Siku moja Moshi mjini mitaa ya Majengo nilichukua room kwenye lodge moja, 20k. Nilipoingia tu nikafunga mlango wa room kwa funguo, nikavua nguo direct kuoga bafuni. Huko bafuni nililazimika kurudishia mlango maana bafu ni dogo sana. Ile nafunga mlango nikasikia kitu kinaanguka upande wa pili wa mlango (upande wa chumbani). Sikujali nikaendelea kuoga.
Nimemaliza kuoga nafungua mlango haufunguki. Kumbe handle ya kitasa upande wa nje na kile kijichuma kinaunganisha handles na kitasa ndio vinedondoka.
Niliita wahudumu kwa nguvu sana ila wasisikie mpaka koo likauma na matusi yote hapo nimeshamaliza, na hakuna hata mteja mwingine room jirani anisikie awaambie. Wamekuja baada ya nusu saa hivi ila hawawezi kuingia chumbani kwangu kwani nimefunga. Funguo za akiba hawana anazo boss mwenye guest house. Boss amepigiwa yupo mbali, shambani. Alikuja baada ya kama 3hrs hivi. Muda wote huo nipo chooni tu.
Walipofungua nikatoka. Jicho nililowakata wakaelewa namaanisha nini. Wakanirudishia hela yangu bila kusema chochote nikaondoka kutafuta lodge nyingine.
Ulikua unaoga, unakauka, unarudia tena kuoga hivo hivo zoezi likawa endelevu