Waluguru wanafukia ufuo wa maiti chumbani

Waluguru wanafukia ufuo wa maiti chumbani

Ndio utaratibu wa kiislamu unaposikia kuosha maiti.

Utaratibu wa kiluguru kabla ya kuinteract na waarabu haukuwa na maswala ya kukamua. Na maiti ilikuwa inakunjwa kama anavyokaa mtoto kwenye mfuko wa uzazi
Na sio warugulu wote wanafanya hvyo,mfano wale wa upande wa Mgeta ambako ukristo ndio umeshamiri zaidi sidhani kama wanafanya hivyo,hivyo hiyo inawezekana sio mila halisi ya kirugulu na ndio maana wa upande huo hawamtendei marehemu wao hivyo
 
Wana mtindo mmoja na Wazigua. Sema wazigua ufuo wa mwisho huwa wanakinga wanachanganya na maji ya kupikia chakula cha msibani. Ukienda msiba wa Wazigua ukila chakula ujue umekunywa uharo wa maiti

Wanasema ni kujenga ushirika wa kudumu na mpendwa wao. Mimi sioni tatio. shida ni kwamba, kwanini wawalishe wahudhuriaji wote?! Walipaswa kula peke yao kama ndugu wa marehemu.
Mkuu acha ujinga acha kuchafua kabila mbweha mmoja Wazigua wa wapi wanafanya huo ujinga😬😬
 
Na washuhudiaji wengi wanakuwepo pale binti akioshwa bora ungesema hata ni vijana kwa sababu nchi hii ina vijana wa hovyo ni wababa na familia zao wengine wanadindisha wakitoka hapo wanaadithiana

Na huu ni ukweli sisingizii mtu
Kwani akifa binti anakamuliwa na wanaume,sio na wanawake wenzake?
 
Maiti wa kiislamu Ni lazima akamuliwe mavi..ngama ..wakati wa kukoshwa.
Hii Ni Sheria sio sunna...

Kila dini Ina Sheria zake,kuna hata hao mabaniani wanao chomana Moto!
Ndio Sheria ya dini yao hiyo..
 
Mkuu upumbavu bado ni tatizo kubwa sana nchini.

Kwani mtu akifa na akazikwa akiwa na mavi huko mbinguni huyo mungu hataki mavi ama hakuna vyoo vya kunya huko mbinguni?

Je hayo mavi akifa anaenda nayo ama yanafukiwa tu ardhini? Kwa mfano mtu akimezwa na samaki na mavi yake, mungu anafanyaje ama anamkataa kwamba hajakamuliwa mavi? Ama akiliwa na mamba na mavi yake, je mungu anamkataa kwamba hajakamuliwa mavi?

Ama mtu akiungua na moto ama akilipuliwa na bomu akateketea kabisa ama akaenda na maji akafariki na mwili wake usipatikane, je mungu anawafanyaje watu wa hivyo, anawakataa kwamba hawakukamuliwa mavi?

Dini nyingine bwana, halafu unaambiwa hayo maelekezo yamendikwa na mungu ambae inasemekana ana akili na uwezo kuliko binadamu halafu anaandika uharo kama huo.

Dini+mila na desturi za kipumbavu zinaonyesha kabisa huyo mungu nae hana akili kabisa.
Hawa watu waliletewa dini wakmeza namazingira ya didni yasiyoendana na mazingira yao:
Kuosha kwa kumkamua marehemu: Hii ilitokana na mazingira ya waanzilishi wa dini ambapo kutokana na haliya hewa yao mwili ukiwa na bacteria wengi unaweza kuoza haraka, kinyesi kikiwa tumboni ni host wa bacteria.

Kuzika haraka pia ilitokana na mazingira ya joto ambapo mwili hauwezi kukaa mda mrefu na ukizingatia kuwa wakati huo hakukuwa na refridgeration technology
 
Mkuu upumbavu bado ni tatizo kubwa sana nchini.

Kwani mtu akifa na akazikwa akiwa na mavi huko mbinguni huyo mungu hataki mavi ama hakuna vyoo vya kunya huko mbinguni?

Je hayo mavi akifa anaenda nayo ama yanafukiwa tu ardhini? Kwa mfano mtu akimezwa na samaki na mavi yake, mungu anafanyaje ama anamkataa kwamba hajakamuliwa mavi? Ama akiliwa na mamba na mavi yake, je mungu anamkataa kwamba hajakamuliwa mavi?

