Pre GE2025 Wamasai wa Ngorongoro watoa tamko kunyang'anywa haki ya kupiga kura 2024 na 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wamasai wahame tu. Walishaanza kujenga maghorofa Ngorongoro. Hiyo hifadhi ina manufaa kwa watanzania wote na sio wamasai tu. Fidia wanayopewa hakuna kabila lingine liliwahi kupewa. Serikali isiwachekee.
 
Ardhi ni ya nani?
Tunakodisha kwa nani?

Kuhama kwa kuridhia ni sawa, lakini kukataa kuhamishwa kama ng'ombe ni akili. Wanachofanya Wamasai ni kuutetea utu wao.

Kwa sababu watawala wameshindwa kutumia akili kukabiliana na changamoto husika wanakimbilia kutumia maguvu, jambo ambalo halipaswi kuwepo katika karne hii.
Sheria ya kumtambua Rais kama custodian wa Ardhi yote ibadilishwe,Raia akimiliki Ardhi yake iwe ni yake mpaka Dahari.
Wamehamishwa kama Ng'ombe kivipi?
Wanapewa Nyumba yenye Ardhi ya kutosha,shamba la kilimo,eneo la malisho,Huduma ya Maji,Hospitali,shule zimejengwa na Fedha wamelipwa!
Ndio Ng'ombe anavyohamishwa hivyo?
 
Mkuu, ninaloweza kukubaliana nawe ni moja tu, SHERIA IBADILISHWE.

Suala la kujengewa nyumba na hospital si hoja. Kwa nchi zilizoendelea wanyama Wana hospital Bora kuzidi za nchi nyingi za Kusini mwa jangwa la Sahara.

Hata nilipoenda Mwika mkoani Kilimanjaro, nilimkuta mfugaji aliyemjengea ng'ombe wake bafu. La mkulima wa kawaida tena wa kijijini asiye na Elimu ya darasani aliweza kufanya hivyo, je kwa wafugaji walioelimika?

Serikali unakosea sana kutumia maguvu badala ya nguvu ya ushawishi. Ukiona inatumia maguvu kwa mambo kama hayo ujue kuna wakubwa wanaonufaika na hilo linalotekelezwa.
 
Wamasai wahame tu. Walishaanza kujenga maghorofa Ngorongoro. Hiyo hifadhi ina manufaa kwa watanzania wote na sio wamasai tu. Fidia wanayopewa hakuna kabila lingine liliwahi kupewa. Serikali isiwachekee.
Kama kuna kabila lilistahili fidia lakini halikupewa fidia, ni ujumbe kuwa hilo kabila lina watu wengi wasiojitambua. Wanaweza kuburuzwa na mtu yeyote hata kama wana haki ya kutoburuzwa, maadam tu huyo mtu ana "cheo".
 
Mkuu, ninaloweza kukubaliana nawe ni moja tu, SHERIA IBADILISHWE.

Suala la kujengewa nyumba na hospital si hoja. Kwa nchi zilizoendelea wanyama Wana hospital Bora kuzidi za nchi nyingi za Kusini mwa jangwa la Sahara.

Hata nilipoenda Mwika mkoani Kilimanjaro, nilimkuta mfugaji aliyemjengea ng'ombe wake bafu. La mkulima wa kawaida tena wa kijijini asiye na Elimu ya darasani aliweza kufanya hivyo, je kwa wafugaji walioelimika?

Serikali unakosea sana kutumia maguvu badala ya nguvu ya ushawishi. Ukiona inatumia maguvu kwa mambo kama hayo ujue kuna wakubwa wanaonufaika na hilo linalotekelezwa.
Wakubwa hawanufaiki na nini Nchi hii?
Hoja yangu Mimi ni Moja tu,Baada ya miaka 30 hao Raia na Mifugo Yao itakuwa imefika idadi Gani?
Maendeleo ya makazi ya watu hao yatahitaji eneo kubwa Kiasi Gani?
Wanyama pia Wana Haki zao,wataenda wapi?
Kama vipi tukubaliane hilo neno "Hifadhi" lifutwe,ibaki Wilaya tu.
Huwezi kuita eneo hifadhi ya wanyama,na ndani yake Kuna Mji mkubwa wanaishi Watu.
 
