Chanzo kikubwa ni kuwa akina mama wanapoolewa katika koo za watu wengine wao ndio wanakuwa chanzo cha kuleta kelele ndani ya koo walizoolewamo (bado sina uhakika na tetesi hii)
Kuna baadhi ya wataalam niliohojiana nao walipata kuniambia kwamba tafiti za kisaikoloji inaonesha kwamba mtoto ni rahisi sana kuamini maneno ya mama kuliko ya baba. Yaaani mama akikwambia kuwa yule mke wa baba yako mdogo amenitukana na kuanzia leo msiende kwao, na kweli watoto watatembelea mkoa huo lakini hawataenda nyumbani kwa baba yao mdogo/mkubwa tofauti kabisa akiambiwa na baba yake.
USHAURI KWA WABABA WENZANGU: Msikubali wanawake mliowaoa wavunje undugu wenu kwa maana nyie mmetoka mbali zaidi tangia mpo wadogo huko kwenu kuliko hao wake zenu mliokutana nao ukubwani.