Ama mtu akiungua na moto ama akilipuliwa na bomu akateketea kabisa ama akaenda na maji akafariki na mwili wake usipatikane, je mungu anawafanyaje watu wa hivyo, anawakataa kwamba hawakukamuliwa mavi?

Dini nyingine bwana, halafu unaambiwa hayo maelekezo yamendikwa na mungu ambae inasemekana ana akili na uwezo kuliko binadamu halafu anaandika uharo kama huo.

Dini+mila na desturi za kipumbavu zinaonyesha kabisa huyo mungu nae hana akili kabisa.
Wote hatumjui MUNGU lakini wewe Amin tu kuwa yupo
 
Naomba nichangie kidogo hapa.

Kwanza nitamke wazi mimi ni miongoni wa WAISLAM waliobahatika kusoma elimu zote mbili, yaani DINI na hii ya DUNIA.

Kabla ya kusogea mbele kuweka hoja au kuielezea hoja ya mleta mada, niseme wazi WAISLAM tuna changamoto ya kutosoma DINI yetu kwa kina mpaka tukajua kiini cha makatazo, zuio, kufanya kitu fulani, au ruhusa ya kufanya kitu fulani. Hivyo hoja yoyote inapoletwa haijibiwi kwa muktadha wa mtu kuelewa, bali tunajibu as if mtu amekashfu dini yetu. Nitoe mifano mitatu hapa ambapo WAISLAM karibia 80% hawajui mantiki ya kuzuia vitu vifuatavyo.
1. KAMARI
2. POMBE
3. KITIMOTO
Katika hivyo vitu hapo juu waislam wengi watashindwa kujibu kwa fact halisi ambazo Mwenyezi Mungu (S.W) alikusudia na msingi hasa wa kukataza.

Tuje sasa kwenye mada tajwa hapo juu. Hapa nitajibu kwa FACT, MAAGIZO, UZOEFU wangu, na Lengo kuu hasa la kufanya yote hayo.

1. KUOSHA MAITI NI FARDHI (LAZIMA KWA WAISLAM)

Muislam yeyote aliyafariki, kwa hali yoyote na maiti yake ikapatikana basi ni Sharti aoshwe, akafiniwe, aswaliwe.
A. KUOSHWA
B. KUKAFINIWA
C. KUSWALIWA
D. KUZIKWA

Kwa mtiririko huo, maiti lazima kwanza ioshwe, hapa tutaona mambo muhimu, kama anayetakiwa kuosha, namna ya kuosha, aina za uoshaji nk.

Sheria za Dini ziko wazi, kuwa MWANAUME ataoshwa na MWANAUME na MWANAMKE ataoshwa na MWANAMKE.

Lkn pia inaruhusiwa pasi na shida yoyote MUME akamuosha MKEWE au MKE akamuosha MUMEWE ni halali na inaruhusiwa kabisa na hapa nadhani sihitaji nguvu kubwa kuelezea kwann inaruhusiwa maana ushaona hao ni mke na mume hivyo hakuna ambacho hajakiona kutoka kwa mwenzake.

Kwenye Kuosha maiti, inatakiwa kwanza wale ndugu wa marehemu ndio wawe waoshaji, BABA, MAMA, KAKA, MJOMBA nk nk. Hii inatokana na sheria ambayo unatakiwa kuijua kuwa unapaswa kutunza siri yoyote juu ya maumbile yoyote ya marehemu kama vile kovu kubwa, majeraha, au kabda anatoa kinyesi nk nk. Hivyo sheria inataka kwanza ndugu ndio wawe waoshaji.
Lakn kama ndugu hawapo basi waislam wengine watatakiwa kumuosha.

Maiti inatakiwa iwe safi kabisa, na haitakiwi aina yoyote na najisi itokee, labda kwa kesi maalum kama ajali, ambapo mtu anavuja damu hata kama utamuosha mara zote saba.

Kama alikuwa chochote basi atakalishwa kidogo ili kuona kama kuna kinyesi kitatoka na kama kipo basi inashauriwa kusafisha, na ikumbukwe marehemu yeyote hana uwezo wa kucontrol matundo ya mwilini mwake hivyo, mkojo, kinyesi, damu nk huweza kutoka muda wowote. Hapana naweka kwenye mabano ili watu wengi waelewe dhana hii (PAMOJA NA VIPIMO VYA MADAKTARI KUWA MTU FULANI SASA NI MAREHEMU LKN KITU KINACHOONESHA WAZI KUWA KWELI MTU AMEFARIKI BASI NI HUU UTARATIBU WA KUMKALISHA NA KUONDOA UCHAFU ULIOPO MWILINI (KINYESI) KWANI NDIO UTHIBITISHO HALISI WA KUWA MTU HUYU HAYUKO HAI.)

