Waliowahi kupotelewa na ndugu au mtu wa karibu mje mtupe experience

Waliowahi kupotelewa na ndugu au mtu wa karibu mje mtupe experience

Inasikitisha Sana alikuwa mtu Mmoja mpole Sana hatukujua kama ni polisi mpaka siku alilipopotea baada ya askari wenzake kuja na kubomoa kwake na kukuta sale za polisi
Duuh watu wana siri yaani jamaa ni polisi na wazazi hawajui kuwa ni polisi
 
Mimi nilivyohitimu darasa la 7 nilitoroka nyumbani nikaenda visiwani kwa ajiri ya kuvua samaki ili nipate pesa ya kusomea secondary lkn niliacha barua nikiwaelezea nia yangu hiyo,hawakunitafuta kwakuwa walipata taarifa.

Watu wapuuzi ktk familia husababisha hali hii kutokea ijapo kwa baadhi ya watu wazima wengi hupotea kutokana na kufanya matukio maovu hasa sisi wanaume.

Nina dada yangu mkubwa ni mtu mmoja mpumbavu sana sema mimi niliamua kuondoa ukaribu naye ili awe anapata taarifa zangu kupitia ndugu wengine.

Mimi kukata miaka 15 bila kuongea naye wala kuonana ni kawaida wakati kwa ndugu wengine nikienda likizo ninaenda sana.

Poleni kwa mliokutwa na mikasa ya kupotelewa ndugu,jamaa na marafiki kiukweli jambo hili halifai hata sekunde 1.

Nilipotelewa na 2 boys ndani ya masaa mawili niliuchukia mkoa ule na ukizingatia hata mwaka nilikuwa sijamaliza baada tu ya kuripoti kazini niliwehuka.

Ilikuwa hivi;
Baada ya kuwa nimeajiriwa,nikaenda kuripoti baadae nikarudi nyumbani kuchukua familia.
Siku 15 tu baada yangu na familia yangu kuwasili ktk huo mkoa mke wangu aliugua sana.

Sasa kwakuwa haukua ugonjwa wa ki -biology ilibidi nimuombe mama mkwe aje anisaidie kuangalia watoto na kuuguza. Tulipambana miezi mitatu baadae akapona.

Sasa haya mambo ya kanisani mama mkwe akawa na binti mmoja hivi urafiki. Basi ikawa hivyo.
Sasa kutokana na dharura iliyotukuta watoto walichelewa kusoma hivyo mwezi flani hivi tukaamua tukawafanyie manunuzi ya vifaa vya shule.

Hao tukaingia mjini kati ambako huyu rafiki yake mama mkwe alikuwa akiishi na mmewe,lkn pia tulihitaji kuhama pale tulipokuwa tukiishi hivyo ilikuwa pia atupeleke kuangalia nyumba nyingine sehemu.

Sasa hawa watoto wetu akasema ngoja wabaki kwake wawe wanaangalia cartoon tukimaliza tuwspitie.
Basi ikawa hivyo.

Saa tisa mara kumi na mbili hii hapa,watoto hawapo na nyumba imefungwa.
Duh! Yaani mimi nimebaki na mabegi ya shule halafu watoto wangu wamechukuliwa?

Huyu dada akampigia simu mmewe,jamaa akamuambia "ni lini sisi tumekuwa na watoto hapo mpaka uniulize habari za watoto?

Sasa nikawaza,huyu jamaa mkewe kamuacha dukani,lkn sasa hivi duka kaliacha wazi lkn watoto nyumbani kwake hawapo maana yake nini?

Tuliongea mengi lkn kufupisha maneno ni kwamba huyu jamaa aliwatimua wale watoto ndani,wakakaa nje baadae kaja mpangaji mwenzao akawahoji hapo basi akawachukua,shukurani kwa watoto wangu walikuwa wanaweza kujieleza wakamuelekeza wanakoishi,walikuwa wamekariri baadhi ya njia,wakifika sehemu wanamuakbia kuwa huwa tukitoka kanisani tunapitia hapa mwishowe walifika nyumbani.

Sasa huyu mpangaji mwenzao kumbe haziivi,na hata huyu binti na mmewe pia wana mgogoro.
Kuja kujua watoto wameshafika nyumbani jasho lilishanitoka kwenye kucha mpaka kwenye meno.
 
Nikajua
2006 Kipindi Nimemaliza kidato cha nne nilienda moshi kwa demu wangu nilikaa wiki 4 sionekani nyumbani nimetafutwa kote sionekani,ndugu wamenitafuta vituo vyote vikubwa vya police sionekani,radio free africa mpaka ITV kile kipindi cha matukio,hospital zote za dar sionekani wakajua nimekufa.
Wakati nipo moshi mjini nakula bata na uyu demu kumbe kuna jirani aliniona ikabidi apige simu nyumbani kuwa ameniona! ndugu wakamwambia mpeleleze mpaka anapokaa,kweli akajua ninapokaa akawapa taarifa nyumbani siku ile ile bonge moja la crew la watu 8 wametoka dar mpaka moshi.
Sielewi ili wala lile ghafla nikasikia mlango ukigongwa kwenda kufungua nakutana na ndugu zangu,aisee nilichezea kichapo sio cha Dunia hii nilikula bakora nilichezea mbata balaa, kuna jamaa alinipa hifadhi kwake nae akajumuishwa katika kichapo tukachukuliwa msobe msobe mpaka moshi police .
ila uyo demu ndio mama chanja wangu nimemuoa
Nikadhani dem wa KIJITA,kumbe KICHAGA!
 
