Waliosoma shule za kata na kuumbuliwa na kiingereza tukutane hapa

mimi nilijua tabia za kihaya zinaanzia ukubwani kumbe... Mhaya
 
Halafu mi hadi leo sikijui na hata nikijaribu kile cha kuombea maji bado mdomo unabwabwaja utafikiri sina ulimi.

Binti Sayunii pliz nifundishe kimombo.
Rahisi tukiamua,kujifunza tu..tafuta mtu ambae ana kingereza kizuri,ambae utakua unazungumza nae au kuchat mara kwa mara,..Muige anavyotengeneza sentence,anavyotamka maneno..kama kuna mtu hapo juu kakwambia I NEVER WENT THROUGH THAT SO I CANT RELATE,si umeona sentence imenyooka bila kosa la kisarufi? Mgande awe anakuchorea za kingereza,
 
Nikikumbuka una kariri dictionary πŸ˜‚πŸ˜‚ Nina rafiki yangu instead y kusema kolera anasema choleraa kama neno lilivyo
Nimecheka, nimekumbuka ktk Geog, Penumbra, yeye akasema "ripemberu" class nzima hoi kwa kucheka.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚, likawa jina lake la utani pale shule.
 
I never went through that, can’t relate ila pole mupenziiiiii

Hapo kwenye Sex - Sita, hebu nielezee ilikuwaje kuwaje ukaunda hivyo.
Mwalimu mkuu alikuwa anatoa mawaidha pale paredi kuhusu wanafunzi waliojamiiana katika stoo ya shule akaaendelea na mwaidha (kwa kiingereza) alipofika mishoni akasema "Is there anyone who committed sex here at school apart from these two partners" nilinyoosha mkono kwa kudhani kuwa mwalimu alisema "leo aliyewahi saa kumi na mbili asubuhI ni nani shuleni kati yenu nyote"


Kilichonikuta sikuelezi baada ya knyoosha mkono.

holoholo Mbaga Jr Nomadix
 
Haongera sana mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…