Walioruhusu picha hii itumike hawakuwa wajinga

Walioruhusu picha hii itumike hawakuwa wajinga

Tutakubaliana kuwa adhabu zilitofautiana, mfano waliotuhumiwa kutaka kufanya uasi hadi wahalifu wa mitaani na Yesu alihukumiwa kwa msingi wa sheria ya watu wake.

Kisa cha mashtaka hadi hukumu ya Yesu hakina tofauti sana na kisa cha mashtaka hadi hukumu ya Sadam Husein, kwa Yesu Mrumi alikuwepo kuangalia tu sawa na Mmarekani kwa Sadam alikuwa anaangalia tu.
Unajua kisiasa sababu ya kifo cha Yesu ni uhaini???
 
Kisai, long time no see you. I hope you are doing just fine 🙏

Picha zao ni kweli hazikuwepo ila Portraits zao zilikuwepo. Watu walitumia michoro kuhifadhi kumbukumbu
Walitumia michoro ya sura za watu au watu walitunza Elimu na mafundisho ya watu husika ?

Unaweza kututhibitishia hiyo ndiyo sura ya Yesu kweli ?
 
Seventh Day Adventist Church, baadhi yao walitaka kwenda ulaya bila passport wala nauli. Upuuzi dot Com
sasa kumbe unaongelea kundi la watu waliojitenga kutoka kwa wasabato....wale si wanaitwa wasabato masalia
unaposema wasabato awamuamini yesu wala utatu mtakatifu una ushahidi wa ayo mafundisho au ni utashi wako??
 
Uzi mzuri Mr. na ninaunga mkono hoja.

Binafsi ninapotazama picha yoyote ya Yesu akiwa na wale 12 basi huwa sikawii kumtambua Petro, bila kujali yuko sehemu gani katika picha!

Namtambuaje?
1. Siku zote petro huonyeshwa kama mwanaume mwenye nywele fupi zilizo sokotwa, kwasasa mtindo huo huitwa Jew-Fro.
2. Pia Petro alikuwa na umri mkubwa kuliko wenzake na pengine kukiko Kristo.

IMG_7342.jpg


[Jew-Fro]

Tazama picha za Yesu na wanafunzi wake.

IMG_7353.jpg


Jaribu kumtambua Petro kwenye picha ya ‘The last supper’ by Leonardo da Vinci.


IMG_7343.jpg


Umemtambua Petro.

IMG_7345.jpg



Hapo?

IMG_7346.jpg



IMG_7351.jpg


Hii ndio sanamu ya Mt. Petro kama inayopatikana huko Vatican.

Katika Biblia hakuna ‘reference’ yoyote kuhusu mtindo wa nywele au umri wa Petro, ajabu ni kuwa wachoraji na wachongaji wamekubaliana kuhus muonekano wa Petro karne nyingi baada ya kifo chake.

My take. Kama alivyoandika mleta uzi, muonekano huu wa Petro sio wa kubahatisha.

IMG_7353.jpg


Nawasilisha.
 
Haijalishi kama ni mataputapu, au zinamake sense. Bado zitabaki tu kua theory, not FACTS!

Kiufupi, haujathibitisha beyond reasonable doubts kwamba huo ndio muonekano wa Yesu!
You're missing the point sir...lengo la mada yangu sio kuthibitisha kwamba hiyo ndio picha ya Yesu bali ni kuwatazamisha watu kua inawezekana kweli hiyo inafanania au ndio yenyewe kwa sababu nilizoeleza.

Ukisoma btn lines dhima kuu ya mada yangu sio kuthibitisha picha sahihi ya Kristo
 
Uzi mzuri Mr. na ninaunga mkono hoja.

Binafsi ninapotazama picha yoyote ya Yesu akiwa na wale 12 basi huwa sikawii kumtambua Petro, bila kujali yuko sehemu gani katika picha!

Namtambuaje?
1. Siku zote petro huonyeshwa kama mwanaume mwenye nywele fupi zilizo sokotwa, kwasasa mtindo huo huitwa Jew-Fro.
2. Pia Petro alikuwa na umri mkubwa kuliko wenzake na pengine kukiko Kristo.

View attachment 2547510

[Jew-Fro]

Tazama picha za Yesu na wanafunzi wake.

View attachment 2547572

Jaribu kumtambua Petro kwenye picha ya ‘The last supper’ by Leonardo da Vinci.