Bro, hata mimi Nina bro wangu aliondoka tangu 2001 hatukujua Yuko wapi Hadi 2017 tulipigiwa simu na mtu kuwa ndugu yetu Yuko kibaigwa(wilaya ya kongwa) nilimfuata nikamrudisha nyumbani lakini alikaa mwezi Mmoja tu akatoroka kuanzia hapo hatujawahi kumuona tena. Huwa akionwa na mtu yoyote anamjua anakimbia,. Kiufupi hataki ndugu zake tujue Yuko wapi na hataki kurudi nyumbani.
Siyo kwamba amepatia maisha ila ana maisha magumu sana.
Hili huwa linatuimiza sana ndugu zae ila mama ndiye huwa anaumia zaidi.
Ana matatizo ya akili ? Au yupo fresh

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Mjomba! Binamu yake bmkubwa alipotea mwaka 2000, alitafutwa kila sehemu akupatika, mwaka 2015 mama ake alienda kwa mganga kumuita(issue ya mganga sielewi chochote apa) baada miezi kadhaa
Jamaa alipatikan kilombero huko akiwa mahututi akurudishwa home

2017 akapata marder case lakini now yko free
 
Kuna jamaa tukiwa wadogo miaka ya 90 alikuwa ndio mtoto wa mwisho kwao kati ya 7. yeye mkubwa kidogo kwetu. Sasa hakuwa na hela kama ndugu zake. Baba yake akamwambia nenda kamuulize mama yako akuonyeshe baba yako. Mimi watoto wangu wana hela. Wazee wa Moshi nyoko zao, yule jamaa wala hakuaga alipotea mazima. Kama Bahati ya Mungu nikaja kumkuta Namibia Windhoek miaka ya 2008 kashaoa na uraia kabadili na ana hela hatari. Akawa mwenyeji wangu hakuna kipind kwenye maisha yangu nikula bata kama Wakati huo. Nilikuja kuwaambia nyumbani kwao nimemuona kijana wao hawakuamin walitoka ndugu zao wanne kumfuata na Baba yao na Jan la sale. Jamaa walivyoonana ni kila mtu kulia baba yake akaomba msamaha mengine code. Long live Masssawe. We ni mtu na nusu nilijifunza sana vitu vingi kwako bro.
Daaah acha hyo feeling..kuombwa msamaha na mzazi@mnajikuta wotee mnalia kama msiba
 
Kipindi kile Mkuu wa mkoa Makala aliposema ukimkosa mwanao politics nenda hospitali. Kipindi hiki kulikuwa na panyaroad sana

Kuna mdogo wangu mtoto wa baba mkubwa alipotea. Tulizunguka hospitali zote Dar, mochwari ndo usiseme. Tukaenda polisi Ostrrbay na vituo vingine wapi.

Kijana hakuonekana kwa siku tatu. Kila unapopita walimuona majuzi yake. Tukajua tu huyu sio kawaida take kipotea atakuwa amekufa

Siku ya nne huyo karudi yuko job hana hili wala lile. Napigiwa simu namfata namuliza kwa nini hukuwa unapatikana kwa siku 3? Ananijibu "mwanaume hatafutwi, umuliizaje mwanaume alikuwa wapi?"

Yule dogo no kum* kweli niliapa hata apotee miaka 20 simtafuti. Tutakutana Rombo kwenye matukio
Kasamehe tu. Ni katoto bro. Kwenda kaa mweni msheku akushingia mba. Msamehe tiki.
 
Kasamehe tu. Ni katoto bro. Kwenda kaa mweni msheku akushingia mba. Msamehe tiki.
Mwana shu nesukwa. Ngilesuva
Nilikagua maiti mwananyama mpaka Leo naota mandato ya ajabu.
 
Mwana shu nesukwa. Ngilesuva
Mboga aisee. Ini ngikumbuke ngete kaka ekaa dar kwete siku mama alemkabia simu alemkolea kwi. Acha anipigie simu kama kichaa. Mbona simpati fulani wakati naishi km 600 kutoka alipo aisee. Yani msheku uya aleva Sha msukwa kabisa aisee.
 
Mboga aisee. Ini ngikumbuke ngete kaka ekaa dar kwete siku mama alemkabia simu alemkolea kwi. Acha anipigie simu kama kichaa. Mbona simpati fulani wakati naishi km 600 kutoka alipo aisee. Yani msheku uya aleva Sha msukwa kabisa aisee.
DALALI MKUU ni mshaka wa kaa kabisa. Aledisha kaa toka 2017, usikute ni yeye huyo kama yako.

Namuonea huruma mama, mtoto gani hajali mama yake anapitia sonona. Mzazi anaona amefeli kweli
 
Back
Top Bottom