Mkuu 'utala utala TU', mimi napenda kuchangia katika swali lako ifuatavyo, na kwa namna hiyo nitakuwa nimejibu sehemu ya swali lako.
Ni hivi mkuu: Pamekuwepo na mpango wa siku nyingi wa kuunganisha gridi ya nchi za Kusini mwa Afrika, na ile ya nchi za kaskazini mwa Afrika kupitia nchi za Zambia, Tanzania na Kenya.
Umeme unaozalishwa kusini mwa nchi za Afrika, ukijulikana kuwa" Southern African Power pool" usafirishwe kwenye waya hizo, kuja Tanzania na kuendelea kuusafirisha kuelekea Kaskazini kupitia Kenya; na wakati panapokuwepo na upungufu kusini mwa Afrika, umeme huo usafirishwe toka Kaskazini.
Mpango huu umekuwepo kwa muda kitambo, na tumechukuwa hadi mikopo ya Benki ya Dunia kuutekeleza. Ni hivi majuzi tumekamilisha eneo la kuunganisha na Kenya.
Inavyo onekana sasa ni wazi kwamba palikuwepo na msukumo toka kwa kundi fulani kuukamilisha haraka mpango huu. Lakini katika mpango wote huu, uwepo wa Bwawa na Mwalimu Nyerere haukuwepo. Ina maana kwamba, uwepo wa Bwawa hilo kume athiri kiasi fulani mipango ya hao walio buni hiyo gridi ya Southern Power Pool na ile ya huku Kaskazini. Kwa bahati mbaya, sasa wapigaji hao wanaona wafanye kila liwezekanalo mpango wao wa mwanzo uendelee bila kujali uwepo wa umeme wa ziada hapa kwetu.
Hawa watu hata hawaoni aibu kufanya utapeli wa namna hii.
Kwa hiyo swala la "kutokuwepo nyaya zinazounganisha mikoa ya Kaskazini, hilo halipo kabisa. Kwani hata kabla ya hiyo gridi niliyo zungumzia hapo juu, mikoa hiyo ilikuwa ikihudumiwa na gridi yetu ya taifa iliyopo sasa.