Wamiliki shule za EMs waumizwa na mtaala Mpya. Wazazi wengi sasa wanawatoa watoto Wao shule za EMs kiwarejesha Kayumba

Unazungumzia Ems hizi hizi ambazo walimu wanalipwa laki 2 Kwa mwezi na wana hama hama shule Kwa sababu ya kutolipwa Kwa wakati?

Zipo EMS nyingi ambazo, hazipo hivyo na huo mtazamo wako, zipo na standard na kikubwa kwao ni Elimu na Ada yako tu.

Hakuna justification yeyote ya kufananisha hizi Kayumba na EMS, tukisema tupange shule za Kayumba 100 Vs EMs 100 bado hizo Kayumba 300 zinazoweza kuleta vijana wazuri haiwezi kuzidi 5 na hizo EMs unaweza kuzipata hata 80.

Tunapaswa tupiganie Mapinduzi ya Elimu katika nchi yetu ili standard ya Elimu iendane na dunia ya sasa na iwe level moja shule zote.
Tukianza haya mashindano ilihali kiwango cha Elimu kipo chini hasa kwenye hizo Kayumba hatuwezi kufika popote.

Hebu nitajie Kayumba unayoweza kufananisha na Feza, Ahmes, kifungiro, St Anthony, Kaiziregi ya kipindi kile, Almuntaziri, Mzizima, St Francis, Rozimini, St christina nk.
 


You have got a very little understanding about children pyschology.


1. Watoto hupenda michezo.

2. Watoto huenda shuleni kucheza.

3.Watoto huenjoy zaidi wanapokuwa na watoto wenzao wengi.


Shule za Kayumba chumba kimoja cha darasa kina wanafunzi Sabini .


Ems darasa Lina watoto wanane.

Yani mtoto akatae darasa lenye wanafunzi I 70 ambao ataenda kucheza michezo mingi ila akubali darasa lenye watoto wanane ambako ataenda kuwa bored?
 
According to Kingwendu
 
Kwanza hakuna umuhimu wa elimu, sio English Medium wala kayumba wote kwa asilimia kubwa wanapoteza muda mwingi wa maisha yao kujifunza vitu ambavyo havina mchango wowote kwenye maisha yao bora watoto wangejivunza kilimo, ufugaji na ujasiriamali
Exactly, wajanja wametujia na vitu vyao wametulisha ujinga kuwa ndo maendeleo, tumeacha yetu yote tunakimbilia wanavyoviita vya kisasa na tumegeuzwa soko lao la kudumu,,,,
But ukikaa ukiangalia hivyo vitu vyote havikusaidii kitu zaidi ya kukufanya uwe mtumwa wao.
Badala ya kuishi sasa tunapigania maisha..
 
Exactly, wajanja wametujia na vitu vyao wametulisha ujinga kuwa ndo maendeleo, tumeacha yetu yote tunakimbilia vwanavyoviita vya kisasa na wametugeuza soko lao la kudumu,,,,
Badala ya kuishi sasa tunapigania maisha..
100,% Fact.

Halafu elimu inapaswa kuwa huduma na Sio biashara.

Mzazi wa kitanzania anafurahia kabisa jinsi wamiliki wa shule za EMs wanavyo mfanya mtoto wake kama bidhaa.
 

Kwani huko EMS hawachezi?.

Unafikiri kucheza bila mipango wala uangalizi nako ni sawa?.

Mbona Africa ni masikini sasa na watu wake tunaonekana dunia ilihali mashuleni darasani tulikuwa zaidi ya 100 kucheza muda wote wakati China watoto wanakula, wanalala na muda kidogo wakucheza then practical classes nk. Mbona hao wachina wako mbali na sisi tumebaki kama mazombie?..

Binafsi ni muumini wa ELIMU bora Kwa wote, mfumo hauko sawa uboreshwe uwe sawa na standard ya Elimu ifanane halafu uone kama kuna atakayehangaika kwenda huko EMS.
 
Ushauri wangu wa bure wahi hospitali ya vichaa mirembe hali mbaya kichwani kwako unahitaji kwenda matibabu hospitali ya mirembe

Kwa hili niko serious
 
100,% Fact.

Halafu elimu inapaswa kuwa huduma na Sio biashara.

Mzazi wa kitanzania anafurahia kabisa jinsi wamiliki wa shule za EMs wanavyo mfanya mtoto wake kama bidhaa.

Elimu inapaswa kuwa huduma sio biashara, NAKUBALIANA NA WEWE.

Imekuwa biashara baada ya watu kuanza kutapatapa baada ya wenye mamlaka kushindwa kuset mfumo Bora wa Elimu kwenye public school na kuruhusu Elimu iwe biashara.
 
Tumeambiwe tuitafute Elimu mpaka Uchina.

Kama unaona sio sawa kuhakikisha mwanao anapata Elimu kwa gharama yeyote basi muachishe tu shule akae nyumbani.
 
Walikurupuka kuanzisha shule hizo, hawaku focus hali itakuaje miaka ya mbeleni. Wanaweza kufanya enterprises kubadili biashara kwenye hayo majengo waliyoyafanya shule.
 
Walimu wa shule za Kayumba mna tabu sana, sasa umeandika kitu gani? Ushahidi uko wapi? Huo wingi wa watoto wanaohamia uko mtaani kwako tu? Mwalim tueleze huo mtaala mpya umeathili nini hizo shule mpaka wazazi wawahamishe watoto?
 
Walimu wa shule za Kayumba mna tabu sana, sasa umeandika kitu gani? Ushahidi uko wapi? Huo wingi wa watoto wanaohamia uko mtaani kwako tu? Mwalim tueleze huo mtaala mpya umeathili nini hizo shule mpaka wazazi wawahamishe watoto?
Waongo tu!mtaala mpya unaweza tekelezwa na shule za private walau wanaweza kununua hata hivyo vitendea kazi kuliko huko serikalini
 
Acha Urongo wewe!kwa hiyo huko shule za serikali ndio kuna maajabu gani?mwalimu mkuu mwenyewe hata laptop hana
 
😭😭😭😭
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…