Waliosambaza taarifa potofu dhidi ya Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango kukiona cha mtema kuni. Waziri Nape atoa maelekezo

Tatizo linaanza na Serikali yenyewe. Makamu alipoindoka kwenda "kazi maalum", mungetoa taarifa kuwa amekwenda kwa kazi hiyo.

Munapokaa kimya, watu hujitafutia majibu.
 
Swali la mleta mada ni kosa au sio kosa kumzushia mtu kifo?(kwa mujibu wa sheria)
 
Hivi Kuna watu wanamchukulia Nape serious?
Mkuu Tindo tuachane na Nape ila mimi nataka kujua ni kosa au sio kosa mkumzushia mtu kifo?(tena mtu anaongea kwa kusisitiza utafikili kaiona maiti)
 
Tumemsikia Nape akisema kuwa wote waliosambaza habari za uongo kuhusu hali ya makamu wa rais Dr Philipo Mpango watakiona! Nafikiri yeye (Nape) kama waziri wa habari anapaswa kukiona kwa kushindwa kuwahabarisha watanzania kuhusu hali ya makamu wa rais na alipokuwa kwa kipindi cha mwezi mzima! Tanzania tuna utamaduni mbovu wa viongozi wetu kutokuwajibika kwa wananchi.
 
Swali la mleta mada ni kosa au sio kosa kumzushia mtu kifo?(kwa mujibu wa sheria)
Makosa yaanzia kwa kutowajibika.

Walioleta uzushi ni watumishi wote wa ofisi ya VP hawa wote walitakiwa wajiuzulu hadi sasa kwa kushindwa kuujulisha umma kiongozi wao yuko wapi.

Kabla ya kushughulika na tatizo tuanzie chanzo cha tatizo.


Dawa ya uzushi ni taarifa sahihi tu sio vinginevyo, hawa watumishi wa ofisi ya VP walishindwa kutolea nini ufafanuzi alipo.

Msemaji mkuu wa serikali yupo , waziri wa habari yupo na ndio huyo empty kabisa walishindwa nini kukanusha uvumi?

Kuna msemo unasema uongo ukiachwa ushamiri sana hugeuka kuwa ukweli.
 
Huyu kima ile bastola kumbe ilikuwa halali yake
 
Mbona VP mwenyewe ameshawasamehe na amewaombea msamaha kwa Mungu. Hao ni wa kupuuzwa tu kwani wamevuna aibu. Ila kwa upande wa serikali nao wanapokaa kimya kwenye jambo linalohitaji taarifa kwa umma ndiyo wanatoa nafasi kwa wazushi kuleta uzushi wao. Ninaamini wengine waliokuwa wanauliza alipo VP walikuwa wanauliza kwa nia njema kwani huyo ni kiongozi wao.
 
Uko sahihi kwa 100%
 
Mkuu Tindo tuachane na Nape ila mimi nataka kujua ni kosa au sio kosa mkumzushia mtu kifo?(tena mtu anaongea kwa kusisitiza utafikili kaiona maiti)
Kwa ufupi tu;

Ni kosa chini ya Sheria ya uhalifu wa Mitandaoni ya 2015.

Pia kama aliyesambaza Taarifa ni chombo Cha habari ni kosa chini ya Sheria ya huduma ya vyombo vya habari ya 2016

Lakini pia aliyezushiwa anaweza kufungua shitaka la Defamation dhidi ya aliyezusha na akamdai fidia

Cha muhimu Sheria zote hizo zimeweka vigezo, hivyo ni lazima vigezo vizingatiwe.
 
Makamu wa rais ni mtumishi wa serikali,wananchi kuhoji hawamuoni ni mahaba yao tu sio kosa.
Yuko tumemuona salama wala haina tabu.
Mnaanza kupeleka watu .
mahabusu Badala ya kutoa shukri.
Hivi Wananchi wamehoji au wamesema kabisa kuwa kafanyiwa opeshesheni ya..... na amefariki Dunia ila Serikali inachelewesha kutangaza tu kama kifo cha hayati?
Ninavyojua mimi kuhoji wangeuliza Makamu yupo wapi mbona hatumuoni wangeishinikiza Serikali waseme Makamu alipo ilawalichofanya wao ni kuzua taharuki kuwa Makamu ameiaga Dunia
 
Hii sii sawa bwana Nape, kwanini useme leo baada ya mzee wetu kujitokeza?! Huoni kwamba hata wewe ulikuwa na mashaka sawa na hao wengine waliothubutu kutapatapa kwa kuandika hisia zao mitandaoni??
Tena pengine kanuna kuona mwamba yupo hai!
 
Nitaamini hili limewezekana pale ambapo nitaona account ya kigogo haipo active
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…