Waliomuua Dkt. Isack wa Nyamongo HC wakamatwe haraka

Waliomuua Dkt. Isack wa Nyamongo HC wakamatwe haraka

Hilo swala la undugu ndio kbs.. ndio moja ya sifa sasa ktk vyombo vya usalama.

Yaan kama ww ni mtt wa NYOKA bas na ww utakuwa NYOKA unapewa kipaumbele ndio maana ktk majeshi yamejazana makabila flan flan ambao kiuhalisia nature ya hilo kabila ktk swala la reasoning ni 0%.

Pia hii nchi haina ushindani ktk swala la Ulinzi.

Nchi za ughaibuni wana kampuni zinazojitegemea ktk maswala yote mfno ULINZI, KIINTELIJENSIA, Forensics and data/information gathering. YOTE yanafanywa na kampuni binafsi wakishindana na SERIKALI ila hapa kila kitu ni SERIKALI hakuna ushindani ndio maana kunakuwa na Uzushi Mwingi.

Ipo siku.
Halo tuna safari ndefu kufika nchi ya maziwa na asali nchi hii. Yani kigezo Sio ubora ni undugu na favoritism, na Kuna kabila yalishajimilikisha hivo nafasi na reasoning Yao inajulikana Iko low below average wanaoamini kwenye kutumia nguvu, wakati sikuhizi watu wamewekeza kwenye technology na kutumia akili kwenye mambo ya msingi
 
mapenzi lazima yawazike wengi sana...hadi tutakapojitambua tutakuwa tumeisha sana
 
Nilichosema mchana naona huyu kaja kuthibitisha sasa. Yawezekena huyo mhudumu ilikuwa chakula ya mtu dokta kadandia gari kwa mbele. Poleni sn wafiwa.
 
Dactari na barmed ila kichwa cha chini hakinaga adabu.

Dr mfawidhi ana cheo tiyari ni kioo cha jamii anajulikana to some extent sasa iweje anaokoteleza? Saa 5 usiku yuko bar? Then anaondoka na barmed bila kujua kuwa akitokaga barmed huyo ana wanaume wengine. So sad.
Anyway rip dr.ila uliuwawa na mambwana wa barmed wako.
 
hawa vijana wadogo madaktari wengi ni wahuni sana, huyu jamaa atakuwa anatoka na mke au demu wa mtu
 
BINTI 'ZUCHU' ADAIWA KUWA NA DR. ISACK SIKU NZIMA KABLA HAJAUAWA NYAMONGO!

Mpendwa,
Mimi ni mkazi wa Nyamongo katika Wilaya ya Tarime. Ninaomba kupitia kwako umma ujue mambo ya msingi kuhusu tukio la kutekwa na kuuawa kwa Dr. Isack Daniel Athumani.

Kwanza tunaomba ifahamike kuwa watu wa jamii ya Nyamongo tuliokuwa tunahudumiwa na Dr. Isack hatukuwa na tatizo naye. Ni kijana mmoja aliyekuwa na moyo wa kujituma kwenye kazi yake, alikuwa na moyo wa kujitoleo sana. Kama jamii hatukuwa na shida naye kwani ni mtu ambaye alikuwa social sana na wananchi. Kama jamii hatukuwahi kuona kitisho chochote kwa Dr. Isack alipokuwa miongoni mwetu, na tulishirikiana naye vyema hata kwenye matukio mengine ya kijamii hapa kijijini.

Marehemu Dr. Isack alikuwa anafanya kazi kama Mganga Mfawidhi katika Kituo cha Afya cha Nyamongo katika kijiji cha Kerende, Kata ya Kemambo, na alikuwa anaishi hapo hapo kituoni yeye na familia yake.

Siku ya tukio, Daktari alionekana akiwa kituoni hadi majira ya saa 3 usiku. Baada ya hapo, alielekea kwenye Bar moja iliyopo hapo Kijijini Kerende kwa jina la "Charles Bar and Guest House." Hiyo ni Bar ambayo ipo umbali chini ya kilomita 1 kutoka hapo Kituo cha Afya. Taarifa za watu waliokuwa naye pale Bar zinasema kuwa ilipofika majira ya saa 5 usiku, aliwaaga kwamba anaondoka kwenda kutafuta chakula Nyangoto (hii ni Senta kubwa iliyopo mbali kidogo na Kijiji cha Kerende).

