Nangu Nyau
JF-Expert Member
- Jul 1, 2022
- 5,015
- 14,139
Unazungumzia Ems hizi hizi ambazo walimu wanalipwa laki 2 Kwa mwezi na wana hama hama shule Kwa sababu ya kutolipwa Kwa wakati?
Zipo EMS nyingi ambazo, hazipo hivyo na huo mtazamo wako, zipo na standard na kikubwa kwao ni Elimu na Ada yako tu.
Hakuna justification yeyote ya kufananisha hizi Kayumba na EMS, tukisema tupange shule za Kayumba 100 Vs EMs 100 bado hizo Kayumba 300 zinazoweza kuleta vijana wazuri haiwezi kuzidi 5 na hizo EMs unaweza kuzipata hata 80.
Tunapaswa tupiganie Mapinduzi ya Elimu katika nchi yetu ili standard ya Elimu iendane na dunia ya sasa na iwe level moja shule zote.
Tukianza haya mashindano ilihali kiwango cha Elimu kipo chini hasa kwenye hizo Kayumba hatuwezi kufika popote.
Hebu nitajie Kayumba unayoweza kufananisha na Feza, Ahmes, kifungiro, St Anthony, Kaiziregi ya kipindi kile, Almuntaziri, Mzizima, St Francis, Rozimini, St christina nk.