Ikiwa mtu ameoshwa zaidi ya mara saba na bado anatoa kinyesi, mkojo au damu sehemu zenya matundu basi atazibwa na pamba sehemu hizo ili taratibu zingine za kukafini zifuate.

3. KAKAFINI ni kuvikwa sanda, kuveshwa sanda maiti, hiyo ndio kukafini, atavikwa sanda tayari kwa hatua ya kuswaliwa kisha KUZIKWA.

2. UFUO, kama alivyodai mleta mada kuwa hufukiwa ndani.

Ni kweli waislam lazima uwe na UFUO katika uoshaji wa maiti na hapa utaona aina kadhaa. Kuna wale ambao watachimba shimo sehemu ambayo maiti ile itaoshewa na maji, na uchafu wote kuwa directed kwenye shimo hilo kisha mara baada ya kuoshwa basi wafukia kama uchafu mwingine tu. Pia unaweza kutumia mchanga kuwekwa chini ya kitanda kinachotumia kuoshea maiti lengo likiwa ni lile lile kuwa mara baada ya kuosha basi ule uchafu ukachimbiwe sehemu husika.


4. Kama sehemu hiyo akiyefariki ni MWANAMKE na hakuna MWANAMKE yeyote eneo hilo na hakuna MUMEWE basi Maiti hiyo haitooshwa bali, waliopaswa kuosha yaan hao wanaume watatumia mchanga kama vile wanatawadha kisha watampaza marehemu yule kwenye viganya vyake, kisha kwenda kuswaliwa.
Na hiyo ipo kwa jinsia ya kiume kama hakuna wanaume basi utaratibu ndio huo huo.

Tuhitimishe hapa, kwa kuweka sawa kwann maiti inaoshwa, kwann waoshaji lazima wawe jinsia moja na marehemu isipokuwa kwa MUME na MKE kama ikibidi.

Maiti huoshwa ili kupata wasaa wa kumsafisha na uchafu wowote, kwani tunaambiwa ni lazima maiti hiyo iswaliwe, na huwezi kuswali bila usafi wowote au kuswali ukiwa na najisi, hivyo kuosha ni njia moja ya kupelekea uhalali wa ibada ya Swala ya maiti.

Kuondoa harufu kali ambayo hutokea kwa maiti hiyo, wakati mwingine maiti hutoa harufu mbaya hivyo kuosha hupunguza karaha miongoni kwa wazikaji.

Pia kwenye kuosha unaruhusiwa kutumia maji ya vuguvugu au baridi kutegemeana na aina ya maiti husika.

Kwa wanawake wenye MISUKO RASTA nk hufumuliwa nywele zao na husukwa pande mbili yaani njia mbili tu. Na wanaume mwenye Rasta, dread na nywele kubwa sana basi zitanyolewa wataoshwa vizuri na kukafiniwa.
Maiti pia hupakwa manukato ili kuondoa harufu mbaya.

Kwa ujumla wake, maiti itaoshwa sambasamba na kuondoa kinyesi chake, mkojo, damu, usaha kama upo nk.

Ni mafundisho ya DINI ya UISLAM. Kutoosha maiti basi waliopaswa kufanya hivyo wao watahesabika kuwa wamefanya dhambi na watawajibika mbele za Allah S.W.

AHSANTENI.
 
Ukisha_flush yale mavi yanaendelea kuwepo mule chooni chumbani!?
Hahahahaha, na kabla ya ku flush na maji yenyewe haya DAWASA au kwenu wapi wewe?

Ni vyema kuwa umekiri kuna shimo unajiwekea mwenyewe, au ni ndoo?

Sasa jifikirie, ipi bora, shimo la chini ya ardhi, uchafu unawekwa mule, mkimaliza kuiosha maiti, linafukiwa na panasakafiwa kama palivyokuwa zamani, na mashonde mnayo lala nayo kutwa kucha siku maji ya kigoma?

Halafu nyie wakuja huko kwenu hata vyoo hamvijui, mnakwenda kuchimba dawa tu. Mnataka kusema nini nyinyi? Mnasema Waluguru, semeni na nyinyi kwenu wapi mjiumbuwe wenyewe hapa.
 
Back
Top Bottom