Naomba nichangie kidogo hapa.
Kwanza nitamke wazi mimi ni miongoni wa WAISLAM waliobahatika kusoma elimu zote mbili, yaani DINI na hii ya DUNIA.
Kabla ya kusogea mbele kuweka hoja au kuielezea hoja ya mleta mada, niseme wazi WAISLAM tuna changamoto ya kutosoma DINI yetu kwa kina mpaka tukajua kiini cha makatazo, zuio, kufanya kitu fulani, au ruhusa ya kufanya kitu fulani. Hivyo hoja yoyote inapoletwa haijibiwi kwa muktadha wa mtu kuelewa, bali tunajibu as if mtu amekashfu dini yetu. Nitoe mifano mitatu hapa ambapo WAISLAM karibia 80% hawajui mantiki ya kuzuia vitu vifuatavyo.
1. KAMARI
2. POMBE
3. KITIMOTO
Katika hivyo vitu hapo juu waislam wengi watashindwa kujibu kwa fact halisi ambazo Mwenyezi Mungu (S.W) alikusudia na msingi hasa wa kukataza.
Tuje sasa kwenye mada tajwa hapo juu. Hapa nitajibu kwa FACT, MAAGIZO, UZOEFU wangu, na Lengo kuu hasa la kufanya yote hayo.
1. KUOSHA MAITI NI FARDHI (LAZIMA KWA WAISLAM)
Muislam yeyote aliyafariki, kwa hali yoyote na maiti yake ikapatikana basi ni Sharti aoshwe, akafiniwe, aswaliwe.
A. KUOSHWA
B. KUKAFINIWA
C. KUSWALIWA
D. KUZIKWA
Kwa mtiririko huo, maiti lazima kwanza ioshwe, hapa tutaona mambo muhimu, kama anayetakiwa kuosha, namna ya kuosha, aina za uoshaji nk.
Sheria za Dini ziko wazi, kuwa MWANAUME ataoshwa na MWANAUME na MWANAMKE ataoshwa na MWANAMKE.
Lkn pia inaruhusiwa pasi na shida yoyote MUME akamuosha MKEWE au MKE akamuosha MUMEWE ni halali na inaruhusiwa kabisa na hapa nadhani sihitaji nguvu kubwa kuelezea kwann inaruhusiwa maana ushaona hao ni mke na mume hivyo hakuna ambacho hajakiona kutoka kwa mwenzake.
Kwenye Kuosha maiti, inatakiwa kwanza wale ndugu wa marehemu ndio wawe waoshaji, BABA, MAMA, KAKA, MJOMBA nk nk. Hii inatokana na sheria ambayo unatakiwa kuijua kuwa unapaswa kutunza siri yoyote juu ya maumbile yoyote ya marehemu kama vile kovu kubwa, majeraha, au kabda anatoa kinyesi nk nk. Hivyo sheria inataka kwanza ndugu ndio wawe waoshaji.
Lakn kama ndugu hawapo basi waislam wengine watatakiwa kumuosha.
Maiti inatakiwa iwe safi kabisa, na haitakiwi aina yoyote na najisi itokee, labda kwa kesi maalum kama ajali, ambapo mtu anavuja damu hata kama utamuosha mara zote saba.
Kama alikuwa chochote basi atakalishwa kidogo ili kuona kama kuna kinyesi kitatoka na kama kipo basi inashauriwa kusafisha, na ikumbukwe marehemu yeyote hana uwezo wa kucontrol matundo ya mwilini mwake hivyo, mkojo, kinyesi, damu nk huweza kutoka muda wowote. Hapana naweka kwenye mabano ili watu wengi waelewe dhana hii (PAMOJA NA VIPIMO VYA MADAKTARI KUWA MTU FULANI SASA NI MAREHEMU LKN KITU KINACHOONESHA WAZI KUWA KWELI MTU AMEFARIKI BASI NI HUU UTARATIBU WA KUMKALISHA NA KUONDOA UCHAFU ULIOPO MWILINI (KINYESI) KWANI NDIO UTHIBITISHO HALISI WA KUWA MTU HUYU HAYUKO HAI.)
Ikiwa mtu ameoshwa zaidi ya mara saba na bado anatoa kinyesi, mkojo au damu sehemu zenya matundu basi atazibwa na pamba sehemu hizo ili taratibu zingine za kukafini zifuate.
3. KAKAFINI ni kuvikwa sanda, kuveshwa sanda maiti, hiyo ndio kukafini, atavikwa sanda tayari kwa hatua ya kuswaliwa kisha KUZIKWA.
2. UFUO, kama alivyodai mleta mada kuwa hufukiwa ndani.
Ni kweli waislam lazima uwe na UFUO katika uoshaji wa maiti na hapa utaona aina kadhaa. Kuna wale ambao watachimba shimo sehemu ambayo maiti ile itaoshewa na maji, na uchafu wote kuwa directed kwenye shimo hilo kisha mara baada ya kuoshwa basi wafukia kama uchafu mwingine tu. Pia unaweza kutumia mchanga kuwekwa chini ya kitanda kinachotumia kuoshea maiti lengo likiwa ni lile lile kuwa mara baada ya kuosha basi ule uchafu ukachimbiwe sehemu husika.
4. Kama sehemu hiyo akiyefariki ni MWANAMKE na hakuna MWANAMKE yeyote eneo hilo na hakuna MUMEWE basi Maiti hiyo haitooshwa bali, waliopaswa kuosha yaan hao wanaume watatumia mchanga kama vile wanatawadha kisha watampaza marehemu yule kwenye viganya vyake, kisha kwenda kuswaliwa.
Na hiyo ipo kwa jinsia ya kiume kama hakuna wanaume basi utaratibu ndio huo huo.
Tuhitimishe hapa, kwa kuweka sawa kwann maiti inaoshwa, kwann waoshaji lazima wawe jinsia moja na marehemu isipokuwa kwa MUME na MKE kama ikibidi.
Maiti huoshwa ili kupata wasaa wa kumsafisha na uchafu wowote, kwani tunaambiwa ni lazima maiti hiyo iswaliwe, na huwezi kuswali bila usafi wowote au kuswali ukiwa na najisi, hivyo kuosha ni njia moja ya kupelekea uhalali wa ibada ya Swala ya maiti.
Kuondoa harufu kali ambayo hutokea kwa maiti hiyo, wakati mwingine maiti hutoa harufu mbaya hivyo kuosha hupunguza karaha miongoni kwa wazikaji.
Pia kwenye kuosha unaruhusiwa kutumia maji ya vuguvugu au baridi kutegemeana na aina ya maiti husika.
Kwa wanawake wenye MISUKO RASTA nk hufumuliwa nywele zao na husukwa pande mbili yaani njia mbili tu. Na wanaume mwenye Rasta, dread na nywele kubwa sana basi zitanyolewa wataoshwa vizuri na kukafiniwa.
Maiti pia hupakwa manukato ili kuondoa harufu mbaya.
Kwa ujumla wake, maiti itaoshwa sambasamba na kuondoa kinyesi chake, mkojo, damu, usaha kama upo nk.
Ni mafundisho ya DINI ya UISLAM. Kutoosha maiti basi waliopaswa kufanya hivyo wao watahesabika kuwa wamefanya dhambi na watawajibika mbele za Allah S.W.
AHSANTENI.