Kupitia mtandao wa kijamii X, Waziri Nape Nnauye amesema kuwa ameelekeza vyombo vinavyohusika kuchukua hatua za mfano dhidi ya wote waliozusha na kusambaza taarifa za uongo dhidi ya Makamu wa Rais
Nanukuu
"Pole sana Mhe Makamu wa Rais. Tumekusikia. Kwakuwa tuna sheria zinazoelekeza mitandao itumike vizuri na kwakuwa tuna Taasisi na watu wa kusimamia sheria hizi, bila kuathiri uhuru wa watu, TUTACHUKUA HATUA kutokomeza matumizi haya mabaya ya mtandao! Naamini wote watatuelewa
Nimeelekeza vyombo vyote vinavyohusika kuchukua hatua za mfano, ili tujenge jamii inayoheshimu uhuru wa kila mtu. Uhuru wowote unapoingilia uhuru wa mwingine ni uvunjaji wa sheria, hatuwezi kujenga jamii inayoona hilo ni jambo la kawaida"