Ingekuwa Uislamu unakumbatia elimu ya kisasa au Kikoloni, leo hii ungekuta karibu kila msikiti una taasisi rasmi ya kutoa elimu dunia, kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu.
Zan...
Sikulaumu.
Huijui historia ya Waislam na juhudi yao katika elimu.
Soma hapo chini niliyoandika katika kitabu cha Abdul Sykes kuhusu suala la elimu:
Mkutano wa Kwanza wa Waislam (Muslim Congress), 1962
Baada ya uhuru kupatikana mwaka 1961 Waislam waliamini kuwa hali yao ya baadae katika serikali huru itakuwa nzuri.
Mwaka 1962 ukaitishwa mkutano wa Waislam wa nchi nzima kujadili nafasi ya Uislam katika Tanganyika huru.
Taasisi zifuatazo zilihudhuria mkutano huo: East African Muslim Welfare Society (EAMWS), Daawat Islamiyya, Jamiatul Islamiya fi Tanganyika, Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na Muslim Education Union.
Mkutano huu ulikubaliana pamoja na mambo mengine, umuhimu wa kuanzisha idara ya elimu chini ya EAMWS.
Waislam hawakusubiri serikali itimize ahadi yake ya kurekebisha upogo uliokuwepo wa elimu kati ya Waislam na Wakristo.
Waislam walianzisha mipango yao wenyewe ili isaidiane na juhudi ya serikali.
Mipango ikatayarishwa ya kujenga shule Tanganyika nzima na mwishowe kujenga Chuo Kikuu cha kwanza kwa Waislam katika Afrika ya Mashariki.
Mkutano ukamchagua Tewa Said Tewa waziri wa serikali, mwanasiasa wa TAA na mmoja wa wale wazalendo 17 walioanzisha TANU kuwa mwenyekiti wa EAMWS kwa upande wa Tanganyika.
Huu ndiyo ukawa mwanzo wa uadui kati ya Waislam na serikali.
Uelewano uliodumu wakati wa kudai uhuru ukaanza kutoweka na siasa zikachukua sura mpya ya uhasama, kutoaminiana na kutafutana.
Kisa cha hali hii mpya ikiwa ni sababu ya Waislam kutaka kuondoa hali ya kikoloni iliyowakandamiza kwa miaka mingi.
Waislam waliona kuwa hili lilikuwa ni jambo lisilokuwa na pingamizi kufanyika.
Uhuru ili uwe na maana ni lazima Waislam wajitoe ndani ya unyonge waliogubikwa na wakoloni.
Kwa upande wa serikali hali hii ilisababisha hofu kubwa.''
(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes)
Ukitaka kusoma zaidi kuhusu tatizo hili ingia: