Wamama wengi wa Afrika huwafundisha watoto kuwachukia ndugu wa upande wa baba. Mashangazi ni wachawi, bibi mzaa baba anaturoga ila MJOMBA NI MAMA

Wamama wengi wa Afrika huwafundisha watoto kuwachukia ndugu wa upande wa baba. Mashangazi ni wachawi, bibi mzaa baba anaturoga ila MJOMBA NI MAMA

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Familia nyingi sana za ki Afrika zina mpasuko mkubwa. Ndugu wa mume wakitembelea familia hufanyiwa vitimbi na vibweka vya kila aina.

Wakija dada wa baba wa mwenye nyumba watasimangwa kwa maneno mbalimbali kwamba wamekuja kuvunja ndoa, wameleta uchawi na mbaya zaidi inafikia wanakataliwa hata kuwabeba watoto na kuandaa chakula kwa hofu ya kurogwa.

Mama zetu hebu badilikeni aiseee
 
Kabsa aseee mimi ni mhanga wa hayo unayoyasema aseeee uyo shangazi kajua kutunyoosha mwanamama anafanya ad uchawi hadharani
 
Inahitaji utafiti....... Lkn kwenye familia nyingi utakuta ndugu upande wa Mke wanaishi bila shida... Wale wa upande wa mume huwa kasheshe kila siku mashitaka mpaka mume anaona isiwe tabu anawaondoa ndugu upande wake..
 
Aisee, nakumbuka jinsi ambavyo tulimtenga shangazi yetu kwa kumuhisi kuwa ni mchawi.

Tukiwa darasa la tatu tulienda kuishi kwake. Baba alikuwa masomoni nje ya nchi, na mama pia alikuwa nje kwa masomo.

Tukiwa kwa shangazi kwasababu ya kubadili hali ya hewa tulikuwa tukiumwa mara kwa mara.

Mama yetu mdogo akamtumia barua mama kuwa shangazi anaturoga ndio maana tunaumwa mara kwa mara, mpaka nilipokuwa mkubwa nikajua tulipandikiziwa chuki.

Kwa kweli nampenda sana shangazi yangu, licha ya kuwa sina uwezo nilihakikisha naikarabati nyumba yake.

Nimemjengea choo cha kukaa. Kutokana na utu uzima na umbo lake nene kuchuchimaa ni changamoto kwake.

Nyumba yake nimeiwekea tiles, madirisha ya kisasa na paa jipya.

Mungu anisamehe kwa kuyafanya yale yote mabaya niliyomfanyia
 
Inahitaji utafiti....... Lkn kwenye familia nyingi utakuta ndugu upande wa Mke wanaishi bila shida... Wale wa upande wa mume huwa kasheshe kila siku mashitaka mpaka mume anaona isiwe tabu anawaondoa ndugu upande wake..
Inasikitisha.
Ila kwa kweli wanawake tuna matatizo sana, hasa tukiwa ndio kina mama wenye nyumba hapa mjini
 
Wamama wengi wa kiafrica awajui au wanapwaya Sana juu ya malezi ya watoto, uwapandikizia Sana watoto negativity zaidi kwenye makuzi yao. Thus tunapata jamii mfu wasiowezza kujitambua kujisimamia.
 
Shangazi na mama ni mtu na wifi yake always mke na mawifi plus wakwe huwa haziivi pana bifu la asili la kugombea umiliki.

Wamemlea mtoto kwa tabu kwa kuunga unga leo mtoto kafanikiwa wanahisi mke ndo anaeffaidi jitihada zao. Mkeo nae ujiona ye ndo boss ndo mmiliki halali asiyepaswa kuchanganywa. Kia asili wanawake ni wabinafsi.
 
Nakumbuka utotoni Masahngazi walisingiziwa vitu vingi sana

Mama anakuchapa, ukileta mgomo unasikia kagome kwa shangazi yako huko sio hapa kwangu
Hahahaha mashangazi tunateseka sana, Mungu atatulipia.
 
Mambo mengine ni kweli mtoto anapandikizwa chuki lakini mengine watoto wanajionea wenyewe,
Sisi tulikua tukienda kwa bibi tunabaguliwa kabisa na tunajua, watoto wa wengine wale sisi tukifika ni kuosha vyombo vyao.
wakati mwingine mashangazi wanadiliki kusema mbele yetu wewe hautufananii utakua sio damu yetu.
Nakumbuka dada yangu wa kwanza alisoma kwa shida kwasababu alifeli la saba na mashangazi wakamshauri baba asimsomeshee kwasababu amefeli hana akili, mama akasimama akamsomesha na leo amekua msaada sana kwetu.
Mambo mengine mashangazi nao wanakosea kuingilia ndoa za kaka zao kama zao.

Mimi ni shangazi pia, kwa tuliyopitia najitahidi kua shangazi mzuri.
 
Back
Top Bottom