Gift mzalendo
JF-Expert Member
- Dec 13, 2019
- 1,856
- 2,417
- Thread starter
-
- #21
Kama umemuelewa MTU ambaye hata muandiko wake hauleweki Basi wote mnafanana akiliAngalau umejaribu kumuelezea japo sio kwa kisayansi sana. Analaumu kumbe tatizo ni la kwake la kuwa na uelewa mdogo kwenye masuala ya nishati.
Kama maarifa ni kununua umeme unaotoka km maelfu kwa fedha za kigeni na kuucha umeme unaozalisha nyumbaniHakuna cha skendo tatizo letu tunalemazwa na udaku wa mitandaoni. Ni biashara inayofanywa na mataifa makubwa kina USA, Ujerumani na Japan sembuse sisi Watanzania.
Ukiwa tayari kununua umeme pia unao utayari wa kuuza umeme. Tutafute maarifa ili tupunguze haya malalamiko ya kitoto, yanatushushia heshima.
Hahahah. Unaambiwa kununua mchele ni ghali kuliko kununua wali.Hapa ni pamoja na viongozi watetezi wao akiwepo Mzee wa Pp anayeona Marekani haikoseagi kiuchumi
Huyu Anatuokotea Kila kitu nje Kama Dodoki bila kutuambia mazingira au Mfumo wa shirika la umeme la Marekani ukoje ni WA ushindani au Monopoly
Nchi inapambana walau tuongeze export ya maparachichi , tunapata Fursa ya kuuza umeme tunaiacha tunaenda kununua sisi ety
Hata Kama ndo mnatadharau wananchi lakini msidharau na viongozi wetu
Umeme wa Ethiopia chanzo chake ni mto Nile unaotoka nchini kwetu ziwa Victoria
Unaenda kuzalisha umeme nchi iliyoko maelfu ya kilometa unarudishwa nchini kwa maelfu ya kilometers tunauzia kwa mamamilion ya hela za kigeni
Inawezekanaje Ethiopia isafirishe umeme Hadi Kenya Namanga ipate faida lakini tupate hasara kusafirisha humu humu NDANI
Kama tunataka vyanzo mbadala tunatanunuaje chanzo kile kile kinachofanana Cha maji Tena yanayotoka nchini kwetu
Kwanini tusizalishe vyanzo vingine Kama solar upepo SINGIDA same, geothermal humu humu NDANI
Incase ikitokea ukame ?
Je mabwawa yaliyoko kaskazini nayo yanazalisha kwa hasara ?
Hata mtoto aliyesoma geography ya Darasa la tano utamweleshaje umeme KUTOKA Ethiopia ni rahisi kuliko Rufiji akuelewe ???
Uvumilivu wetu Kama wazalendo una mwisho pia
Kama hawatahojiwa Kuna siku tutachukua nchi yetu wazalendo tutawahoji
Sio tumalize uchaguzi tusikie skendo ya umeme wa Ethiopia haitusaidii
kuna siku watatuweka bondi kwa matajiri wakijua ni wafanyakazi wafaraoViongozi wamejua kuwa wanatuongoza sisi WAFU, hivyo wanajifanyia wanavyopenda.. Wakijua sisi ni kelele za chura
Matapeli wa nchi hii ndio hawa, hata chembe ya aibu hawana usoni mwao! Akina Hamza Johari ndio walanguzi wakuu wa mali za nchi hii, halafu mnageuka na kutudhihaki kama unavyo fanya hapa! Tena kwenye jambo la kipuuzi kama hili!Hakuna cha skendo tatizo letu tunalemazwa na udaku wa mitandaoni. Ni biashara inayofanywa na mataifa makubwa kina USA, Ujerumani na Japan sembuse sisi Watanzania.
Ukiwa tayari kununua umeme pia unao utayari wa kuuza umeme. Tutafute maarifa ili tupunguze haya malalamiko ya kitoto, yanatushushia heshima.
Bora hiyo, kuna siku tutaamka na kusikia nchi yoote imeuzwa, tufungashe virago tutafute pa kwenda.kuna siku watatuweka bondi kwa matajiri wakijua ni wafanyakazi wafarao
Hofu yangu kubwa ni kwa hawa viongozi kuendelea kuwepo baada ya huo unaoitwa uchaguzi.Uvumilivu wetu Kama wazalendo una mwisho pia
Kama hawatahojiwa Kuna siku tutachukua nchi yetu wazalendo tutawahoji
Sio tumalize uchaguzi tusikie skendo ya umeme wa Ethiopia haitusaidii
Mkuu 'utala utala TU', mimi napenda kuchangia katika swali lako ifuatavyo, na kwa namna hiyo nitakuwa nimejibu sehemu ya swali lako.Kuliza sio ujinga Jamani,nataka elimu tu mwenzenu,kama ntauliza swali la kipumbavu mniwie radhi sana,,mi nauliza tu,kwani hakuna uwezekano wa kuunganisha umeme unaoishia mikoa inayopakana ni iyo mikoa ya kaskazini ?au huu umeme wa strigo kuekea kaskazini mwa nchi unaishia wapi?