Wakati anaondoka pale Bar aliondoka na binti mmoja maarufu kwa jina la "Zuchu" ambaye inasemekana kuwa ni Msukuma na alikuwa Mhudumu wa ile Bar. Pia taarifa zinasema kuwa marehemu alikuwa na mahusiono ya kimapenzi ya muda na huyo mhudumu wa Bar. Siku hiyo hiyo kabla daktari hajaondoka kituoni saa tatu usiku, huyu mhudumu alionekana pale hospitali kwenye Benchi akiwa anamsubiria daktari. Majirani wa eneo lile wanasema kuwa ilikuwa ni kawaida yake kwenda pale kumwona Dr. Isack. Wakati anaondoka pale Bar alitumia pikipiki yake ambayo ni mali ya serikali.

Wakati Dr. Isack anavamiwa, watu wa kwanza kufika eneo la tukio majira ya saa tano usiku, walimkuta huyo binti naye ametekwa pamoja na Dr. Isack. Kwa taarifa za awali ilionekana huyo binti alibakwa na wale watekaji na suruali yake ilichanwa na aidha kisu au panga. Japo kuna watu wanaojiuliza ni wabakaji wachane suruali ya binti yule bila hata kumchubua ngozi. Kama alibakwa au la hilo litabaki kuwa ni suala la kitabibu zaidi.

Usiku uleule Dr. Isack na yule binti walipelekwa Kituo cha afya Nyangoto kwa ajili ya kupatiwa msaada wa kuokoa maisha yao. Ilisemekana baada ya taratibu za kitabibu, binti alikabidhiwa mikononi mwa Jeshi la Polisi ambalo baadaye lilimwachia na kurudi kijijini. Wakati bado tupo msibani na taharuki, taarifa zinasema Polisi walimfuata yule binti, baada ya muda akarudi tena kwa boda boda. Lakini sisi hatukujua tena kilichokuwa kinaendelea.

Jambo la msingi tunalohitaji kutoka kwenye vyombo vya dola ni kuhakikisha kuwa wahalifu wanapatikana na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Kwa kuwa siku ya kuaga mwili hapa Kerende, OCD wa Wilaya ya Kipolisi Nyamwaga alitamka hadharani kwamba wameanza kupata muelekeo wa kuwapata washukiwa wa uhalifu huo, tunaomba hiyo aliyosema OCD yatimie ili tumalize vitendo vya uhalifu katika jamii yetu.

Mwananchi wa Nyamongo
Tarime, Mara; 7 Mei 2023

Nilisema ni umalaya mkasema hapana,
Nyamongo ukigusa mke wa mtu kubali mapanga
 
Attachments

  • IMG_9905.MP4
    8 MB
Graduates wenye akili hamuwachukui ktk recruitment mnakesha kuweka vigezo vya JKT na upumbavu kama huo. Hutapata wenye akili ktk Pool..
Hizo akili mnazozisema ni zipi?
Kuwa na degree haimaanishi una akili.Akili ni kitu tofauti sana na unavyofikiri.
Graduates wengi ni wale wenye vipaji vya kukumbuka na kuiga maandishi.Akili ni kitu ambacho mtu anazaliwa nacho hakipati shuleni wala chuoni.
 
Polisi wanamkamata Mtu ambaye ndio chanzo cha kifo na tena alihusika katika tukio kisha wakamwachia then wakamtafuta tena, UJINGA GANI HUO?

Hawa ni Polisi waliopitia mafunzo kweli?
 
