Waliondamana Dar es Salaam kupinga mkataba wa bandari wakamatwa na polisi. Mratibu wa maandamano na wenzake 10 wanahojiwa na Polisi

Waliondamana Dar es Salaam kupinga mkataba wa bandari wakamatwa na polisi. Mratibu wa maandamano na wenzake 10 wanahojiwa na Polisi

Vijana waandamana jijini Dar es Salaam Tanzania kupinga mkataba wa bandari kati ya serikali na Dubai Ports World pamoja na muswada wa marekebisho ya sheria ya Usalama wa Taifa.

Vijana walioandamana jijini Dar es Salaam kupinga mkataba wa Bandari wamekamatwa eneo la Mnazi Moja.

========

WALIOANDAMANA WAISHIA MIKONONI MWA POLISI

Taarifa za awali zinaeleza kuwa vijana waliokuwa wameandamana kupinga Mkataba wa Bandari eneo la Mnazi Mmoja kuelekea Ikulu ya Magogoni Dar es salaam wamekamatwa na Jeshi la PolisiTaarifa zaidi zitawajia endelea kutufatilia

View attachment 2662138
Huyo Ben Saanane na bandari wapi na wapi?
 
😂😂😂😁😁😁 Jamaa kawatanguliza wenzie yeye katokomea .

Wajinga ndio Waliwao.

========

Jeshi la Polisi limewakamata baadhi ya vijana waliojitokeza kuandamana kupinga mkataba wa ushirikiano wa uendeshaji wa bandari kati ya Kampuni ya DP World na Tanzania.

Hata hivyo, mratibu wa maandamano hayo, Deus Soka katika hali ya kutofahamika, hajatokea kwenye maandamano hayo yaliyopangwa kuanzia Temeke na kuishia Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Mwananchi Digital ilipomtafuta kwa simu zake zote za kiganjani, hakupatikana na katika majina ya waliokamatwa na polisi pia jina lake halikuwepo.

Juni 15 mwaka huu Deus Soka ambaye aligombea udiwani katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, alitangaza kuitisha maandamano kupinga mkataba wa ushirikiano wa uendeshaji wa bandari kati ya Kampuni ya DP World na Tanzania.

Hata hivyo Juni 17 Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam likipiga marufuku maandamano hayo na kueleza kuwa, mtu aliyeandaa maaandamano hayo ameshajibiwa kwa barua akielezwa ni marufuku kufanyika maandamano yoyote.

Juni 10, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha azimio kuhusu pendekezo la kuridhiwa kwa mkataba baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la kuanzisha ushirikiano katika uendelezaji wa maeneo ya bandari nchini.

Pendekezo hilo liliwasilishwa bungeni Juni 10, na kupitishwa na Bunge baada ya wabunge kupata fursa ya kuchangia na kuishauri Serikali kuhusu mkataba huo.

Mwananchi
 
Hilo li askari limenenepeana kwa kula vya bure na vinono kutoka kwenye mali za Tanganyika yetu
 
Hilo li askari limenenepeana kwa kula vya bure na vinono kutoka kwenye mali za Tanganyika yetu
 
Ndo maana wanakufa maskini, nchi imejaa wapumbavu sana hii, maanadamo ya amani halafu wanazuia ili iweje?
 
Vijana waandamana jijini Dar es Salaam Tanzania kupinga mkataba wa bandari kati ya serikali na Dubai Ports World pamoja na muswada wa marekebisho ya sheria ya Usalama wa Taifa.

Vijana walioandamana jijini Dar es Salaam kupinga mkataba wa Bandari wamekamatwa eneo la Mnazi Moja.

========

WALIOANDAMANA WAISHIA MIKONONI MWA POLISI

Taarifa za awali zinaeleza kuwa vijana waliokuwa wameandamana kupinga Mkataba wa Bandari eneo la Mnazi Mmoja kuelekea Ikulu ya Magogoni Dar es salaam wamekamatwa na Jeshi la PolisiTaarifa zaidi zitawajia endelea kutufatilia.

Ujumbe umefika
 
🤭
 
Back
Top Bottom