View attachment 2547533

Umemtambua Petro.

View attachment 2547539


Hapo?

View attachment 2547540


View attachment 2547556

Hii ndio sanamu ya Mt. Petro kama inayopatikana huko Vatican.

Katika Biblia hakuna ‘reference’ yoyote kuhusu mtindo wa nywele au umri wa Petro, ajabu ni kuwa wachoraji na wachongaji wamekubaliana kuhus muonekano wa Petro karne nyingi baada ya kifo chake.

My take. Kama alivyoandika mleta uzi, muonekano huu wa Petro sio wa kubahatisha.

View attachment 2547574

Nawasilisha.
Mkuu ahsante kwa mchango wako nimejifunza kitu. Hata kwenye muvi mbalimbali Petro amekua akionyeshwa akiwa na nywele za namna hiyo.
Sio wajinga waliofanya hivyo yawezekana ndivyo ilivyokua
 
Nilipoanza tu kusoma uzi huu, hasa ulipowazungumzia Imhotep na Leonardo, nikafahamu kwamba hujafanya tafiti vizuri au umeegemea mlengo fulani. Dunia imekuwa na watu wengi wenye akili, katika nyakati tofauti ambao wameisaidia dunia kufika hapa ilipo leo. Mfano, msomi wa kiarabu Ibin Al-Haytham aliandika kitabu ambacho kilibadilisha mwelekeo wa sayansi ya dunia mpaka leo hii hadi kuwafunda wakina Leonardo.

Wanasayansi wakubwa wa Ulaya kuanzia Bacon, Kepler, Newton, Leonardo na Galileo walianza kufanya mapinduzi makubwa kwenye ulimwengu wa sayansi baada ya kusoma kazi za Al-Haytham ambazo zilitafsiriwa na Bacon. Dunia nzima leo, hakuna kazi ya kisayansi inayofanyika bila kutumia, The Scientific Method iliyobuniwa na Al-Haytham. Hata wewe unatumia, The Scientific Method kufanya mambo yako. Kusema Imhotep na Leonardo ndiyo watu wenye akili zaidi, ni matusi kwa ulimwengu wa sayansi.

Tuwekane sawa kwenye hili, halafu ndiyo tuje kuzungumzia suala zima la Vatican na Yesu.
Angalau ungemtaja Ibni Sinna /Avicenna ningekuelewa
 
Mheshimiwa
Kwanza fahamu kwamba ulichoweka hapa ni concpiracy tu hakuna uhalisia wowote kuhusu taswira ya Yesu. Hata ile shroud of Turin ni super hoax kwa sababu hakuna aliyechukua ile sanda na kuifanyia lolote. Mojawapo ya washuhudiaji wa sanda ya Turin wanasema kuwa ilitunzwa haikuharibika na kadhalika.

Ushuhuda pekee wenye nguvu kuwa Yesu alikuja na kuishi kwetu na hata kufa kwa ajili yetu ni kupitia Neno hai la Mungu na Kazi alizozifanya na anazoendelea kufanya kati yetu.
Roman Catholic ni Universal church lililobuniwa na kuandaliwa na dola la Rumi ndiyo maana Kanisa Katoliki linaongoza katika historia ya mauaji ya watu waliosimama kutetea na kuhubiri Injili ya kweli.
Tusimulie historia bila kuupotosha ukweli wa Injili kwa sababu hao unaosema ndiyo makao makuu ya Ukristo ni watumishi ambao Mungu hawakuwatuma kuleta makao makuu ya Ukristo duniani bali makao yetu makuu ni Mbinguni kwa Baba.
Sir naomba kujua wewe ni muabudu wa dhehebu lipi?
 
I hope y'all are doing just fine, It has been long time since I was here[JF Inteligence]
View attachment 2545863
Kuna mtu alileta mada humu akiuliza kwamba picha inayotumiwa na wakristo hasa wakatoliki ya mtu mmoja mzungu kua “ndie” yesu, je hiyo picha ni ya Yesu kweli? Akaongeza kwa kusema kwamba wakati yesu akiwepo kulikua hakuna teknolojia ya Photography wala Motion Picture…So wao waliitoa wapi picha hiyo na wana ushashidi upi kwamba yule ndio Yesu mwenyewe??

I’m glad you asked coz I would like to use this moment to Splendid Explain these stuffs to you!