Lengo ni kulifanya jeshi letu la police liwe la vijana weledi, dunia ya sasa ni technology sio mibavu, hawa vijana watakua trained vema na watakuja na attitude mpya,mfano tunapeleka vijana 500 Botswana wakajifunze kuwa traffic officer's,,(nchi hii almost ina zero corruption ),vijana 300 peleka pale USA wakajifunze kuhusu foresinc investigation, crime profile, 200 peleka pale UK, 350 peleka pale Israel wajifunze ili wawe special unit ya public order, hostages, ndio maana tunahitaji young graduates
Graduates wa hapa kwenye majalala

USSR
 
Nakaribia kupata kitu sasa.

Siyo kila mtu anasema lake na kulaumu ovyo hadi wale waganga na manesi wenzake wanaongea hovyo huko tweeter eti 'ooh tuondoke wote' au tuwanyime huduma' nk.

Naendelea kujifunza tabia ya mwanadamu na kunapotokea jambo ni kuwa na subra kabla ya kukurupuka!.
Waondoke tu wote wapeleke vitoto vyao vikatili ili wakauwane wao kwa wao
 
Sasa hyo kichwa ngumu ya kuona umalaya na kula wake za watu kumemuondoa kijana mdogo hivi hivi.
Remember Kuna unwritten laws Sasa vichwa ngumu Huwa hamsikii Hadi mlete machungu Kwa familia na hasara Kwa taifa
Kwani huyo bar maid ni mke wa mtu? Sioni kosa lolote mtu kujichukulia zake bar maid eti auwawe
 
Vijana acheni umalaya Dr una mke unahamgaika na baamedi you don't care even about ur health, majanga mengine yakujitakia licha ya usomi shule haijamkomboa
Kwenye mbonyeo hakunaga cha kaomando, msomi wala jambazi. Wote hukutanikia hapo
 
Hizo akili mnazozisema ni zipi?
Kuwa na degree haimaanishi una akili.Akili ni kitu tofauti sana na unavyofikiri.
Graduates wengi ni wale wenye vipaji vya kukumbuka na kuiga maandishi.Akili ni kitu ambacho mtu anazaliwa nacho hakipati shuleni wala chuoni.
Wengi wajinga wanadhani akili ni hayo makaratasi wanayotunukiwa vyuoni. Ingekuwa hivyo vyeti ni akili mbona sasa wameshindwa kujiajiri. Wengi wetu humu ni graduate na post graduate lakini angalia michango ndipo utajua hapana tofauti na polis wanaowalalamikia. Namna pekee ya kuwatofautisha na wale wa la saba ni ushamba wao wa mkanda nje na ujiaji lakini pesa mifukoni sifuri.
 
BINTI 'ZUCHU' ADAIWA KUWA NA DR. ISACK SIKU NZIMA KABLA HAJAUAWA NYAMONGO!

Mpendwa,
Mimi ni mkazi wa Nyamongo katika Wilaya ya Tarime. Ninaomba kupitia kwako umma ujue mambo ya msingi kuhusu tukio la kutekwa na kuuawa kwa Dr. Isack Daniel Athumani.

Kwanza tunaomba ifahamike kuwa watu wa jamii ya Nyamongo tuliokuwa tunahudumiwa na Dr. Isack hatukuwa na tatizo naye. Ni kijana mmoja aliyekuwa na moyo wa kujituma kwenye kazi yake, alikuwa na moyo wa kujitoleo sana. Kama jamii hatukuwa na shida naye kwani ni mtu ambaye alikuwa social sana na wananchi. Kama jamii hatukuwahi kuona kitisho chochote kwa Dr. Isack alipokuwa miongoni mwetu, na tulishirikiana naye vyema hata kwenye matukio mengine ya kijamii hapa kijijini.

Marehemu Dr. Isack alikuwa anafanya kazi kama Mganga Mfawidhi katika Kituo cha Afya cha Nyamongo katika kijiji cha Kerende, Kata ya Kemambo, na alikuwa anaishi hapo hapo kituoni yeye na familia yake.

