Waliondamana Dar es Salaam kupinga mkataba wa bandari wakamatwa na polisi. Mratibu wa maandamano na wenzake 10 wanahojiwa na Polisi

Waliondamana Dar es Salaam kupinga mkataba wa bandari wakamatwa na polisi. Mratibu wa maandamano na wenzake 10 wanahojiwa na Polisi

Hiyo ni kamba ndefu sana umeandika. JF ina members mamilioni. Sema wakati wa issues muhimu kama maandamano, huwa kila mmoja yuko very committed hawezi kupata muda wa kutokea.
Siku Profesa Lipumba akiitisha maandamano, ndo kidooogo naweza hata kuchungulia dirishani, Yule anakaaga frontline Hadi kuna clip moja polisi anamwambia we Profesa mzima unaungana na hawa watu wasiosoma🤣🤣🤣
 
Vijana waandamana jijini Dar es Salaam Tanzania kupinga mkataba wa bandari kati ya serikali na Dubai Ports World pamoja na muswada wa marekebisho ya sheria ya Usalama wa Taifa.

Vijana walioandamana jijini Dar es Salaam kupinga mkataba wa Bandari wamekamatwa eneo la Mnazi Moja.


========

WALIOANDAMANA WAISHIA MIKONONI MWA POLISI

Taarifa za awali zinaeleza kuwa vijana waliokuwa wameandamana kupinga Mkataba wa Bandari eneo la Mnazi Mmoja kuelekea Ikulu ya Magogoni Dar es salaam wamekamatwa na Jeshi la PolisiTaarifa zaidi zitawajia endelea kutufatilia.


MRATIBU WA MAANDAMANO AINGIA MITINI

Jeshi la Polisi limewakamata baadhi ya vijana waliojitokeza kuandamana kupinga mkataba wa ushirikiano wa uendeshaji wa bandari kati ya Kampuni ya DP World na Tanzania.

Hata hivyo, a mratibu wa maandamano hayo, Deus Sokkatika hali ya kutofahamika, hajatokea kwenye maandamano hayo yaliyopangwa kuanzia Temeke na kuishia Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Mwananchi Digital ilipomtafuta kwa simu zake zote za kiganjani, hakupatikana na katika majina ya waliokamatwa na polisi pia jina lake halikuwepo.

Juni 15 mwaka huu Deus Soka ambaye aligombea udiwani katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, alitangaza kuitisha maandamano kupinga mkataba wa ushirikiano wa uendeshaji wa bandari kati ya Kampuni ya DP World na Tanzania.

Hata hivyo Juni 17 Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam likipiga marufuku maandamano hayo na kueleza kuwa, mtu aliyeandaa maaandamano hayo ameshajibiwa kwa barua akielezwa ni marufuku kufanyika maandamano yoyote.

Juni 10, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha azimio kuhusu pendekezo la kuridhiwa kwa mkataba baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la kuanzisha ushirikiano katika uendelezaji wa maeneo ya bandari nchini.

Pendekezo hilo liliwasilishwa bungeni Juni 10, na kupitishwa na Bunge baada ya wabunge kupata fursa ya kuchangia na kuishauri Serikali kuhusu mkataba huo.


Mwananchi
Taarifa za kijinga kutufanya tuendelee kuwa watumwa
 
Polisi na serikali wameonyesha udhaifu wa hali ya juu kuzuia maandamano ya amani.

Wanaogopa nini?
 
Vijana waandamana jijini Dar es Salaam Tanzania kupinga mkataba wa bandari kati ya serikali na Dubai Ports World pamoja na muswada wa marekebisho ya sheria ya Usalama wa Taifa.


Mwananchi
Huyo askari Alie mkamata dada ana matako makubwa.....Big Booty 😊😊😊🤓🤓🤓

Mm ningekamatwa na hao maaskar ningewaambia washituke maana hata NYERERE NA MAGUFULI walikufa Kwa mashaka....

Mm ningewaambia hao maaskar waniue najua damu yangu ingekua chachu ya ukombozi wa bandari zetu.....

I know na ndio maana nimejiweka mbali na African politics 🤓🤓

Wasalaam
Wasalaam 🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿
 
he mahabusu tena ina maana mulilo keshafanya yake kuonekana anawajibika🤷‍♀️
Ndio! Sasa kama watu wanaleta vurugu barabarani tuwasaidieje? Ni kuwapeleka mahabusu unawasindikiza na teke moja la matako hawatarudia tena.🤣🤣🤣
 
Uandamane au usiandamane maazimio yao watapitisha tu!! Bongo unafiki umejaa sana yaani mtu anaratibu maandamano halafu anakula nyoya.Anawaachia msala muhangaike na mbu wa central.
 
Ndio! Sasa kama watu wanaleta vurugu barabarani tuwasaidieje? Ni kuwapeleka mahabusu unawasindikiza na teke moja la matako hawatarudia tena.🤣🤣🤣
sio sawa demokrasis hiyo mlosema mmefanya maridhiano iko wapi?
 
Back
Top Bottom