Toka dunia kuumbwa, dunia imeshuhudia kuzaliwa kwa watu wawili wenye akili zaidi.watu hao walikua wenye uwezo wa kujifunza mambo wao wenyewe yaani Autodidacts na walikua wana uelewa na uwezo wa kufanya mambo meengi kwa wakati mmoja yaani Polymaths…watu hao si wengine bali ni Imhotep kutoka Misri ya zamani (Ancient Egypt) na Leonardo Da’Vinci kutoka Sicily Rome.

Imhotep alikuwepo duniani Zaidi ya miaka 5000 kabla ya kuzaliwa kwa Da’Vinci, Da’Vinci kazaliwa miaka 600 iliyopita yaani 1400s.Imhotep alikua kuhani mkuu wa mungu mkuu wa wamisri aitwaye mungu jua Ra, mbali na hayo jamaa alikua mbobevu katika hesabu,fizikia na biology hivyo alijikita sana katika usanifu wa majengo na tiba mbalimbali. Ukiziona Pyramids zilizopo misri wala usidanganyike kua alien ndio wamejenga bali ni huyu Inhotep ndio alizisanifu.

Wagiriki walimuabudu huyu mtu kama mungu wao wa tiba kutokana na mchango wake mkubwa katika tafiti zake zi kitabibu.

Kwa waliosoma mada zangu kadhaa zilizopita nilielezea jinsi utawala wa Ugiriki ulivyotokea na kuanguka na matokeo yaliyotokea baada ya ugiriki kuanguka. Kwa ambao hawajasoma nitaelezea kwa ufupi sana nini kilitokea.
Miaka ya nyuma ugiriki ya zamani ilikua imeundwa na miji ipatayo 100 na kila mji na ulikua na utawala wake japo walikua wakiungana na kusaidiana pindi uvamizi unapotokea, enzi hizo superpower wa dunia alikua Persia yaani Iran ya sasa. Iran ilikua inajitanua kwa kuvamia maeneo na kuyachukua hapo ndio alipoikaribia Ugiriki akitaka aanze kuchukua mji baaada ya mji, hapo ndio unakutana kisa cha mfalme Leonidas wa jiji la Sparta.

Vumbi ilitimka kweli kwa wapenzi wa muvi waliotazama muvi ya 300 na 300 Rise of Empire wanaelewa.
Baada ya vamizi kadhaa zilizokua zinafanywa na nchi kubwakubwa wagiriki wakaamua kuungana na kutengeneza nchi moja ya Greece. Mikaka ikaenda akatokea alexander the great akaikuza sana Greek, akaanzisha mji wake ulioitwa Alexandria katika nchi ya Misri. Kipindi hicho misri ilikua ndio hazina na kitovu cha Elimu dunia nzima.
View attachment 2545869
[Mwigizaji Gerald Butler aliyeigiza kama mfalam Leonidas wa sparta kutoka muvi ya ]

Wanafalsafa wengi na walienda hapo kusomea, hata mwandishi wa injili Luka alisomea hapo. Miaka ikaenda baada ya Ugiriki kuanguka Superpower aliyeibuka akawa Rome, Rome ilienda kuchukua kila kitu kilichokua misri wakakihamishia kwao. Maarifa yote yaliyokua Misri kwenye Maktaba ya kwanza kuanzishwa duniani yalihamishiwa Rumi.

Wakati nchi ya Israel ikitawaliwa na Rumi anazaliwa Yesu anafanya kilichomleta duniani kisha anafariki miaka 33 baadae, wafuasi wa Yesu wanaongenzeka na kupata ushawishi mkubwa katika serikali na maeneo mengi duniani.

Kwa wanaopenda Conspiracy, inasemaekana baada ya utawala wa Rumi duniani kuanza kuanguka watu wenye kufikiria mbali (futurist) wakiongozwa na mfalme Nero walikabidhi madaraka kwa wafuasi wa Yesu Kristo wa kipindi hicho ili Rumi iendelee kutawala dunia kupitia mlango wa nyuma (indirectly) ndipo ukristo ukatambuliko rasmi duniani kama Roman Catholic na wakapafanya Rumi kama ndio makao makuu ya Ukristo badala ya Yesrusalemu. (Sina uhakika kama nadharia hii ina ukweli ndani yake ila ina make sense sana maana wote twafahamu nguvu na ushawishi iliyonayo RC katika mataifa mbalimbali)

Miaka kadhaa tawala ya Rumi inaanguka, Ukatoliki ukawa umeenea maeneo mengi na ushawishi mkubwa ulimwenguni anazaliwa Leonardo Da’Vinci 1452, kutokana na uwezo mkubwa katika mambo mbalimbali kila alichokifanya kiliweza kua Perfecto. Davinci aliweza kuifanya tasnia ya uchoraji kua kubwa na yenye thamani sana kutokana na kazi zake bora na zenye kufikirisha za uchoraji.