Siku ya tukio, Daktari alionekana akiwa kituoni hadi majira ya saa 3 usiku. Baada ya hapo, alielekea kwenye Bar moja iliyopo hapo Kijijini Kerende kwa jina la "Charles Bar and Guest House." Hiyo ni Bar ambayo ipo umbali chini ya kilomita 1 kutoka hapo Kituo cha Afya. Taarifa za watu waliokuwa naye pale Bar zinasema kuwa ilipofika majira ya saa 5 usiku, aliwaaga kwamba anaondoka kwenda kutafuta chakula Nyangoto (hii ni Senta kubwa iliyopo mbali kidogo na Kijiji cha Kerende).

Wakati anaondoka pale Bar aliondoka na binti mmoja maarufu kwa jina la "Zuchu" ambaye inasemekana kuwa ni Msukuma na alikuwa Mhudumu wa ile Bar. Pia taarifa zinasema kuwa marehemu alikuwa na mahusiono ya kimapenzi ya muda na huyo mhudumu wa Bar. Siku hiyo hiyo kabla daktari hajaondoka kituoni saa tatu usiku, huyu mhudumu alionekana pale hospitali kwenye Benchi akiwa anamsubiria daktari. Majirani wa eneo lile wanasema kuwa ilikuwa ni kawaida yake kwenda pale kumwona Dr. Isack. Wakati anaondoka pale Bar alitumia pikipiki yake ambayo ni mali ya serikali.

Wakati Dr. Isack anavamiwa, watu wa kwanza kufika eneo la tukio majira ya saa tano usiku, walimkuta huyo binti naye ametekwa pamoja na Dr. Isack. Kwa taarifa za awali ilionekana huyo binti alibakwa na wale watekaji na suruali yake ilichanwa na aidha kisu au panga. Japo kuna watu wanaojiuliza ni wabakaji wachane suruali ya binti yule bila hata kumchubua ngozi. Kama alibakwa au la hilo litabaki kuwa ni suala la kitabibu zaidi.

Usiku uleule Dr. Isack na yule binti walipelekwa Kituo cha afya Nyangoto kwa ajili ya kupatiwa msaada wa kuokoa maisha yao. Ilisemekana baada ya taratibu za kitabibu, binti alikabidhiwa mikononi mwa Jeshi la Polisi ambalo baadaye lilimwachia na kurudi kijijini. Wakati bado tupo msibani na taharuki, taarifa zinasema Polisi walimfuata yule binti, baada ya muda akarudi tena kwa boda boda. Lakini sisi hatukujua tena kilichokuwa kinaendelea.

Jambo la msingi tunalohitaji kutoka kwenye vyombo vya dola ni kuhakikisha kuwa wahalifu wanapatikana na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Kwa kuwa siku ya kuaga mwili hapa Kerende, OCD wa Wilaya ya Kipolisi Nyamwaga alitamka hadharani kwamba wameanza kupata muelekeo wa kuwapata washukiwa wa uhalifu huo, tunaomba hiyo aliyosema OCD yatimie ili tumalize vitendo vya uhalifu katika jamii yetu.

Mwananchi wa Nyamongo
Tarime, Mara; 7 Mei 2023
Polisi wa nchi hii ni matutusa. so wanafanya kazi kwa misingi ya kitutusa.
 
Ahsante sana kwa uzi huu uliotoa mwanga kidogo kuhusiana na kifo hiki cha Doctor, my blame ni kwa police, hawa jamaa ni bado sana na hawataki kwenda na technology ili isaidie case kama hii,why mpaka leo police hawana foresinc lab yao?,nini police walikikusanya pale kwenye crime scene?,je ilikuwa secured vema ili evidence isipotee?,home affairs pls anza mchakato wa kutoa IDs kwa watanzania wote including to capture finger prints na kuzihifadhi kwenye systems, pikipiki ni mine gold ya evidence, huyu dada ni key witness to Crack hii case, ningekuwa na uwezo jeshi lote la police ningelifumua,all above 40yrs wastaafu, ingiza graduates wengi wa 25yrs to 30yrs
Kwa hiyo ukiondoa hivyo vizee hapo polisi ndio uingize hawa graduate vijana wanaokesha kubet, kutafuta video za connection mitandaoni, uchawa, kuuza mirungi, kutwa kushabikia Simba na Yanga?
 
Back
Top Bottom