Wamarekani lile jiji la New York waliamua aisee!

Wamarekani lile jiji la New York waliamua aisee!

Halafu kwa jiji la Kinshasa kule DR Congo kwangu mimi binafsi Dar es Saalam bado tuko nyuma sana.
Kin la Belle (Kin the Beautiful)

Kinshasa mji ambao una Bendera yake na Seal yake, mji mzuri kwa muonekano wa majengo na mpangilio wa makazi Je! Dar es Salaam ina bendera yake na Seal yake km mji na mpangilio wa makazi je ?

Screenshot_20230522-201448.png

Bendera ya Kinshasa

Niliambiwa kwamba miji ya Congo zilikua ni Nchi zilizoamua kuunganishwa na P Lumumba Ila akawa na anapigwa Vita na wahasimu akiwemo Tshombe ambae alikua ana ushirika na Marekani pamoja na Waberigiji hata kifo Cha Lumumba Marekani na Waberigiji wamehusika maana walikua wanamsaidia Tshombe ambae alikua amejitangaza km rais wa Jimbo au mji wa Katanga kwa kipindi kile ilikua inachukuliwa km Nchi si Jimbo au mji
 
Daah umeongelea Helsinki (Finland) umenitamanisha sana mkuu, ni kati ya majiji ambayo huwa natamani sana nifike, pamoja na Dublin (Ireland) napo

Nakuunga mkono binafsi majiji ninayoona mazuri kwa North America na Europe ni New York (US), Toronto (Canada), London (UK), Oslo (Norway), Paris (France), Stockholm (Sweden), Geneva (Switzerland), Munich (Germany) et al

Baadhi nimefika baadhi nimeyaona kwenye picha na video za ndugu na jamaa zangu waliofika na waliopo huko, binafsi hii ndio passion yangu yani nataka nikikusanya hela za kutosha kila likizo ndefu ninayopata niwe naitumia kusafiri nchi mbalimbali duniani, sisi wengine bila kusafirisafiri hatuoni kama maisha yana maana yoyote
👌👌👌Aisee safi sana
 
Kuna jambo nimeamua kushea kidogo humu.

Kwa kazi yangu nashukuru Mungu nimetembea tembea kidogo katika majiji mengi makubwa duniani.

Nilipofika New York Marekani, aisee lile jiji ni zuri sana. Wiki mbili nilizokaa niliziona chache sana. Wenyeji wangu walinitembeza sana, nilienjoy mno, nilikuwa na wakati mzuri sana. (Naamini kuna siku nitarudi tena).

Nilimelitaja jiji la New York kuwa zuri sana nikilinganisha na majiji niliyowahi kufika ingawa yote sikuwahi kukaa zaidi ya mwezi. (Unaweza kupingana na mimi kwa majiji ambayo umewahi kufika mimi sijawahi)

Majiji yenyewe ni haya:

Afrika.
Bujumbura(Burundi), Nairobi, Kisii na Kisumu(Kenya), Blantyre, Karonga, Mzuzu, Zomba na Lilongwe(Malawi), Maputo, Cabo Delgado, Tete na Chimoio (Msumbiji), Luanda na Calulo (Angola), Kinshasa na Lubumbashi (DR Congo), Johannesburg((Afrika Kusini)

Ulaya
Frankfurt na Berlin (Ujerumani), London (England), Helsinki(Finland), Paris (Ufaransa)

Midlle East
Beirut (Lebanon)

Asia
Hon Kong na Beijing (China), Seoul (Korea Kusini), New Delhi na Mumbai (India)

Latin America
Huku sikufika katika nchi tano tu (Argentina, Paraguay, Uruguay, Chile na Venezuela) zingine zote nimefika

North Amerika
Marekani(New York)

Hitimisho langu, katika majiji yote hayo niliyofika mimi, kwakweli nakiri kabisa, New York ni JIJI haswa.

Halafu kwa jiji la Kinshasa kule DR Congo kwangu mimi binafsi Dar es Saalam bado tuko nyuma sana. Kabla hujafika ukisikia mambo ya vita ya Congo unaweza kudhani Kinshansa ni kajiji tu kahovyo, lakini aisee, nalo ni jiji kweli kweli.
Pambana ufike Singapore Mzee baba. Zile garden zake ni balaa
 
Back
Top Bottom