Huyo uliye mjibu hapa ni sehemu ya wakala muhimu wanao inadisha Tanzania sasa hivi.Kama umemuelewa MTU ambaye hata muandiko wake hauleweki Basi wote mnafanana akili
Na hizi akili za namna hii ndo zinazofanya viongozi waseme lolote bila kufikiria
Nakuelewa sana mkuu,shukraniMkuu 'utala utala TU', mimi napenda kuchangia katika swali lako ifuatavyo, na kwa namna hiyo nitakuwa nimejibu sehemu ya swali lako.
Ni hivi mkuu: Pamekuwepo na mpango wa siku nyingi wa kuunganisha gridi ya nchi za Kusini mwa Afrika, na ile ya nchi za kaskazini mwa Afrika kupitia nchi za Zambia, Tanzania na Kenya.
Umeme unaozalishwa kusini mwa nchi za Afrika, ukijulikana kuwa" Southern African Power pool" usafirishwe kwenye waya hizo, kuja Tanzania na kuendelea kuusafirisha kuelekea Kaskazini kupitia Kenya; na wakati panapokuwepo na upungufu kusini mwa Afrika, umeme huo usafirishwe toka Kaskazini.
Mpango huu umekuwepo kwa muda kitambo, na tumechukuwa hadi mikopo ya Benki ya Dunia kuutekeleza. Ni hivi majuzi tumekamilisha eneo la kuunganisha na Kenya.
Inavyo onekana sasa ni wazi kwamba palikuwepo na msukumo toka kwa kundi fulani kuukamilisha haraka mpango huu. Lakini katika mpango wote huu, uwepo wa Bwawa na Mwalimu Nyerere haukuwepo. Ina maana kwamba, uwepo wa Bwawa hilo kume athiri kiasi fulani mipango ya hao walio buni hiyo gridi ya Southern Power Pool na ile ya huku Kaskazini. Kwa bahati mbaya, sasa wapigaji hao wanaona wafanye kila liwezekanalo mpango wao wa mwanzo uendelee bila kujali uwepo wa umeme wa ziada hapa kwetu.
Hawa watu hata hawaoni aibu kufanya utapeli wa namna hii.
Kwa hiyo swala la "kutokuwepo nyaya zinazounganisha mikoa ya Kaskazini, hilo halipo kabisa. Kwani hata kabla ya hiyo gridi niliyo zungumzia hapo juu, mikoa hiyo ilikuwa ikihudumiwa na gridi yetu ya taifa iliyopo sasa.
Maneno mengi umeandika gazeti zima lakini utumbo mtupu. Umeshawahi kumtafuta huyo Mramba akuelezee kitaalam kwanini umeme unanunuliwa huko Ethiopia?Kwa hiyo ukishataja hayo mataifa unaona umemaliza Kabisa
Kwamba hayo mataifa hayawezi kukosea
Mfumo wao wa uchumi na level zao na sababu zao za uchumi zinafanana na za kwetu
Taifa linalopambana kuongeza export ya maparachichi ili liongeze fedha za kigeni unalinganisha mataifa makubwa yenye viwanda vikubwa yanayoexport na kuingiza mabillion ya fedha za kigeni
Yaani unaacha HUDUMA ambayo unameshagharamia kuzalisha nchini kwako unaenda kununua nje ili ufanane na Marekani
Badala tupambane kuongeza export tunakazana kuongeza import kwa HUDUMA ambazo tuna uwezo nazo ili tulingane na Ujerumani yenye heavy industry
Badala tuongeze fedha za kigeni Kwa kuuza umeme nje tunaenda kulipa fedha za kigeni kununua HUDUMA ya umeme ambayo uzalishaji wake umekamilika ili tufanane na Japan yenye maviwanda makubwa yanayozalisha na kuingiza fedha zakigeni
Kama wewe ni miongoni mwa wasomi Basi tuna hasara kubwa Sana kubwa Sana Kwa Taifa
Ni vizuri uhojiwe kwa uhujumu uchumi wa ada za wazazi
Tafuta uelewa mpana wa mada mbalimbali, usipende kuongea maneno mengi wakati elimu ni ya kuokoteza huko google.Kama umemuelewa MTU ambaye hata muandiko wake hauleweki Basi wote mnafanana akili
Na hizi akili za namna hii ndo zinazofanya viongozi waseme lolote bila kufikiria
Ungejua wanavyofanya kazi usiku na mchana usingekuja na hizi lawama za kudhani kila mtu mwenye cheo anao mpango wa kuiba mali ya umma. Punguza mazingira na sababu za kujirundikia dhambi.Matapeli wa nchi hii ndio hawa, hata chembe ya aibu hawana usoni mwao! Akina Hamza Johari ndio walanguzi wakuu wa mali za nchi hii, halafu mnageuka na kutudhihaki kama unavyo fanya hapa! Tena kwenye jambo la kipuuzi kama hili!
Umeme haununuliwi kama machungwa yanavyonunuliwa pale sokoni Tandale. Ethiopia wanauleta mpaka hapo Kenya na Kenya anatuuzia sisi, tukishawalipa Kenya huyo Muethiopia anamalizana na Mkenya.Kama maarifa ni kununua umeme unaotoka km maelfu kwa fedha za kigeni na kuucha umeme unaozalisha nyumbani
Kisa tu unacopy na kupaste mataifa makubwa yenye viwanda ambavyo return hayo sio maarifa ni ujinga