MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Sheria ya kumtambua Rais kama custodian wa Ardhi yote ibadilishwe,Raia akimiliki Ardhi yake iwe ni yake mpaka Dahari.Ardhi ni ya nani?
Tunakodisha kwa nani?
Kuhama kwa kuridhia ni sawa, lakini kukataa kuhamishwa kama ng'ombe ni akili. Wanachofanya Wamasai ni kuutetea utu wao.
Kwa sababu watawala wameshindwa kutumia akili kukabiliana na changamoto husika wanakimbilia kutumia maguvu, jambo ambalo halipaswi kuwepo katika karne hii.
Mkuu, ninaloweza kukubaliana nawe ni moja tu, SHERIA IBADILISHWE.Sheria ya kumtambua Rais kama custodian wa Ardhi yote ibadilishwe,Raia akimiliki Ardhi yake iwe ni yake mpaka Dahari.
Wamehamishwa kama Ng'ombe kivipi?
Wanapewa Nyumba yenye Ardhi ya kutosha,shamba la kilimo,eneo la malisho,Huduma ya Maji,Hospitali,shule zimejengwa na Fedha wamelipwa!
Ndio Ng'ombe anavyohamishwa hivyo?
Kama kuna kabila lilistahili fidia lakini halikupewa fidia, ni ujumbe kuwa hilo kabila lina watu wengi wasiojitambua. Wanaweza kuburuzwa na mtu yeyote hata kama wana haki ya kutoburuzwa, maadam tu huyo mtu ana "cheo".Wamasai wahame tu. Walishaanza kujenga maghorofa Ngorongoro. Hiyo hifadhi ina manufaa kwa watanzania wote na sio wamasai tu. Fidia wanayopewa hakuna kabila lingine liliwahi kupewa. Serikali isiwachekee.
Wakubwa hawanufaiki na nini Nchi hii?Mkuu, ninaloweza kukubaliana nawe ni moja tu, SHERIA IBADILISHWE.
Suala la kujengewa nyumba na hospital si hoja. Kwa nchi zilizoendelea wanyama Wana hospital Bora kuzidi za nchi nyingi za Kusini mwa jangwa la Sahara.
Hata nilipoenda Mwika mkoani Kilimanjaro, nilimkuta mfugaji aliyemjengea ng'ombe wake bafu. La mkulima wa kawaida tena wa kijijini asiye na Elimu ya darasani aliweza kufanya hivyo, je kwa wafugaji walioelimika?
Serikali unakosea sana kutumia maguvu badala ya nguvu ya ushawishi. Ukiona inatumia maguvu kwa mambo kama hayo ujue kuna wakubwa wanaonufaika na hilo linalotekelezwa.
Je, unaweza kuthibitisha kwamba zoezi la Uthamini na uhakiki wa Mali zao ulifanyika lini?Hata hao wanalipwa fidia ya nyumba, ardhi, na hela juu, hebu watoke hapo, wasituletee drama za mashuka
Kwa bahati mbaya sijawahi fila Ngorongoro japo nilikulia Arusha. Sipajui zaidi ya nilivyoelezwa. Lakini hata kama kulikuwa na kulazimika wa kuhamishwa, ingetumika bottom up approach na siyo hiyo iliyotumiwa na Serikali.Wakubwa hawanufaiki na nini Nchi hii?
Hoja yangu Mimi ni Moja tu,Baada ya miaka 30 hao Raia na Mifugo Yao itakuwa imefika idadi Gani?
Maendeleo ya makazi ya watu hao yatahitaji eneo kubwa Kiasi Gani?
Wanyama pia Wana Haki zao,wataenda wapi?
Kama vipi tukubaliane hilo neno "Hifadhi" lifutwe,ibaki Wilaya tu.
Huwezi kuita eneo hifadhi ya wanyama,na ndani yake Kuna Mji mkubwa wanaishi Watu.
Hawakulazimishwa! Waliyauza kwa hiari yao kwa manufaa yao. Ni tofauti na Wamasai wa Ngorongoro wanaohamishwa kwa kulazimishwa kwa hasara yao kwa maslahi ya watawala wa Tanganyika na matajiri wa Uarabuni.
Ardhi ni ya nani?
Tunakodisha kwa nani?
Kuhama kwa kuridhia ni sawa, lakini kukataa kuhamishwa kama ng'ombe ni akili. Wanachofanya Wamasai ni kuutetea utu wao.
Kwa sababu watawala wameshindwa kutumia akili kukabiliana na changamoto husika wanakimbilia kutumia maguvu, jambo ambalo halipaswi kuwepo katika karne hii.
Kinachofanyika Ngorongoro ni kwa manufaa ya Waarabu!Kasome na kujielimisha kuhusu kuhamisha au kununua ardhi kwa lazima kutoka kwa wananchi kwa manufaa ya umma.
UNESCO ndio walioipandisha hadhi hiyo Hifadhi miaka ya sabini,ikawa World heritage site.Kwa bahati mbaya sijawahi fila Ngorongoro japo nilikulia Arusha. Sipajui zaidi ya nilivyoelezwa. Lakini hata kama kulikuwa na kulazimika wa kuhamishwa, ingetumika bottom up approach na siyo hiyo iliyotumiwa na Serikali.
Mara zote mashirika ya Kimataifa yamekuwa mstari wa mbele kuutetea hifadhi ya mazingira, lakini safari hii Serikali ndiyo inayoonekana inajali mazingira kuzidi hayo mashirika yanauotoa hela ya kuhifadhi wanyama pori na mazingira kwa ujumla. Huoni hapo kuna "walakini?"
Kama mpaka mashirika ya Kimataifa yanaziodoa Tanzania kwa uamuzi wake, huoni kuwa hapo kuna kitu kisicho sawa?
Tofautisha KUWASOGEZA na KUWAHAMISHA.Hivi wazaramo wangekataa kuachia mitaa ya posta, kariakoo, magomeni, hii Dar tunayoijua ingekuwepo?
Andika tu kwa kiswahili ndugu. Kiingereza hukiwezi.
Kajielimishe kuhusu mazoezi yanayoendelea huko.Kinachofanyika Ngorongoro ni kwa manufaa ya Waarabu!
Kama wanakuja kufanya uwekezaji ambao utakuwa himilivu kwa uhifadhi basi na waje tu,kuliko hivi watu wanajenga Mitaa na kuzaliana hifadhini.Kinachofanyika Ngorongoro ni kwa manufaa ya Waarabu!
JF ni darasa huru! Iweke hiyo Elimu hapa japo kwa ufupi kwa manufaa ya wengi.Jibu hoja acha kurukaruka
Kajielimishe kuhusu mazoezi yanayoendelea huko.
Nakusihi kwa heshima na taadhima ili usiendelee kujiaibisha.
Ninachofahamu ni kuwa:Kama wanakuja kufanya uwekezaji ambao utakuwa himilivu kwa uhifadhi basi na waje tu,kuliko hivi watu wanajenga Mitaa na kuzaliana hifadhini.
Mtu kuliwa na Simba huko hifadhini ni msiba wa Kawaida,kama mvuvi kufia baharini!
Maisha Gani hayo!
JF ni darasa huru! Iweke hiyo Elimu hapa japo kwa ufupi kwa manufaa ya wengi.
Wewe!!Ninachofahamu ni kuwa:
1. Hakuna mmasai aliyewahi kushambuliwa na Simba Ngorongoro
2. Uwepo wa Wamasai hifadhini ni moja ya vivutio vya utalii Ngorongoro!