Waliondamana Dar es Salaam kupinga mkataba wa bandari wakamatwa na polisi. Mratibu wa maandamano na wenzake 10 wanahojiwa na Polisi

Waliondamana Dar es Salaam kupinga mkataba wa bandari wakamatwa na polisi. Mratibu wa maandamano na wenzake 10 wanahojiwa na Polisi

Waandamanaji wamepangwa, hakuna cha maandamano wala mavi, the whole process ni scam

Kwani mmesahau tunatengeneza tatizo kisha tinalitatua wenyewe 😂😂
 
Hii inshu imekosewa mapema...

Lazima ajenda iwepo, na ajenda hiyo iwaunganishe...

Sasa mnaingia kwenye maandamano huku mumeshapasuliwa...

Wakristo huku... Waislamu kule...

Wengine Dp World... Wengine Ben saanane na Azory...

How?
 
Eti mama mpenda democracy, kumbe hana lolote na bado asubirie kichinjio 2025 labda waendelee kuiba kura
 
Jeshi la Polisi limewakamata baadhi ya vijana waliojitokeza kuandamana kupinga mkataba wa ushirikiano wa uendeshaji wa bandari kati ya Kampuni ya DP World na Tanzania.

Hata hivyo, mratibu wa maandamano hayo, Deus Soka katika hali ya kutofahamika, hajatokea kwenye maandamano hayo yaliyopangwa kuanzia Temeke na kuishia Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Mwananchi Digital ilipomtafuta kwa simu zake zote za kiganjani, hakupatikana na katika majina ya waliokamatwa na polisi pia jina lake halikuwepo.

Juni 15 mwaka huu Deus Soka ambaye aligombea udiwani katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, alitangaza kuitisha maandamano kupinga mkataba wa ushirikiano wa uendeshaji wa bandari kati ya Kampuni ya DP World na Tanzania.

Hata hivyo Juni 17 Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam likipiga marufuku maandamano hayo na kueleza kuwa, mtu aliyeandaa maaandamano hayo ameshajibiwa kwa barua akielezwa ni marufuku kufanyika maandamano yoyote.

Juni 10, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha azimio kuhusu pendekezo la kuridhiwa kwa mkataba baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la kuanzisha ushirikiano katika uendelezaji wa maeneo ya bandari nchini.

Pendekezo hilo liliwasilishwa bungeni Juni 10, na kupitishwa na Bunge baada ya wabunge kupata fursa ya kuchangia na kuishauri Serikali kuhusu mkataba huo.

#mwananchiupdates
#tunaliwezeshataifa
 
Hapo central mi napaogopa hata kusogea sitaki maana father house anafanya kazi hapo
Kumbe nisingekaa muda mrefu eeeh?[emoji847]
Ngoja niende nikaandamane[emoji23][emoji23]
Mtanitoa[emoji23]
 
Watu nyuma ya keyboard wana mkwala mkuu [emoji1]

Ova
Tanzania sio nchi ya kuamini watu, Watanzania ni waoga sana,
Hatujiamini

Tungekuwa twajiamini tungeanza maandamano tokea Magu yupo madarakani.
Ila yalipotangazwa maandamano nilifika posta pako kimya sana kuliko hata Jumapili
 
Back
Top Bottom