Wamiliki wa lodge kuweni serious


Ulikua unaoga, unakauka, unarudia tena kuoga hivo hivo zoezi likawa endelevu
 
Kahama, mbinga, kasulu, nyakanazi, kibondo, sumbawanga, babati, singida, iringa, morogoro, mbeya, mbalizi, newala, bariadi, ngara, biharamuro, muleba, karagwe, mutukula, mpanda, kigoma mjini, manyoni, nzega, igunga, gairo, kibaigwa, tandahimba, Arusha, Mwanza, ngudu, sengerema, tukuyu, mlowo, vwawa, chimala, songea, uvinza, na maeneo mengine mengi ya mikoani chumba cha tsh.25000 hadi 30000 kwa dar unakipata kwa 60000 hadi 100000 na kinakua na hadhi ileile tena muda mwingine kinakua bora zaidi, kwa uzoefu wangu eneo lolote nikifika natafuta lodge au hotel mpya mpya ndio nafikia hapo maana zile zenye majina na za muda mrefu unakuta zimechoka sana hivo sio bora kwa sababu hazina maboresho, kwa mfano hotel au lodge au guest house lazima ifanyiwe ukarabati mdogo kila mara inapotokea kuanzia mfumo wa maji, umeme, na kadhalika lakini lazima kukagua vitanda, kubadili mashuka kila baada ya muda kuangalia vitu kama AC , feni kama zinafanya kazi imara, vitanda walau kukaza kila mara na usafishaji wa chumba inatakiwa ufanyike chumba kizima wengine unakuta chini ya kitanda pachafu au nyuma ya kitanda vumbi, madirisha lazima yafutwe kila mara, ubadilishaji wa mashuka lazima uwe na pea tatu za shuka kwa kila chumba na foronya pea tatu, lakini pia taulo lazima uwe na pea mbili,kila chumba,
 
Halafu kwa wamiliki wa lodges na hotel jitahidi kufunga kamera za usalama kwenye jengo lako hua zinasaidia sana wakati mwingine hasa nje, mapokezi, kwenye korido za kuingia vyumbani, na kila mgeni aandike jina lake halisi either aoneshe kitambulisho au kwa raia wa kigeni lazima akuoneshe hati yake ya kusafiria ili unakili namba zake kwa ufasaha,
 
Kama jengo linaeneo kubwa jitahidi ujenge fence na parking za nje na ndani ziwe bora na sio mbaya ukitenga eneo moja wapo la kupumzikia wateja kijumba cha msonge kidogo, lakini pia jitahidi sana tv za vyumbani uziweke uelekeo sahihi ili mteja asisumbuke kuona screen [emoji342]
 
Room haitakiwi kua na makolokolo mengi yasio na umuhimu, na kwa wamiliki wa hotels na lodges ni muhimu sana kuweka vyoo aina zote japo wateja wengi hupendelea vyoo vya kuchuchumaa vinaweza kua vingi na vya kukaa baadhi na kujitahidi kubadilisha kila vinapochakaa
 
Lakini pia kwenye usafi, mashuka yakifuliwa hapo yakunjwe na kunyooshwa vyema, sabuni za vyooni na air fresh za vyumbani za test tofauti tofauti kama apple, orange, vanila na kadhalika pia usisahau kufanya famigation kila baada ya muda fulani ili kuua wadudu warukao na watambaao, kwenye jengo lako, muhimu sana kutenga chumba kwa ajili ya kunyoshea nguo na ubora wa huduma za ufuaji wa nguo za wateja wetu
 
Wateja wengine hupendelea lodge tulivu, ni vyema usiweke bar, unaweza kuuza hapo vitu kama juice za boksi, soda aina fulani na maji makubwa na madogo ili kwa vitu kama hivo mteja asisumbuke sana bila kusahau condom, walau chumbani kasabuni na kamswaki kadogo viwepo ukiona couple vimiswaki viwili wapatie, na chooni toilet paper zisikose, lakini unaweza kuuza counter ped za dharura wanwake wengine huanza siku zao ghafra hivo huduma iwepo
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ukifanya hivyo wataojielewa tu ndo watakuja, wasiojielewa hutawaona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…