Wamasai Ngorongoro: Spika ataka 'aliyechukua clip' ashughulikiwe, taasisi zilizosajiliwa nchini kufata

Wamasai Ngorongoro: Spika ataka 'aliyechukua clip' ashughulikiwe, taasisi zilizosajiliwa nchini kufata

Hili suala ni gumu sababu wamasai wanadhani Ngorongoro ni Mali yaoo... hata kama wanafanya uharibifu na kuongeza idadi ya makazi hawaoni kama ni shida inabidi Serikali itumie nguvu sasa maana hawaelewi kabisa. Lakini kama unataka kuwahamisha wamasai ujenge hotel pia Serikali itazingua sana
 
Tunaomba huyu askari ajisalimishe Dodoma kwa Tulia kwanza.
IMG_7404.jpg
 
spika ameongea kitu cha maana sana. watu kama Tito magoti, maria sarungi, ole ngurumo na type zake zooote hizo, wanaichafua sana nchi na wanatamani hata masai mmoja tu afe ili wapate cha kuongea. wadhibitiwe mapema, sio afya kwa taifa.
Wakati Magufuli anawapuuza hao wajinga, nyie mlikuwa mnakata viuno humu mkimuita dikteta na mshamba!

Ngoja sasa waanze kuwatia vidole kwenye macho ndio mtajua hamjui.
 
Maridhiano ya KITAIFA NI MUHIMU SANA

Kwenye Giza Majoka yenye ndimi tatu za Moto huwa yanapita huko

CC Yercko Nyerere jasusi la KIGAMBONI
 
Makapi ya mwendazake yanasumbua Nchi
Mwendazake mtamsingizia hata waume zenu wakishindwa kusimamisha!

Huyo mamaenu alikuwa na nafasi ya kumuweka spika wake ila akampa tena huyo huyo sasa sijui mwendazake anaingiaje hapa
 
Watuonyeshe hizo clip tujue kama ni OG au fake
 
Leo Bungeni baada ya Waziri mkuu kuongelea video inayosambaa kwamba kuna mapigano yameanza Ngorongoro, Spika Tulia Ackoson ametoa maoni yake na kutaka mhusika ashughulikiwe na taasisi zilizosajiliwa nchini zifate.

======

Spika: Tupo kwenye vita ya kiuchumi na nchi zingine, tukiwaacha hawa wakaendelea kutumika, wale waliopo hapa nchini sheria zetu zichukue mkondo wake.

Kama mtu anafanya upotoshaji kama huyo ambae amechukua hiyo clip na inajulikana ameichukulia wapi, tunaweza kuanza na huyo halafu wengine watafata ikiwa ni pamoja na hizi taasisi ambazo zimesajiliwa hapa nchini kwetu tukifikiri kwamba zina lengo jema na sisi hapa nchini lakini kama zinafanya jambo tofauti pia sheria zichukue mkondo wake.

View attachment 2256084
Waliochukua clip hawa hapa,

53C4BA38-F780-4AA1-BC2E-9685678BA26E.jpeg
 
Back
Top Bottom