Waliowahi kuwa wanene au vibonge, tukutane hapa

Ipo sana , uvivu tuu yaani nikianza leo kesho naacha, Nilikimbiaga gym kisa mazoezi magumu yani yule tutorial alivoniona alinipigisha mazoezi nikahisi kufa kufa niliondoka na sikurudi tenaa.
Wewe hutaki kupungua aiseh!unakimbia mazoezi?[emoji23]
 
Daah....
Niko 56kg... Ila nikitembea nahema ka nini
[emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85]
Piga squats zinasaidia sana pumzi... Pia kama unaweza fanya bicycle movements...
 
Yaaaani unamaanisha kwa sasa una kilo 110 ??
The last time nimepima nilikuwa na 101 na ilikuwa december mwanzoni 110 nimefanya makadirio tuu maana nimeongezeka zaidi
 
Nilipokuwa form five na six shule fulani huko mbeya nilikua bonge jamani na hivyo mbeya maparachichi kibao ukichanganya na kande lenye harage lina tufunza funza weeee nilikua kama nataka kupasuka. Ila kwa sasa nipo simple na nikajua nikizaa ntafumukaa wala ndo kwanzaaa nakuwa vzr zaidi. 😱
 
Mimi nashindwa kufanya mazoezi wala diet, Nikifanya mazoezi two weeks haziishi naingia majaribuni napumzika[emoji21]
Mi kila siku lazima nikimbie asubuhi,maji ya uvuguvugu+limao daily lazima upungue,nna kamwili kadogo dogo ila sasa nikijiachia nna limwili km kiroba cha mwizi,nanenepa mpaka kichwa[emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…