Ni moja kat ya wachoraji wakubwa kuwahi ktokea hapa duniani kuna vitu kachora hakuna mwingine anayeweza kuchora labda urumie Powerful software…kama utanibishia jaribu kuchora duara na pembe nne vikiwa pamoja kama alivyochora mchoro wake wa Vitruvian man… Jamaa alikua anaweza kujichora yeye mwenyewe sura yake…Baadae anazaliwa Michelangelo ambae na kwa kiasi Fulani alijitahidi sana katika uchoroja unaweza kujionea michoro yake ya Sistine Chapel iliyopo hapo Vatican, lakini pia nae alibobea katika uchonganji (sculptures)
View attachment 2545902
[Sistine Chapel]
Inahusiana vipi na Picha ya Yesu…?

Kama nilivyoeleza huko juu Baada ya Ugiriki na Misri kuanguka na Rumi kuibuka kama Superpower alibeba maarifa yote yaliyokua Rumi na Ugiriki na kuyahamishia Roma, hivyo baada ya rumi kuanguka kanisa katoliki likabaki limeshikilia maarifa kutoka pande zote za dunia hasa misri,ugiriki na Israel. Leo hii hakuna taarifa au maarifa ambayo hayapo Vatican…Vatican inamiliki moja kati ya eneo lenye kulindwa Zaidi duniani ambalo hua haiingii huko mtu bila ruhusu maalumu…Hata Pope inabidi apate kibali kutoka kwa kiongozi wa Jesuists ndio anaweza kwenda huko.

Hivyo basi sidhani kwamba kanisa katopliki wanaweza kua wameshindwa kupata piacha ya yesu wakati wameweza kumiliki taaroifa za kutoka kila pande ya dunia. Kama Plato,Socrate, nk picha zao zipo na waliishi miaka mingikabla ya yesu haiwezekani yeye picha yake isiweze kupatikana.

Nimesema kipindi hicho taaluma ya uchoraji na uchongaji ilitumika Zaidi katika kuweka kumbukumbu za watu mbalimbali ndio maana leo ukiitaka picha ya Plato unaipata, kuna watu wamejaliwa uwezo mkubwa wa uchoraji unaweza kumuelezea kwamba Fulani sura yake ipo hivi na hivi na akaichora kama ilivyo. Njia hii hutumiwa sana na mashirika ya usalama hususan FBI na polisi. Tena sasa hivi kuna msaada wa softwares yaani ukimuelezea mtu anakutulea mchoro kama picha halisi…hivyo basi natumaini hata picha ya yesu watu wa zamani walitumia njia hiyo kuhifadhi taswira ya Kristo.

Ndio maana utakuta picha hiyo inayotumika sura yake ipo mahali pote sio tofauti. Hata miaka ya 1970s wakati wanaandaa filamu ya yesu walijaribu watu Zaidi ya waigizaji 200 ambao watafanana na Sura hiyohiyo ni Brian Deacon pekee ndio alifanikiwa kufit kwenye role hiyo kutokana na sura yake kufanana na sura inayotumika kuwasilisha taswira ya Kristo.
Ndio maana wasiojua wanapoona hiyo taswira ya yesu hua wanasema kwamba ni sura ya mwigizaji Brian Deacon…Si kweli, kwa maarifa waliyonayo RC hawawezi ruhusu hilo.

So kwa kuhitimisha ni kwamba Wakatoliki kukubali kuruhusu picha hiyo ya Yesu kutumika sio wajinga hata kidogo kwamba hawafahamu taswira halisi ya Kristo.​
Yesu alikuwa mzungu?
 
