitwa makaranga kpnd hicho xjui kwa sasa, kuona vijana wanatembea na kiganja cha binadamu ilkua kawaida sana. Kuna siku npo zangu Malecho na pisi yangu ya kikurya nataka kuchakata mbususu mara wakapita jamaa wanatangaza vita mwenzao kakatwa mkono halafu wakawa wanazunguka mtaani wanauonyesha. Hisia zote za kuchakata ziliishia hapohapo nikampa mkono wa kwaheri bhoke wangu[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
[emoji1787][emoji1787]
 
Mimi ni mhanga wa matukio hayo....

Kwa kuonewa tu.....

Kipindi nimemaliza chuo kikuu sina ramani nikawa ninazunguka na mkokoteni ninanunua "scrappers"....

Kama kawaida ya shughuli hizo unavaa "kikazikazi"...makwapa wazi n.k....(jamaa kumbe nilikuja kujua aliibiwa vitu vyake na mtu mrefu anayefanana nami)[emoji1787]

Siku moja ya mapumziko napita mtaani maeneo ya Kivule nikiwa sina KOKOTENI wala nini nilishtukia napigwa KWANJA la mgongo na kichwani baada ya kumpita na kumsalimia tena kwa bashasha huyo mwamba "45years" hivi....ni mwanajeshi yuko kambi moja huko Mbagala.....

Jamaa ni Mkurya na huwa anaonea watu sana mitaani....ana matukio mengi ya hivyo....niligeuka nikamuuliza kosa langu....jamaa akaniambia nikae chini.....

Nikamuambia siwezi kukaa chini....nilighadhibika yaani MSOMI ninayejitambua ninayebangaiza maisha napigwa tu kwa kuwa ni LOFA....namshukuru Mungu toka utoto nimeishi katika mazoezi ya sanaa "zetu zile"....kilichotokea ni historia.....nilikanda ile mikando iitwayo "KIBAMVUA"....tulipotenganishwa mjeshi hoi akawa anasema atanitafuta na kikosi cha Jeshi nikamuambia awalete halafu nione kama HATONISAHAU NA FAMILIA YAKE(amejenga na anaishi mtaani).....

Siku hizi akiniona ananiita mdogo wake kwa heshima[emoji1787]....ameniachia alama naye nimemuachia za kutosha za kwenda nazo kaburini.....

Ushamba, ushamba, ushamba tu wa baadhi ya watu....

#YetzerHatov[emoji120]
 
Back
Top Bottom