Kwa bahati mbaya sijawahi fila Ngorongoro japo nilikulia Arusha. Sipajui zaidi ya nilivyoelezwa. Lakini hata kama kulikuwa na kulazimika wa kuhamishwa, ingetumika bottom up approach na siyo hiyo iliyotumiwa na Serikali.

Mara zote mashirika ya Kimataifa yamekuwa mstari wa mbele kuutetea hifadhi ya mazingira, lakini safari hii Serikali ndiyo inayoonekana inajali mazingira kuzidi hayo mashirika yanauotoa hela ya kuhifadhi wanyama pori na mazingira kwa ujumla. Huoni hapo kuna "walakini?"

Kama mpaka mashirika ya Kimataifa yanaizodoa Tanzania kwa uamuzi wake, huoni kuwa hapo kuna kitu hakipo sawa?
 
Hawakulazimishwa! Waliyauza kwa hiari yao kwa manufaa yao. Ni tofauti na Wamasai wa Ngorongoro wanaohamishwa kwa kulazimishwa kwa hasara yao kwa maslahi ya watawala wa Tanganyika na matajiri wa Uarabuni.

Na kule kwenye gas ntwala?
 
Ardhi ni ya nani?
Tunakodisha kwa nani?

Kuhama kwa kuridhia ni sawa, lakini kukataa kuhamishwa kama ng'ombe ni akili. Wanachofanya Wamasai ni kuutetea utu wao.

Kwa sababu watawala wameshindwa kutumia akili kukabiliana na changamoto husika wanakimbilia kutumia maguvu, jambo ambalo halipaswi kuwepo katika karne hii.

Kasome na kujielimisha kuhusu kuhamisha au kununua ardhi kwa lazima kutoka kwa wananchi kwa manufaa ya umma.
 
Kwa bahati mbaya sijawahi fila Ngorongoro japo nilikulia Arusha. Sipajui zaidi ya nilivyoelezwa. Lakini hata kama kulikuwa na kulazimika wa kuhamishwa, ingetumika bottom up approach na siyo hiyo iliyotumiwa na Serikali.

Mara zote mashirika ya Kimataifa yamekuwa mstari wa mbele kuutetea hifadhi ya mazingira, lakini safari hii Serikali ndiyo inayoonekana inajali mazingira kuzidi hayo mashirika yanauotoa hela ya kuhifadhi wanyama pori na mazingira kwa ujumla. Huoni hapo kuna "walakini?"

Kama mpaka mashirika ya Kimataifa yanaziodoa Tanzania kwa uamuzi wake, huoni kuwa hapo kuna kitu kisicho sawa?
UNESCO ndio walioipandisha hadhi hiyo Hifadhi miaka ya sabini,ikawa World heritage site.
Wao UNESCO ndio waliosema kuwa Ili hifadhi hii iendelee kuwepo wakazi wasizidi 25000,na Idadi ya mifugo isiyozidi 50000!
Hiyo idadi ilishapita miaka mingi lakini kwa unafiki wetu Watanganyika na Viongozi kuogopa maneno kama haya waliwanyamazia wamasaai.
Ilikuwa suala muda tu Wamasaai kuhama humo hifadhini.
Muda umefika waondoke,kama fidia waliyopewa ni ndogo waende Mahakamani!
Sio kusema tu sisi hatutaki kuondoka,hawataki wao kama kina nani?
 
Kama wanakuja kufanya uwekezaji ambao utakuwa himilivu kwa uhifadhi basi na waje tu,kuliko hivi watu wanajenga Mitaa na kuzaliana hifadhini.
Mtu kuliwa na Simba huko hifadhini ni msiba wa Kawaida,kama mvuvi kufia baharini!
Maisha Gani hayo!
Ninachofahamu ni kuwa:
1. Hakuna mmasai aliyewahi kushambuliwa na Simba Ngorongoro
2. Uwepo wa Wamasai hifadhini ni moja ya vivutio vya utalii Ngorongoro!
 
Wewe!!
Hilo la watu kushambuliwa na wanyama wakali ushahidi upo.
Hilo la Watu na wanyama kuishi pamoja kweli ni kivutio,lakini wingi wa watu,mifugo Yao na maendeleo Yao sio rafiki Tena kwa Hifadhi!
 
Back
Top Bottom