Mkuu wewe ni Shahidi wa Jehovah kiimani kama sijakosea. Hua hamuamini kama Yesu alitundikwa msalabani katika mti uliokaa kama jumlisha ➕ bali mti mmoja mnyoofu. So sishangai wewe kuona unasema Yesu alikua na nywele fupi.
Bila shaka ww pia ni RC hampendi kuchimba nyie binafsi maandiko, Mnalofundishwa mnabeba kama lilivyo bila kureason limetoka andiko gani.
Hakuna msalaba.
Yesu hakusema tusherehekee kuzaliwa kwake(xmass). Kwanza hakuzaliwa mwezi huo wa December ukitazama hata majira ya miaka ya kiyahudi.
 
Bila shaka ww pia ni RC hampendi kuchimba nyie binafsi maandiko, Mnalofundishwa mnabeba kama lilivyo bila kureason limetoka andiko gani.
Hakuna msalaba.
Yesu hakusema tusherehekee kuzaliwa kwake(xmass). Kwanza hakuzaliwa mwezi huo wa December ukitazama hata majira ya miaka ya kiyahudi.
Yesu hakuzaliwa ndio mwezi December, tunachofanya ni Kuadhimisha siku ya kuzaliwa Yesu kristo. Kuadhimisha sio lazima iwe siku ile ile tukio fulani lilipotokea.
So Yesu aliwekwa kwenye Msalaba wa aina gani?
 
With no offense, ulichokiandika hapa ni logical fallacy, not all well intuitive scientist , physicist, mathematician and astronomers wa mataifa ya ulaya i.e Germany, walikua influenced na Kazi ya bwana ibin al-haytham.

Of course he wrote a revolutionary book and we physicist are grateful for that, but science is contribution of many daring minds who devotedly ventured their minds into new horizons.
Usiandikie ushabiki ,
Also you've failed to instill the intent of Da'Vinci, he was trying to make a point that there has been a lot of artists who drew pictures into realistic Sense.
Such an Outstanding reply.
If you won't mind...What kind of scientist are you??
 
Mkuu kwa heshima kabisa sikubaliani na fikra yako kwasababu zifuatazo;

Yesu wakati wa uhai wake hakuwa mtu maarufu bali umaarufu wake umekuja miaka mingi baada ya yeye kufariki na habari zake kutangazwa. Sasa kama hakuwa maarufu ni wazi watu walimpuuzia ndio maana hata wakamuua kama waalifu wengine.

Ilihitajika awe mtu maarufu ndipo kumbukumbu zake ziwepo kwa watawala hasa picha sababu alitakiwa kulipia achorwe, kumbukumbu za Yesu zilizopo ni stori za mambo aliyofanya. Ni sawa na stori za babu wa machifu kabla ya kuja mkoloni kamwe hutaona picha zao bali stori tu.

Angalau kwa Mtume Mohammed yeye alieneza dini ya uislamu, ingekuwa rahisi sana kwa picha za Mtume kuwepo sababu yeye ndio mtu aliyekuwa nyuma ya uislamu tofauti na Yesu ambaye hata Ukristo wenyewe hakuuhubiri sababu yeye alikuwa myahudi na alitumwa kwao wayahudi.

Hii picha ni dhana tu au ndoto za wanadamu wa kipindi cha utambuko wakaamua kuileta tuitumie.

Jambo lingine ni uvaaji, huo uvaaji sio wa miaka hiyo watu wa zamani naweza kusema walikuwa rafu sana kuanzia nywele kichwani, ndevu zao hadi mavazi sasa yeye ilikuwaje akawa smart hivyo?, wakati alikuwa ni mtoto wa seremala tu? Mfano mzuri ni vikkings angalia walivyokuwa rafu na miaka waliyoishi ndio sembuse Yesu aliyeishi 2000 nyuma?.

Tubaki tu na imani ila hakuna uhalisia hapo.
Kwamba mpaka Wakuu wa Makuhani wanapanga kumuua hakuwa na umaarufu wowote?

Mtu hadi analisha watu elfu tano (na hao ni wanaume, wanawake hawajahesabiwa) unasema siyo maarufu?

Au nini maana ya maarufu/umaarufu, mkuu?
 
Wasabato mnaupinga utatu mtakatifu, mnapinga fumbo la imani. Kristo alikufa,Akafufuka na atarudi tena. Nyie ndio wapinga kristo
Sijawahi waelewa. Na bado wanasoma maandishi ya mtume Paulo na kubagua vyakula.
 
Back
Top Bottom